Zitto: Kesi nyingi za uhujumu uchumi ni za kubambika na kukomoa sasa wanatafuta hela. Nchi ya GANGSTERISM 100%

Zitto: Kesi nyingi za uhujumu uchumi ni za kubambika na kukomoa sasa wanatafuta hela. Nchi ya GANGSTERISM 100%

Mfano mtu katuhumiwa kwa kosa moja au mawili cha ajabu watengeneza kesi wanamjazia kesi za kujibu 400 au hata zaidi ukizisoma kesi zenyewe hazina tofauti zaidi ya kubadili sentesi tu, utitiri wa kesi unatumika vibaya kuwachanganya watuhumiwa, na je?wale wanaotumika kuwabambikia kesi wao watachukuliwa hatua gani? Kumtesa mtu miaka 4 mwingine ni masikini kama Michael Wambura atarudisha pesa ipi? akaotoe wapi?au wauze nyumba zao?
Naona Michael Wambura waliamua tu kumnyoosha maana yeye binafsi anapendaga kesi balaa,kidogo tu ameenda kuanzisha kesi mahakamani.

Nadhani akitoka huko hatatamani tena kuanzisha ma-kesi hovyo hovyo.
 
Absolutely true

Na ndiyo yanayoikuta nchi hii hivi sasa, huyo Bwana anaagiza wapinzani wake wa kisiasa wakamatwe na wabambikiwe kesi za uhujumu uchumi, lakini wanajua kwenye mahakama zetu hawatashinda kesi hizo...........

Kutokana na ushahidi unaotakiwa huko mahakamani, kwa hiyo amekuja na " gia" ya kuwaonea huruma watuhumiwa hao, kwa hiyo amekuja na sheria za kutaka "kuwakamua" watuhumiwa hao kwa kuwalazimisha wakiri wenyewe ili watoke magerezani huko na walipe mabilioni ya pesa
Nadhani unapobambikiwa kesi.. anayetakiwa kutoa ushahidi usio na shaka ni yule anaekubambika hiyo kesi ili kuishawishi mahakama. Hivyo aliye kwenye nafasi nzuri zaidi mahakamani ni yule mbambikiwa kwa kuonyesha hahusiki kwa namna yoyote ile. Lakini leo inaonekana kampuni X ilijipatia fedha isivyo halali, mmiliki wa kampuni hiyo ni wewe na nyaraka zote zinaonyesha ulichukua hiyo hela . Halafu useme huhusiki umeonewa.

Kutoa tamko la jumla hivi kwamba kila mhujumu uchumi kabimbikiwa kesi ni uhuni wa kisiasa. Wananchi wamelalamika sana huko nyuma kuhusu ufisadi. Wanasiasa wamepiga kelele sana including mwanasiasa uchwara, Zitto. Sasa hatua zimechukuliwa wanageuka kuwatetea walewale mafisadi.

Hebu tujiulize ni Mpinzani gani wa kisiasa wa magufuli aliebambikiwa kesi ya uhujumu uchumi. Halafu tujiulize tena hizo fedha ziliibwa au hazikuibwa? Na zikirudishwa zinamnufaisha nani ? Magu au taifa kwa ujumla. Acheni chuki, unafiki na ushabiki wa kipumbavu.
 
Mm ningekuwa Rais wa nchi watu wenye choko choko kama Zito mngehama nchi watanzania hatujazoea ujinga huu
 
Duh!..Ina maana hizo kesi ni vyanzo vipya vya mapato?
 
Wewe ndiyo shabiki pumbavu waliokula pesa za kivuko cha Dar Bagamoyo wameshitakiwa wapi? Kivuko kipo wapi sasa? Thamani yake tshs ngapi? Chuki unafiki unavyo wewe mshamba, wapo wapi walitafuna pesa za Richmond? Pesa za Rada, bomba la Gesi, kiwanda Hewa huko Lindi, wapo wapi waliouza nyumba za Serikali wakajiuzia nyumba kibao kienyeji na zingine kugawa kwa hawala ambao hawakuwa watumishi wa Serikali, wapo wapi walio kula Tilion 1.5 kienyeji wakata kumtoa kafara CAG kwa njia haramu? CCM mmetafuna pesa nyingi list ya tuhuma ni kubwa acha kujitoa fahamu kuja hapa kutaka kuwatukana wachangiaji wakati wewe mwenyewe huna kumbukumbu ya madhambi yenu kibao.
 
Mm ningekuwa Rais wa nchi watu wenye choko choko kama Zito mngehama nchi watanzania hatujazoea ujinga huu
Watanzania wa wapi? Labda wewe mwenyewe usiwasingizie watanzania ambao magufuli mwenyewe alisema watanzania siyo wajinga na wanajua vingi kuliko wewe na kamwe hawawezi kusikiliza ushauri wako milele.
 
Uchunguzi kwanza ukamilike ndipo kunakuwa na kesi cha ajabu wanaanza na tetesi unakamatwa kisha uchunguzi unaanza slow slow huku mtuhumiwa akisota baadae ukija kukosekana ushahidi unaambiwa ukiri kosa urejeshe pesa hi hali umekaa jela miaka 4 biashara zimeyumba mali imetawanyika huna kitu, only Tanzania unakutana na haya maajabu.
 
Wa kulaumiwa ni yeye kwa kutucopia katiba ya udikteka Wa swahiba wake Dikteta Mao na kuipaste kama katiba ya nchi.100% za lawama zote zitabakia kwa mwalimu.Angeibadili alipoona hatari hio maana yaliyomo yalikuwepo.Aina hii ya katiba umfaa mtu mwenye hekima na busara.

Tatizo siyo katiba, ni watu wanaokubaliana na hali hiyo huku wakilalamikia maandishi.
Kwani katiba iliyopo haijawahi kuvunjwa?
Uwepo wa katiba (maandishi) ni jambo moja na watekelezaji (watu) ni jingine.
Bila watu wanaojielewa na majasiri, makubaliano ya kimaandishi hayana uzito wowote.
 
Upelelezi unaendelea miaka3 hadi 4 hii sio sawa .Hata kesi zenye prima-facie evidence unasema bado upelelezi unaendelea? hapo kuna mashaka.
 
.... wamekuja na plan ya waandike barua kukiri walipe Pesa,kuomba msamaha tyr ni kukiri kosa bila kujali umebambikwa sababu uhuru wako na haki yako imeporwa.Haya mambo yanaaibisha .Na pia yatakuwa yakitumika kuumiza watu ili wachomolewe Pesa kama chanzo cha mapato .Unakamatwa unabambikwa unachomolewa unafilisiwa.
Mfumo wa Ki-mafia
 
Back
Top Bottom