Zitto, Makamba na mwakilishi wa TANESCO ndani ya mdahalo wa Star Tv

Zitto, Makamba na mwakilishi wa TANESCO ndani ya mdahalo wa Star Tv

Jamani mnyika ni form six leaver kama Dj mbowe sasa ataongea nini zaidi ya kwamba solution ni kuandamana.tatizo la wanaJF chanzo chao cha habari ni mwanahalisi pekee.
Na chanzo cha habari za magazeti mara nyingi ni JF,hapo sasa!
 
Mara baada ya ufisadi huu mkubwa wa DOWANS unaomkera kila Mtanzania leo, kuna uwezekano mkubwa sana ufisadi mwingine mkubwa zaidi tena utakaogharimu taifa mpaka vitukuu endapo HAWA WABUNGE VIJANA WANAOUTUMIA UDHAIFU WA CCM hivi sasa watakapoachiwa maswala hasa ya mradi wa gesi na madini kuchezea wapendavyo kwenye kujipeleka nazo kama mali binafsi kwa makampuni ya kimataifa.

Tusipoziba ufa leo juu ya mikataba zaidi na hasa itakayosaidiwa kuingiwa na January Makamba na pengine kuchangi KUMPOFUSHA KABISA huyu Zitto Kabwe na huku kucharaza ndimimbili kwake,
UFISADI UTAKAOFWATIA hasa juu ya MAJADILIANO JUU YASIODHIBITIWA NA WADAU WENGI JUU YA MIRADI ITAKAYOTOKANA NA GESI NCHINI, watu tujiandae kulia na kusaga meno zaidi.

Onyo langu ndio hilo hapo, hutaki basi!!
 
Zitto aje hapa jamvini aseme ni kwann aende yeye wakati waziri kivuli yupo? Hiki kitakuwa kimbele mbele na uroho wa madaraka. km kwenye midahalo tu anakuwa mroho hv je akipata huo urais si atakuwa anaenda hadi kwenye midahalo ya kata

Siku zote nyie ndio mnasababisha chama kionekane ni cha upande watu wa upande fulani, Hivi mnachohoji kuhusu Zitto ni nini?
Hivi mnyika ni nani?
Hivi nani asiyejua kuwa zitto n M/kiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma ambayo TANESCO ni mojawapo?
Hivi ni kukosa uelewa au ni makusudu tu ya kutotambua kuwa mdahalo ule ulihusu wenyeviti wa Kamati za Bunge na sio Waziri wala Waziri kivuli?
Mnaonekana kuwa na chuki binafsi na zitto tu na hamna sababub nyingine yeyote.
Ikumbukwe kuwa zittoanasimama kwa uwezo wake na sio kubebwa km hao watu wenu.
Napata wasiwasi na Mrengo wa Chama sasa.
 
zitto kabwe alikuwa nani aliposimamia hoja ya dowans? Alikuwa nani aliposimamia hoja ya buzwagi? Unaweza ukawa waziri kivuli usiwe na ajenda na unaweza kuwa mbunge wa kawaida na ukawa na ajenda na hoja, huyo ndio zitto.
ZZK ni msomi wa uchumi na sheria, mbunge wa muda mrefu mwanaharakati. Anaupeo na uelewa wa kuelezea TANESCO imefikaje ICU

Well said!
 
Makamba: Hatuwezi kulazimisha mtu kujiuzulu, tutasema tunachoamini ni sahihi ili mtu ajihukumu mwenyewe.
Unaweza ukawa smart,lakini kama unatetea ufisadi,unaonekana kama something is wrong in your thinking capacity!

Yani uko affected kiasi cha kwamba unakuwa kama mtu aliyevaa suti nadhifu lakini kwenye makalio pako wazi kabisa!
What the ef is this for real?

Kiongozi halazimishwi kujiuzulu,eti ajihukumu mwenyewe,huo uongozi wamejipa wenyewe?Yani mkishakuwa viongozi mnakuwa accountable to your own self?

No wonder wanauza nchi hawa.Kumbe wanaamini ni yao binafsi.

Hii kauli imeniudhi sana.Huyu mtu ni very out of touch!
 
Zitto: Iwe marufuku wanasiasa kuingilia utendaji wa TANESCO

Zitto: Reform ya TANESCO ni jambo ambalo halina mjadala.
Na huyu ni mwanasiasa anayesema TANESCO isi ingiliwe na wanasiasa kwenye kikao cha wanasiasa ambapo anataka wanasiasa waifanyie TANESCO reform bila mjadala kwenye mjadala huu wa kisiasa!
 
Kwa bahati mbaya sana katiba yetu haijatoa nafasi kwa mgombea wa kujitegemea, yaani mgombea ambaye halazimiki kubeba bedera ya chama cha siasa wakati wa kutafuta vyeo vya kisiasa. Na hii haina maana kuwa haki ya kuwa mgombea wa kujitegemea ni kwa raia asiye kuwa mwanachama wa chama cha siasa, ila hata kwa mwanachama wa chama cha siasa lakini chama chake kimekataa kumdhamini. Kutokuwapo kwa haki hii ni hujuma kwa haki ya msingi ya raia, inabidi katiba ijayo isahihishe hujuma hii.

