Zitto Kabwe vs Prof. Kitila Mkumbo juu ya ujenzi wa SGR

Kwa hiyo profesa kajibu kwa kifupi hivyo ili werevu wang'amue wenyewe kwamba nae haungi mkono ujenzi huo wa SGR siyo?
 
Hililililopo tu linawashinda , hiyo ya umeme ndo wataweza ?? Tz kwakweli sijui tulimkosea Nini Mungu
 

..unaiamini kamati ya bunge?

..sidhani kama tunapaswa kujilinganisha na Kenya kila wakati.

..na sina uhakika kama gharama zetu zikiwa chini ya gharama za Kenya basi maana yake mradi wetu uko vizuri.
 
Sijui ni coincidence au ni utaratibu uliopngwa lakini siku za nyuma mimi nimebaini kuna wakosoaji wa serikali ambao wakichangia kwenye mitandao lazima wajibiwe na watu specific. Watu hao ni pamoja na Lissu. Siku za nyuma Zitto alikuwa akijibiwa na Kafulila na baadaye Mwigulu. Naona sasa Prof. Mkumbo naye amekuwa detailed kwa kazi hiyo!
 
Kitia makombo nawenzie huko waliko wanakula Makuku na mivinyo ya italia wanacheka hyahyahwaaahaaa hku wanashika baamedi vishundu... watajali kweli nchi kudaiwa? Muwage siriazi kidogo!!
 
Hawa ni marafiki kuna kamchezo wanacheza hapa!
 
..unaiamini kamati ya bunge?

..sidhani kama tunapaswa kujilinganisha na Kenya kila wakati.

..na sina uhakika kama gharama zetu zikiwa chini ya gharama za Kenya basi maana yake mradi wetu uko vizuri.
Kamati za bunge si zina wabunge wa pande zote (serikali na upinzani)? Kuamini au kutoamini ni swala lingine lakini kisheria wao ndio masikio na macho ya wananchi na hatuwezi kuwakwepa.

Ukija kwenye kulinganisha reli ya Kenya na ya Tanzania, Tanzania imeweza kujenga reli ya urefu unaokaribina na wake kwa nusu ya bei. KE $3.6 bilioni vs TZ $1.2 billion. Hapo utaona kama hata kama watu wanaficha chochote (kitu ambacho sio kweli) itakuwa hela ya kununulia mboga.
 
Hafu jamaa ni power monger kwa sasa anafikiria kulia matunda pori tu ikulu. Sijui alisoma wapi huo uchumi. Anatuletea siasa za chuki tu nchini . Sijui akienda nje anadhani miundombinu anayoiona imejengwa kwa bei ya migebuka ? Wajameni shame on our future oppositions
 
Hiyo SGR itabeba mzigo gani?
Kibandari hiki kidogo cha Dar kitaisupply mzigo wa kutosha?
Bora tungejenga na bandari ya bagamoyo
 
Mada hii ingekuwa kabambe kweli kweli, kama Kitila Mkumbo angeacha kuwa kama 'Robot'. Najua hana uwezo wa kuzijibu hoja za Zitto.

Naye ajitahidi kupata msaada wa data, au amlete Profesa wa Uchumi toka 'Jalalani' tumpambanishe na huyu mchumi mwanasiasa kijana Zitto.

Pangekuwa na utaratibu kama huu, sisi wengine tungekuwa wasomaji tu na kujifunza kama tumo darasani

JF ingekuwa na hadhi kubwa sana!

Hoja za Zitto zinahitaji kujibiwa. Profesa wa (nini vile? Psychology?) hana uwezo wa kuzijibu.
 
Zitto akagombee Burundi apate urais....tz kakwama.
Wanafiki ndio wanakwamisha nchi. Kitila anapotosha hoja ya uchumi wa nchi akijua fika kuwa anachokisema si kweli. Kabla mhe hajapewa ulaji serikalini hoja zake zilikuwa zinasimama. Sasa hivi anashangaza.
Lakini hii ndiyo hulka ya wasomi wa nchi hii. Wapo wale waliotuingiza chaka la makanikia (yamekosa wanunuzi), akini Bashiru, nk.
Mwalimu Nyerere alikuwa "intellectual" na aliziishi busara zake. Hakuwa kiongozi wa kudanganyika kirejareja. Mawaziri na watendaji wake walimjua. Aliwahi kusema:
". . . mtu akikushauri vibaya ukakubali ukijua ushauri wake si mzuri, basi atakuona ni mpumbavu na atakudharau . . ."

Bora hata ujenzi wa miradi mikubwa lakini si uwekezaji mkubwa kwenye ununuzi wa ndege za kwenda India, SA, na Chato. Hakuna return on investment (ROI) ya kurejesha mtaji na riba kwa muda unaokubalika. Hesabu za ATCL kama zilivyo za TISS na Ofisi ya Rais (pamoja na kwamba kwa sasa inafanya kazi za Wizara ya Fedha na mipango) hazikaguliwi!

Nyerere Hydro Power Project (NHPP) lilikuwa wazo la Mwl Nyerere kama la makao makuu ya nchi kuhamia Dodoma. Alisita kutekeleza mipango hiyo kwa sababu ya thathmini ya hali ya uchumi. Tuje kwenye SGR.

Zaidi ya 80% ya watanzania wako vijijini. Ajira yao ni Kilimo. The best strategy ni kuendekeza kilimo kwa kujenga miundombinu. Wakulima na wafugaji wasitegemee mvua tu. Uhaba wa chakula nchini ni matokeo ya wimbo wa "kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu". Nyimbo za " Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati", SGR, umeme wa Stieglers Gorge . . . mg 2015; "haijawahi kutokea tangu tupate uhuru . . ."

Wananchi wanateseka na hali ngumu ya maisha. Wanakamuliwa pesa. Zinapelekwa kwenye miradi. Hata hivyo hazitoshi. Tunakopa mikopo inayoratibiwa na Standard Chartered Bank, nk., benki za kibiashara. "Mabeberu" hayatatusamehe kulipa. Tukinyimwa na fedha na WB serikali inapiga kelele ajabu. Tutamaliza kulipa 3.3 trl/= lenye riba ya 18% (compound) leo?
Kwa vile wao na familia zao hawaguswi na hali hiyo, pofu linawatoka.
 
Kutila mkumbo hajawahi kuwa mpinzani.yule alikuwa mtu wa TISS alipandikizwa upinzani.
Unakumbuka kilichotokea alipokuwa president wa Daruso 1994 wakati wa kunji
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Riba kwa benki za kibiashara ni kubwa mno .Linganisha riba ya 9% stanbic na lending rate ya 3.5% miradi inayo fadhiliwa na ADB. Desperate times call for desperate measures.

In jiwe's case it is rather chaos calls for even more chaotic measures
 
Haueleweki .. nimeelewa ulipotoa povu la tusi tu basi.
Hata darasani mwalimu akifundisha siyo wote wanamuelewa mara moja. Na wengine hawaelewi kabisa kabisa na ndiyo hupata F kwenye mitihani.
 
Hata darasani mwalimu akifundisha siyo wote wanamuelewa mara moja. Na wengine hawaelewi kabisa kabisa na ndiyo hupata F kwenye mitihani.
Ukiona hivyo ujue mwalimu kaishiwa mbinu za kufundisha. Kama wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…