Lyimo
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,826
- 2,023
FF alishawahi kutupa statistics kuwa JK ndiyo kiongozi pekee aliyeweza kuzalisha umeme mwingi kuliko mkoloni na awamu nyingine zote. Ni kweli ilibidi iwe hivyo kutokana na ongezeko la watu (population) , kiuchimi pamoja na maendeleo ya kisasa ambapo nguvu ya umeme ni jambo nyeti. Sasa nasikitika kuona jambo hili linakuwa kwenye makaratasi tu na midomoni kwa viongizi wenye dhamana ama kubebwa kisiasa zaidi. Kukosekana kwa umeme katika karne hii,ni wazi kuwa kunakwamishwa kwa shughuli nyingi za maendeleo. Tunahitaji uwajibikaji makini kwenye mambo nyeti kama haya, hizi blaablaa zinazoendelea zinazidi kututokomeza kusiko.