Kwa sasa kila mgombea ni lazima ateuliwe na chama chake cha siasa na anapokuwa ameshinda kilicho shinda ni chama chake na akishindwa, chama chake kinakuwa kimeshindwa. Ndio maana mwanachama anapokuwa ameteliwa hutakiwa kuzijua na kizitetea sera za chama chake. Mwanachama asiyejua sera hasitahili kuteuliwa na hata yule anayezijua kama hana uwezo wa kuzitetea sera hizo hasitahili kuteuliwa. Wakati wa kufanya uteuzi chama cha siasa kinatakiwa kwenda mbali zaidi ya kuzijua na kuzitetea sera hizo ikiwa ni pamoja na kuziishi. Ni lazima kuzitekeleza kwa vitendo pasipo kutia shaka yeyote. Sina uhakika kama kila chama kinachofanya uteuzi wa wagombea wake kinazingatia suala hili?

Ninakuwa na mashaka kwa sababu, mwenendo wa rais, wabunge na hata madiwani unatia shaka kwa maana wanaonekana wanajitegemea zaidi kuliko kutegemea sera za vyama vyao. Kinachotia shaka zaidi ni kwamba vyama havionyeshi kukerwa na tabia hii ya wateule wao.

Jana niliangalia madahalo wa “
Nishati na Tanzania tuitakayo” kati ya Mheshimiwa Zitto na Mheshimiwa January Makamba. Sio Makamba wala Zitto waliojitanabahisha na vyama vyao, utadhani sio wana siasa wanaowakilisha vyama. Inaeleweka kwa Mheshimiwa Makamba kutotanguliza chama chake, kwani ujasiri ageupata wapi? Kwa lipi la kujivunia! Haieleweki kwa nini Mheshimiwa Zitto alishindwa kutetea sera dhahiri za CHADEMA. Mheshimiwa Zitto alitamka chama chake mara moja, labda kama sikusikia vizuri. Hata hivyo alionekana kama mtu kando tu na sio naibu katibu mkuu na makamu mwenyekiti wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Mheshimiwa Zitto, hivi unayo maelezo ya kwa nini imekuwa hivyo? Au ni katika ile dhana ya kuwa ” tunapokuwa tunaongeea masuala mazito ya kitaifa, vyama vyetu tuviweke kando?” Kama jibu ni hilo au linakaribiana na hilo, nisaidie kwa kuniambia ni wakati gani siasa za vyama zinafaa?
 
Kwa bahati mbaya sana katiba yetu haijatoa nafasi kwa mgombea wa kujitegemea, yaani mgombea ambaye halazimiki kubeba bedera ya chama cha siasa wakati wa kutafuta vyeo vya kisiasa. Na hii haina maana kuwa haki ya kuwa mgombea wa kujitegemea ni kwa raia asiye kuwa mwanachama wa chama cha siasa, ila hata kwa mwanachama wa chama cha siasa lakini chama chake kimekataa kumdhamini. Kutokuwapo kwa haki hii ni hujuma kwa haki ya msingi ya raia, inabidi katiba ijayo isahihishe hujuma hii.

Kwa sasa kila mgombea ni lazima ateuliwe na chama chake cha siasa na anapokuwa ameshinda kilicho shinda ni chama chake na akishindwa, chama chake kinakuwa kimeshindwa. Ndio maana mwanachama anapokuwa ameteliwa hutakiwa kuzijua na kizitetea sera za chama chake. Mwanachama asiyejua sera hasitahili kuteuliwa na hata yule anayezijua kama hana uwezo wa kuzitetea sera hizo hasitahili kuteuliwa. Wakati wa kufanya uteuzi chama cha siasa kinatakiwa kwenda mbali zaidi ya kuzijua na kuzitetea sera hizo ikiwa ni pamoja na kuziishi. Ni lazima kuzitekeleza kwa vitendo pasipo kutia shaka yeyote. Sina uhakika kama kila chama kinachofanya uteuzi wa wagombea wake kinazingatia suala hili?

Ninakuwa na mashaka kwa sababu, mwenendo wa rais, wabunge na hata madiwani unatia shaka kwa maana wanaonekana wanajitegemea zaidi kuliko kutegemea sera za vyama vyao. Kinachotia shaka zaidi ni kwamba vyama havionyeshi kukerwa na tabia hii ya wateule wao.

