Zitto Kabwe vs Prof. Kitila Mkumbo juu ya ujenzi wa SGR

Zitto Kabwe vs Prof. Kitila Mkumbo juu ya ujenzi wa SGR

Sio kama itatokea wasaliti kushinda uchaguzi lakini ukisema itakuchukua miaka 20 kuweka nchi sawa, inamaanisha unajiwekea kinga kama ukitenda mabaya usilaumiwe. That's not leadership.

..mimi wasiwasi wangu hii SGR inaweza kuwa na MAKOROKOCHO kibao tusiyoyahitaji kama yaliyokuwepo kwenye mkataba wa Kangi Lugola.

..mradi ni wa waTz wote lakini kuna USIRI mkubwa na sioni kama ujenzi wenyewe una ukaguzi wa kutosha toka kwa wabunge.
 
Hiyo miaka kumi na tano inaweza kuwa kweli, hao wakandarasi wanaogopa kumwambia kwasababu hataki kusikiliza ushauri wa mtu, alishakosea kwenye mengine kama la korosho hakujifunza, anakosea sasa kwenye hiyo reli bado hataki kujifunza, na atakosea mengine mbele ya safari, sijui Kikwete alimtoa wapi huyu mtu, bora angempa mwanamke tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unamaanisha hakuchaguliwa kwa kura Bali kapewa na Kikwete?Mfumo wetu wa Uchaguzi ni wa hovyo kiasi hicho?Je,si bora tungefanyia fedha tunazopoteza kuchagua kufanya mambo mengine?
Tudai Katiba Mpya ya Wananchi kuondoa hawa watawala tuweke viongozi wetu.
 
Zitto Kabwe:
Uharibifu wa Uchumi unaofanywa na Serikali yaMagufuli ni mkubwa sana. Itachukua miaka 10 kurudi Hali ya mwaka 2015 ( ambayo nayo haikuwa nzuri) iwapo ataondolewa madarakani mwaka huu. Akipata miaka 5 mingine itachukua miongo 2 ( miaka 20, two decades) na Marais 2 kurudi 2015

Zitto Kabwe:

Uchumi unaanguka kwa sababu ya viongozi kukosa MAARIFA. Tunapaswa kuikoa nchi yetu sasa sio kesho. Mwagapombe2020.

Zitto Kabwe:

SGR kipande cha Dar-Moro kilikuwa kiishe Novemba, sasa kipo 70%. Kuisha mwaka kesho. Sasa mkopo wa Biashara wa Fedha za kigeni umechukuliwa. Riba 9%. Serikali ipo kwenye panic. Gharama za Ujenzi zinaongezeka ( costs over run ). Mbia mmoja wa Ujenzi ( Mreno) kabwaga manyanga

Zitto Kabwe:

Akaanza kujenga. Hela zikatoka kwenye mzunguko. Hali ya maisha ya wananchi ikawa mbaya, ukuaji wa mzunguko wa Fedha ( M3- money supply ukawa NEGATIVE). Serikali ikaanza kushindwa kulipa invoices za Mkandarasi, wakandarasi wadogo wakakimbia. Ujenzi ukasimama! Moro-Dom ikakwama

Zitto Kabwe:

Mradi wa Reli ya Kati ya SGR USD Bilioni 7.5 - Fedha UWEKEZAJI WA UBIA ( PPP ) kutoka Benki ya Exim ya China ulikataliwa na Rais Magufuli akiamini kuwa ni dili la mtangulizi wake. Akasema tutajenga wenyewe kwa kutumia Kodi. Tukamwambia haiwezekani (Assets-Liabilities Match )

zitto Kabwe:

Niongeze kidogo kuwa, Standard Chartered Bank inaunganisha Deni la $1.4bn halafu anasaini CEO wa Dar? Largest single foreign currency denominated loan by Tanzania? Backed by export credit agencies of Sweden and Denmark? Isainiwe vile? Riba ndio 9%? Desperation au nini?

Kitila Mkumbo:
Hoja ya msingi ni hizo hela zinakwenda wapi. Tunajua kwa dhati kabisa fedha inayokopwa inakwenda kwenye miradi ya maendeleo na inaonekana. Ni wewe uliyeshauri kwa bidii kuwa tusijenge miradi hii kwa hela za ndani.

Zitto Kabwe:

Ni kweli nilishauri mwaka 2016 kuwa hamwezi kujenga Mradi mkubwa wa Reli SGR kwa Kodi za wauza nyanya. Imewachukua miaka 4 kuelewa hilo na baada ya Reli kuishia Morogoro, Wakandarasi kutolipwa na kuahirisha uzinduzi mara 7. Kuendesha Nchi ni MAARIFA sio maguvu na Ukatili

Kitila Mkumbo:
Hoja ya msingi ni hizo hela zinakwenda wapi. Tunajua kwa dhati kabisa fedha inayokopwa inakwenda kwenye miradi ya maendeleo na inaonekana. Ni wewe uliyeshauri kwa bidii kuwa tusijenge miradi hii kwa hela za ndani.

