Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,759
- 4,872
- Thread starter
- #61
Niseme moja tu hilo la kusema kilimo kimetelekezwa.Sasa wewe unajichanganya. Magufuli kawafanyia nini watu wa vijijini? Maana kwa taarifa yako kilimo kimeuwawa. Kilimo ndio ajira kuu vijijini, ambako watanzania walio wengi wapo. Serikali zote za CCM baada ya Nyerere, wamepuuza kilimo. Siku hizi wako watu wanaitwa AFISA UGANI. Kilimo kilikuwa enzi za MABWANA SHAMBA. Serikali iliwekeza kwenye research centers kama Mlingano, Ukiriguru, Naliendele, nk. Nenda kawaulize watafiti jinsi walivyotelekezwa.
Bajeti ya kilimo miaka hii ni bilioni kadhaa, wakati bajeti ya ujenzi ni zaidi ya Trilioni 4 kwa mwaka.
Mijini ndio kuna Flyover, madaraja ya baharini. Mabarabara yanayopewa umuhimu ni barabara kuu, sio zile feeder za vijijini. Wafugaji wanafilisiwa, wavuvi wamefilisiwa kwa kuchomewa nyavu na kuuwawa. Sana sana sehemu chache wanaweka umeme kwenye nyumba za nyasi. Hayo ndio maendeleo?
Watu wa ccm mnatambia kwamba pamoja na yote Magufuli ataibuka mshindi.
Kwa uchaguzi huu wa kuengua maelfu ya wagombea wa upinzani, ubabe, unyanyasaji, wala siwezi kukubishia. Endeleeni salama na ushindi wenu wa dhulma, kama mwaka jana uchaguzi wa serikali za mitaa. Ni wagonjwa wa akili tu watashangilia ushindi aina hiyo
Kilimo gani kilichokufa? Una maana waendelee kulima bila faida au una maana gani? Mi nakataa! Kabla ya Magufuli Kilo ya korosho iliwahi shuka hadi sh. 400. Ikapanda na kuishia sh. 800. Alipoingia ikapanda hadi zaidi ya sh. 2000! Kabla ya hapo wakulima walipigwa na hadithi ya Kilimo kwanza. Powertiller wakauziwa mil 9 badala ya 4 au 5!
Mwaka 2012 gunia la mahindi Sumbawanga liliwahi nunuliwa kwa sh. 12,000 hadi 14,000 kwa kukosa soko! Mwaka 2013/2014 wakulima wa mpunga walilizwa na ruhusa ya kuingiza mchele wa nje ya nchi. Mchele wetu ukakosa soko kabisa! Leo hii umesikia mara ngapi mchele umeagizwa nje? Kwani hakuna walaji? Tuseme hivi, tuache sentensi za jumla jumla kwa mambo yasiyo na ushahidi. Ndo mtindo wa Trump kuunda namba za kubuni kichwani tu! Tusichofahamu tuwaachie welevu!