Zitto: Kesi nyingi za uhujumu uchumi ni za kubambika na kukomoa sasa wanatafuta hela. Nchi ya GANGSTERISM 100%

Zitto: Kesi nyingi za uhujumu uchumi ni za kubambika na kukomoa sasa wanatafuta hela. Nchi ya GANGSTERISM 100%

Ila tuendako tutakuja kulipa fidia kubwa sana na itakuwa hasara kwa nchi na sio .......
True ajae Nadhani atamauliza uraisi wake kwa kulipa fidia maana kesi za kuishtaki serikali zitakuwa hazina idadi kuanzia waliobomolewa nyumba zao,walioporwa hela zao bureau de change,watumishi nk.
 
Absolutely true

Na ndiyo yanayoikuta nchi hii hivi sasa, huyo Bwana anaagiza wapinzani wake wa kisiasa wakamatwe na wabambikiwe kesi za uhujumu uchumi, lakini wanajua kwenye mahakama zetu hawatashinda kesi hizo...........

Kutokana na ushahidi unaotakiwa huko mahakamani, kwa hiyo amekuja na " gia" ya kuwaonea huruma watuhumiwa hao, kwa hiyo amekuja na sheria za kutaka "kuwakamua" watuhumiwa hao kwa kuwalazimisha wakiri wenyewe ili watoke magerezani huko na walipe mabilioni ya pesa

Hii ni dhuluma mbaya Sana kutaka kupora Mali za watu haina tofauti na mwalimu kupora Mali za watu walizochuma kihalali tangu enzi ya mkoloni kupitia utaifishaji na uhujumu uchumi alifilisi watu wengi Sana na kuwaachia ufukara.Huku wakijifanya wanaenda makanisani.Hawa kanda ya ziwa huwa na chuki Sana na waliofanikiwa sijui kwann .Ni awamu ya kwanza na ya tano tu ndipo matajiri wamefanywa maadui awamu zingine zote zimeishi vizuri na matajiri.
 
Hizi kesi hazina ushahidi nyingi za kubambikiwa wanajua watashindwa thus miaka 4 sasa wamekosa ushahidi,kama ni kesi halali isingechukua hata mwezi kuupata ushahidi kuwatia hatiani.Kuepuka aibu ya kushindwa watawachomoa vipi ndo wamekuja na plan ya waandike barua kukiri walipe Pesa,kuomba msamaha tyr ni kukiri kosa bila kujali umebambikwa sababu uhuru wako na haki yako imeporwa.Haya mambo yanaaibisha .Na pia yatakuwa yakitumika kuumiza watu ili wachomolewe Pesa kama chanzo cha mapato .Unakamatwa unabambikwa unachomolewa unafilisiwa.
Mfano mtu katuhumiwa kwa kosa moja au mawili cha ajabu watengeneza kesi wanamjazia kesi za kujibu 400 au hata zaidi ukizisoma kesi zenyewe hazina tofauti zaidi ya kubadili sentesi tu, utitiri wa kesi unatumika vibaya kuwachanganya watuhumiwa, na je?wale wanaotumika kuwabambikia kesi wao watachukuliwa hatua gani? Kumtesa mtu miaka 4 mwingine ni masikini kama Michael Wambura atarudisha pesa ipi? akaotoe wapi?au wauze nyumba zao?
 
Watu sio maji kuwa hayana idadi/hayahesabiki.

Ni vizuri ataje majina ya watu anaodai wamebambikiwa kesi ya uhujumi uchumi ili tuwajue kuliko kuongea lugha za kisiasa.

Kinyume cha hivyo ni kutafuta tambo za kisiasa!
Zitto ni mnafki sana!
 
Ningekuwa mzee heri nifie jela sina cha kupoteza kuliko kupoteza Mali ya familia sitoi hata Mia.Heri niiachie familia ile Maisha yao yote kuliko kufilisiwa.
Utawala huu wanaweza hata kuwabambikia kesi familia yako yote pia wakavhukua mali ulizowaachia cha msingi ni kuomba mungu waache hii Dhambi ya kuwabambikia watu kesi kienyeji kwa njia haramu
 
Watu sio maji kuwa hayana idadi/hayahesabiki.

Ni vizuri ataje majina ya watu anaodai wamebambikiwa kesi ya uhujumi uchumi ili tuwajue kuliko kuongea lugha za kisiasa.

Kinyume cha hivyo ni kutafuta tambo za kisiasa!
Waliobambikiwa ni wengi hakuna haja ya kutaja list kuogea in general ndiyo vizuri zaidi wapate kujua watanzania wa sasa siyo wajinga wanajua sinema zote.
 
Huwa nayakumbuka maneno ya Baba wa taifa. "Katiba ya Tanzania imempa madaraka makubwa sana Rais wa Tanzania. Siku akiingia madarakani mwendawazimu, tutapata shida". Hayo ni maneno ya Nyerere. Nitawaletea video clip, ninayo.
Tafadhali ilete tuuone huo unabii wa Nyerere wetu!!!
 
HIZO NDIO SERA ZA ACT KTAFUTA NN KIMESMWA NISIMAMIE WAP ANGALAU NISIKIKE
 
Watu sio maji kuwa hayana idadi/hayahesabiki.

Ni vizuri ataje majina ya watu anaodai wamebambikiwa kesi ya uhujumi uchumi ili tuwajue kuliko kuongea lugha za kisiasa.

Kinyume cha hivyo ni kutafuta tambo za kisiasa!
Hilo linajulikana wazi kuwa watu wengi wanababikiwa kesi, ni wajinga tu waliovaa miwani ya mbao ndiyo hawajui,Wewe angalia wanaambiwa watubu harafu walipe pesa ndiyo watoke hii inamaanisha hawana kesi ya kujibu bali zinatafutwa pesa zao tu!!!!.
 
Back
Top Bottom