Zitto Kabwe:
Mimi sijasema lolote. Nimemwaga data tu kutoka Benki Kuu kuhusu Deni la Taifa. Kwamba wakati Uchumi unakua kwa 4-5% kwa mwaka, Deni la Nje ( Foreign currency denominated) linakua kwa zaidi ya 18% kwa mwaka. Katika miaka 4, Serikali ya Magufuli imekopa zaidi ya miaka 10 ya Kikwete

Kitila Mkumbo:
Replying to Zitto Kabwe
Hoja ya msingi ni hizo hela zinakwenda wapi. Tunajua kwa dhati kabisa fedha inayokopwa inakwenda kwenye miradi ya maendeleo na inaonekana. Ni wewe uliyeshauri kwa bidii kuwa tusijenge miradi hii kwa hela za ndani.
Mh. Zitto anajenga hoja nzito zilizojaa madini ya mambo ya kiuchumi, Prof. Mkumbo anajibu "very lightly" tena kwa jibu moja tu lenye kuonyesha jibu la jumla. Tatizo la wasomi wanao mzunguka Mh. Rais wanakwepa kumwambia ukweli na uhalisia wa mambo. Wanakwepa kusimama ktk nafasi zao kama wasomi, isipokuwa wamebaki kuvizia kumsifia tu hisia zake, kwa ajili ya matumbo yao na wala si vinginevyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitila Mkumbo ,

..angetueleza huu mkopo ni wa MUDA gani na RIBA yake ni kiasi gani.

..pia labda Prof angetuelimisha zaidi kuhusu UNAFUU wa mkopo huo akilinganisha mikopo mingine ambayo Tz imechukua, au nchi nyingine ambazo zimechukua mikopo mikubwa kwa ajili ya miundombinu.
Profesa yuko business anakula,akiongea sana atatema.Umesahau nidhamu yetu.Usionge wakati wa kula utakuwa mbea? Kitila Mkumbo
 
Kitila Mkumbo ,

..angetueleza huu mkopo ni wa MUDA gani na RIBA yake ni kiasi gani.

..pia labda Prof angetuelimisha zaidi kuhusu UNAFUU wa mkopo huo akilinganisha mikopo mingine ambayo Tz imechukua, au nchi nyingine ambazo zimechukua mikopo mikubwa kwa ajili ya miundombinu.
Kichwa kichafu hiki sasa hivi, kikwetu kuna msemo kuwa

"EMBUZI EMPUBI TOSIBIKAO YAWE"

Maana yake ni kwamba UKIONA MBUZI MKOROFI MLAFI NA ANAYEPENDA KULA MAZAO YA WATU EPUKA KUFUNGA MBUZO WAKO MWENYE TABIA NZURI NA MBUZI WA NAMNA HII.

Kitila aliyekuwa UDSM na huyu wa sasa wakikutana watapigana mpka kuuana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zito Kabwe siyo smart kichwani, ni mradi Dunia hii ambao haongezeki gharama ukilinganisha na gharama ya awali? Hiyo ni kawaida sana kwenye miradi yote hata nyumba yako binafsi tu.

Na kwa kuwa huyu jamaa siyo intelligent hakuna mahali ataenda kisiasa, 2020
wanamwaga Ubunge halafu kwisha habari yake.
Punguza jazba za kike alafu jibu hoja kwa hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..mimi wasiwasi wangu hii SGR inaweza kuwa na MAKOROKOCHO kibao tusiyoyahitaji kama yaliyokuwepo kwenye mkataba wa Kangi Lugola.

..mradi ni wa waTz wote lakini kuna USIRI mkubwa na sioni kama ujenzi wenyewe una ukaguzi wa kutosha toka kwa wabunge.
Huwa naona kina Stive Nyerere na wema sepetu ndiyo hupelekwa kwenda kukagua huu mradi na kupiga picha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zito Kabwe siyo smart kichwani, ni mradi Dunia hii ambao haongezeki gharama ukilinganisha na gharama ya awali? Hiyo ni kawaida sana kwenye miradi yote hata nyumba yako binafsi tu.

Na kwa kuwa huyu jamaa siyo intelligent hakuna mahali ataenda kisiasa, 2020
wanamwaga Ubunge halafu kwisha habari yake.
Asipokuwa mbunge ndo anashindwa kutoa hoja kama hizi? Au atanyimwa viza ya kwenda nje kama mkuu wa mkoa fulani?
 
Kitila Mkumbo ,

..angetueleza huu mkopo ni wa MUDA gani na RIBA yake ni kiasi gani.

..pia labda Prof angetuelimisha zaidi kuhusu UNAFUU wa mkopo huo akilinganisha mikopo mingine ambayo Tz imechukua, au nchi nyingine ambazo zimechukua mikopo mikubwa kwa ajili ya miundombinu.

Sio miaka 20?
 
Sio miaka 20?

..Asante.

..Lakini ni miaka 20 tangu lini?

..miaka 20 tangu mradi kuisha?

..huu mkopo sisi [ waTanzania ] ndiyo tumeuchukua. Sisi ndiyo tutaokuja kulipa. Hivyo basi tunapaswa kupewa taarifa za kutosha kuhusu mkopo huo.
 
..mimi wasiwasi wangu hii SGR inaweza kuwa na MAKOROKOCHO kibao tusiyoyahitaji kama yaliyokuwepo kwenye mkataba wa Kangi Lugola.

..mradi ni wa waTz wote lakini kuna USIRI mkubwa na sioni kama ujenzi wenyewe una ukaguzi wa kutosha toka kwa wabunge.
Lakini mbona kamati za bunge wanatembelea sana miradi wa SGR na wanajiridhisha? Hizo kamati zinawabunge wa upinzani pia. Hata hivyo ukilinganisha na Kenya, Tanzania imejengwa kwa bei poa kwa kila kilomita ya reli. Kwa hiyo kama mradi ungekuwa na madudu nadhani ungetugharimu zaidi ya majirani zetu.
 
Back
Top Bottom