Zitto, Lissu na Mbowe wanafanya makosa kama ya Morgan Tsvangirai

Niseme moja tu hilo la kusema kilimo kimetelekezwa.
Kilimo gani kilichokufa? Una maana waendelee kulima bila faida au una maana gani? Mi nakataa! Kabla ya Magufuli Kilo ya korosho iliwahi shuka hadi sh. 400. Ikapanda na kuishia sh. 800. Alipoingia ikapanda hadi zaidi ya sh. 2000! Kabla ya hapo wakulima walipigwa na hadithi ya Kilimo kwanza. Powertiller wakauziwa mil 9 badala ya 4 au 5!

Mwaka 2012 gunia la mahindi Sumbawanga liliwahi nunuliwa kwa sh. 12,000 hadi 14,000 kwa kukosa soko! Mwaka 2013/2014 wakulima wa mpunga walilizwa na ruhusa ya kuingiza mchele wa nje ya nchi. Mchele wetu ukakosa soko kabisa! Leo hii umesikia mara ngapi mchele umeagizwa nje? Kwani hakuna walaji? Tuseme hivi, tuache sentensi za jumla jumla kwa mambo yasiyo na ushahidi. Ndo mtindo wa Trump kuunda namba za kubuni kichwani tu! Tusichofahamu tuwaachie welevu!
 
Patriot,

..How old are you?

..Kwanza Mugabe alikuwa hapigani na Waingereza, alikuwa anapigana na utawala wa Walowezi wa Southern Rhodesia.

..Hivi unadhani Mugabe hakuwa na msaada toka nje wakati akipambana na Walowezi wa Southern Rhodesia?

..Au, umesahau kwamba Mugabe na Zanu walikuwa wanasaidiwa na WACHINA ktk vita vya ukombozi?

..Umesahau kwamba Mandela aliachiwa toka gerezani kwa msaada toka nje ikiwemo nchi za Magharibi?

..Unafikiri ANC na PAC wangeweza kuwatoa makaburu wa Afrika Kusini kijeshi?

..Mimi nadhani kilichosababisha Morgan Tsivangirai ashindwe ni king'ang'anizi cha Robert Mugabe na Zanu-PF.

..Walowezi hawakuwa tayari kuharibu UCHUMI ili kubaki madarakani. Lakini viongozi wengi wa Kiafrika wako tayari kupoteza kila kitu, kuua, na kuharibu uchumi, ili wabaki madarakani.

cc Mindi, Nguruvi3, tindo
 
Don't ask, how old am I? Ask; how knowledgeable am I?
Kwa maswali hayo, huijui Zimbabwe na hukusoma kilichoandikwa vizuri. Ukitaka kujua chochote juu ya Zimbabwe niulize kabla hujaandika.
Naomba nikuulize;
Makubaliano ya Uhuru wa Zimbabwe yalifanyika wapi?
Nani alikuwa msimamizi wa makubaliano hayo na ni kwa nini?
 
Huijui Zimbabwe, huijui SA, FINITO!
Mataifa ya mstari wa mbele yalikuwa yanasumbuana na US na UK kwa sababu gani? Unadhani bila nchi hizo Smith na makaburu wangedumu kwa miaka hiyo yote? Tukiacha mambo ya Yanga, simba tukaanza kujisomea, siku ukipewa uwaziri hutakosa cha kusema na kukosea kama Phillip Mulugo.
 

..achana na mambo ya Lancaster House.

..wengine tumefuatilia harakati za ukombozi wa Zimbabwe toka wakati wako Mgagao.
 
..achana na mambo ya Lancaster House.

..wengine tumefuatilia harakati za ukombozi wa Zimbabwe toka wakati wako Mgagao.
Naijua historia ya Zimbabwe tangu enzi za Chief Tangwena. Najua humfahamu, piga google hapo! huo ndo mwanzo wa Ian Smith.
 
Naijua historia ya Zimbabwe tangu enzi za Chief Tangwena. Najua humfahamu, piga google hapo!

..kama unaifahamu historia kwanini unajaribu kuipotosha?

..Zanu na Mugabe walisaidiwa na outsiders dhidi ya Walowezi, kama ambavyo Tsvangirai alisaidiwa na outsiders.
 
Ni hivi:
1) Maendeleo ya kilimo lazima yajikite kwanza katika utafiti. Bwana Shamba au Afisa Ugani ndio daraja kati ya research center na mkulima. Anawasilisha matatizo na changamoto kule research , na pia kuleta matokeo ya tafiti kwa mkulima. Utatu huu ulifanya kazi vizuri enzi za Nyerere. Sasa research imekufa, daraja pia halipo. Ndio maana sishangai zao la ndizi linatoweka Bukoba sababu ya magonjwa. Pia uzalishaji wa mbegu bora kulingana na eneo hapa nchini umeyumba. Uzalishaji kwa hekta umeshuka kwa sababu hizi na zingine.

2) Kilimo popote duniani kinahitaji ruzuku. Ipo hivyo nchi zilizoendelea pia. Kilimo hivi sasa ni biashara kubwa inayohitaji mtaji mkubwa, huku uncertainties na risks ni nyingi mno. Ndio maana mabenki kwa kawaida hayatoi mikopo kwa wakulima, bila support ya serikali. Enzi za Nyerere ruzuku ilikuwepo, na taifa likajipatia chakula na fedha za kigeni. Wakati wa Mwinyi ruzuku iliondolewa katika awamu tatu, kwa presha ya Benki ya Dunia na IMF.
Bila ruzuku hakuna maendeleo ya kweli ya kilimo, wala kilimo kinachoondoa umaskini wa mtanzania.

