The Farmer
JF-Expert Member
- Jan 7, 2009
- 1,658
- 559
Hawa ndio wa hatari kuliko hata hao wanaoonyesha sura zao kamili. Hawa ndio wanafiki na ndumilakuwili wanaofoka na kutoa povu leo, lakini mwisho wa siku wanaungana na wenzao kupitisha miswada na bajeti za wizi na ya kitapeli. Toka lini maji na mafuta yakachanganyikana kilaini hivyo ?
Selelii, Kilango, na Ole Sendeka,
Mporogomyi, Kimaro na Mwakyembe
Mwambalaswa, Mpendazoe na Shibuda
Shelukindo, Chegeni na Zambi
hivi tuwaeleweje ?
Acheni kelele zenu za kinafiki
wote mwaogelea kwenye uchafu.
Hivyo wote ni wachafu
Mag3, Nakuunga mkono. Wabunge wa CCM ni wanafki sana kelele nyingi bungeni lakini linapokuja swala la kupitisha Budget ndio hao hao wanakuwa wa kwanza.