MsemajiUkweli
Mmoja wa hao watu ni Yusuph Manji!!! Badala ya kumpa kesi ya uhujumu uchumi, kuhatarisha usalama wa taifa, na utumiaji wa dawa za kulevya... alikumbwa na hatia ipi miongoni mwa hizo?!
Mtakana sana, lakini serikali hii wakati mwingine huwa inafanya mambo kwa kukomoa raia wake!!! Ni kutokana na ukweli huo, ndo maana wengi wanaokuwa target ni lazima wapewe kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji pesa kwa sababu ni kesi zisizo na dhamana!!
Lengo ni kuwakomoa wahusika kwamba lazima wakae ndani!!
Na kweli, wengi wanakaa ndani lakini mwisho wa siku, majority wanakutwa kutokuwa na hatia na mashitaka mazito kama hayo... but who cares! Mission Accomplished! WASHAKOMOLEWA TAYARI!!
Aidha ni juzi tu hapa Evans Aveva na Godfrey Nyange (Kaburu) wamefutiwa mashitaka ya utakatishaji wa fedha huku wakiwa wamekaa mahabusu kwa miezi kadhaa!!
Turudi kwa akina Rugemarila!! Kama lengo sio kuwakomoa kwanini walioshirikiana nao kuchota pesa za Escrow bado wanadunda mtaani?!
Ruge na Singasinga hawakutumia mitutu na vifaru kwenda kuchukua pesa za Escrow bali walipata baraka zote za viongozi waandamizi pamoja na mahakama!! Kwanini basi wawekwe ndani peke yao lakini miezi kadhaa baadae waambie waombe radhi na kutoa pesa ili waachie!!!
Mtu kama Singasinga ambae amedhohofika kweli kweli, hata kama hana hatia, unadhani ataacha kuomba radhi?!
Anyway, endeleeni tu kutetea lakini ukweli utabaki pale pale.