3) Masoko. Magufuli 2015 aliahidi kutozuia wakulima kuuza nje. Kwa kuwa hakununua chakula cha akiba, pesa akatumia kujenga barabara, akazuia kuuza nje kwa hofu ya njaa.

Ni kweli sera ya kilimo kwanza ilihujumiwa na utawala wa Kikwete , japokuwa original draft ya SUA ilikuwa excellent . Lakini mimi nilitarajia Magufuli asimamie mapinduzi ya kilimo Tanzania. Hilo halipo, Magufuli hakipendi kilimo kama watangulizi wake. Kujenga flyovers kunaonekana zaidi kuliko kuwekeza kwenye kilimo.
Mimi sio mjinga katika kilimo, najua ninachoongea. Naongelea mambo ya msingi
 
Ivi tukiomba msaada kidogo na ujerumani kutaaribika kitu?
 

.. 🤣 🤣

..wakati mwingine Jiwe hutishia wateule wake kwa kuwaambia atawatumbue waende wakalime.

..sasa hapo ndipo utakapojua mtizamo wa bwana mkubwa kuhusu kilimo, na wakulima.
 
Ivi tukiomba msaada kidogo na ujerumani kutaaribika kitu?
Kidogo ya nini? Wenzako wanataka sana ili wanakoshitaki waweze kutumia nguvu kuwapa madaraka. Kuna siku walijikusanya pale Ubalozi wa EU, wakapewa na kahawa. Sijui walipata nini. Kuna kosa hawa mbumbumbu wetu wasilolijua. Balozi za nchi za ulaya na US. wanamfahamu kila kiongozi wa juu wa nchi walipo. Wanamfahamu Mbowe, Rungwe, Zitto, Cheyo, n.k. Nikisema wanamfahamu ni pamoja na mapungufu yake. Wanajua wamfurahishe kwa lipi. Kama ni mcheza disco kama yule aliyepita, akifika tu anapigiwa ndombolo ili ajione yuko nyumbani. Ina maana wanapofanya maamuzi wanakuwa na taarifa zote!

Unapojipeleka US na EU wanakuwa wanafahamu kama wewe ni political material au rubbish. Wanakupa wanachoona kinakufaa. Ndo maana hawa jamaa wanaambulia comfort tu!
 
Sadakta! Shida za hawa wenzetu hawazami kwenye hoja, wanatanguliza ushabiki
 
Kesho tupo na mzalendo wetu ambaye tangu aingie ikulu hajakanyaga Ulaya.




MAGUFULI4LIFE
 

..hivi viongozi wa juu wa ccm bila dola unadhani ni political material au rubbish?

..wana ccm wanang'ara kwasababu wana dola nyuma yao lakini nje ya hapo si lolote si chochote.
 
Sasa unachobisha nini? Hizo nchi za mstari wa mbele ni nguvu ya ndani? Of course ni nguvu toka nje ya Zimbabwe. Au nje ni lazima awe beberu? Hujaona wazungu wanaounga mkono ukombozi, na weusi wanaunga mkono ubaguzi na ukaburu?
 
Unavyoandika yaonesha wazi wewe ni mtu unayetaka upewe pesa za research, basi! Hizo taasisi za utafiti unazofahamu zilipewa pesa na Kikwete?, Mkapa je?, Mwinyi? Ukijibu hayo ndo uanze kumlaumu Magufuli. Kwa maoni yako, matatizo ya kilimo chetu kwa sasa yanahitaji utafiti ili kutatuliwa? Yaani kulima na kupanda kwa mstari tunahitaji utafiti? Utafiti lengo lake ni jingine, boss! Kilimo chetu hakihitaji utafiti, kinahitaji kusimamia taarifa zilizopo tayari hapa nchini.
 
..hivi viongozi wa juu wa ccm bila dola unadhani ni political material au rubbish?

..wana ccm wanang'ara kwasababu wana dola nyuma yao lakini nje ya hapo si lolote si chochote.
Sawa kabisa, lakini kuna wansiasa huko tunakoita upinzani, hata uwape dola, wataishia kuifilauni tu!
 
Oohhh, sasa nimekuelewa vizuri sana. Kwanza huelewi niandikacho. Nimesema tawala zooote za ccm ukiacha Nyerere, wamedharau kilimo, pamoja na Magufuli .
Kwaiyo research sio muhimu siyo? Sawa mkuu wala sihitaji kuendeleza mjadala na wewe.
 
duh, bado upo????
 
Oohhh, sasa nimekuelewa vizuri sana. Kwanza huelewi niandikacho. Nimesema tawala zooote za ccm ukiacha Nyerere, wamedharau kilimo, pamoja na Magufuli .
Kwaiyo research sio muhimu siyo? Sawa mkuu wala sihitaji kuendeleza mjadala na wewe.
Research ya nini? Niambie nini unachotaka ku-research! KUna watu wanaamini research ni muhimu saaana kwa kuwa tu wameajiliwa kufanya kazi hiyo. Tunataka maendeleo na leo hii ni 4th industrial revolution, unajua inasema nini? Eti research!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…