Jana niliangalia madahalo wa "
Nishati na Tanzania tuitakayo" kati ya Mheshimiwa Zitto na Mheshimiwa January Makamba. Sio Makamba wala Zitto waliojitanabahisha na vyama vyao, utadhani sio wana siasa wanaowakilisha vyama. Inaeleweka kwa Mheshimiwa Makamba kutotanguliza chama chake, kwani ujasiri ageupata wapi? Kwa lipi la kujivunia! Haieleweki kwa nini Mheshimiwa Zitto alishindwa kutetea sera dhahiri za CHADEMA. Mheshimiwa Zitto alitamka chama chake mara moja, labda kama sikusikia vizuri. Hata hivyo alionekana kama mtu kando tu na sio naibu katibu mkuu na makamu mwenyekiti wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Mheshimiwa Zitto, hivi unayo maelezo ya kwa nini imekuwa hivyo? Au ni katika ile dhana ya kuwa " tunapokuwa tunaongeea masuala mazito ya kitaifa, vyama vyetu tuviweke kando?" Kama jibu ni hilo au linakaribiana na hilo, nisaidie kwa kuniambia ni wakati gani siasa za vyama zinafaa?
Umezungumza vizuri sana mkuu wangu na tatizo hili lipo kwa viongozi wengi sana Tanzania. Nimeliona sana na mara zote nimeshindwa kabisa kuelewa mbunge anapoongea huongea kama mwakilishi wa sera za chama au mtaalam mtendaji wa maswala hayo!.

Hawa vijana wetu wote wana tatizo moja kubwa sana, nalo ni kutokuwa Wanasiasa na wameingia siasa kwa sababu ndiko wanakoweza kuonyesha utaalam wao ktk maamuzi ya kiuongozi..Hawana imani na itikadi wala sera isipokuwa elimu za darasani ktk kutafuta ufumbuzi wa maendeleo yetu. Na ndio maana utawaona wakimshangaa Obama ktk maamuzi yake ya kisiasa ambayo ni tofauti kabisa na elimu yake. Bila kufahamu kwamba Obama ni Mwanasiasa kwanza na elimu ya darasa inamsaidia kutafsiri sera za chama na makusudio yake ktk ujenzi wa Marekani ya kesho. Huwashangaa viongozi wa nchi za Marekani na Ulaya kwa sababu huzungumzia kiutaalam sera za chama zaidi ya ukweli uliopo hata kama hakuna ukweli wala uhakika.

Kwa hiyo, vumilia hizi ndio siasa za Bongo na ndio maana wanashindwa kuelewana ndani ya chama kwa sababu kila mmoja wao ana fikra zake ktk utatuzi wa mahitaji yetu. Na ndio maana unaweza kumkuta mwanaChadema akipongeza hatua ya mikataba ya uzalishaji umeme ambayo ni pinzani na sera za chama chake au kupinga hata sera za chama chake kama vile Elimu bure kwa wote. Nina hakika ndani ya Chadema wapo watu wanaamini haiwezekani na vile vile wapo watu ndani ya CCM wanaamini Elimu bure kwa wote ndio njia pekee ya kupambana na adui Ujinga..Wapo wanachadema wanaoamini Ufisadi sio tatizo kubwa isipokuwa Uzalishaji ndio muhimu zaidi na kadhalika...

Kizazi kijacho ni vichekesho vitupu, hakuna wanasiasa bali ni kundi la wasomi ambao wanafikiria wanajua kila kitu ktk kukidhi matatizo yetu na pengine wanaweza kuwa sawa kwa sababu nchi yetu haihitaji Itikadi ya vyama. WATU na MAZINGIRA yetu ni ya kujikimu na matatizo tulonayo hatuhitaji mfumo wa kiitikadi na sera bali kuziba vilaka ktk matatizo tulonayo hivyo wanahitajika zaidi fundi vilaka kuliko siasa za kupanga dira ya huko tuendako!..Tutaweza vipi kufikiria kesho, ikiwa maisha ya leo yanatushinda?...
 
hapa rombo view wameweka star tv
namtazama kwa makini sana,kuna kipindi alitazama kidogo lakini akageuka tena kuendelea na mazungumzo na jamaa zake

Hiyo kali, pamoja na kutotaka kuja, hana hata interest ya kujua kinachozungumzwa? Kama unayosema ni kweli basi nia yake ilikuwa ni kuwapoteza hao washkaji zake wasinyake issue, maana asingeweza kuondoka au ku instruct channel ibadilishwe.
 
Ni sifa zipi zimetumika kwa Zitto kuwa ktk huo mdahalo wakati yeye sio waziri kivuli wa nishati na madini?

Ukiangalia wajumbe wengine wote wana mahusiano ya moja kwa moja na mambo ya umeme. Hapo ni bora wafanye mabadiliko aende Mnyika ambaye hiyo ni wizara yake na Zitto asubirie siku ya wizara yake apambane na Mkullo

Zitto alihudhuria kama Mwenyekiti wa kamati - Mashirika ya Umma kwa sababu suala la Tanesco lipo ndani ya kamati ya Mh. Zitto.... Tuache majungu, hata kama angekua sio M/kiti wa hiyo kamati lakini kama mtanzania ana nafasi ya kushirikia pale kwa sababu hakukuwa na vigezo vya wazungumzaji wakuu!?
 
Kufanya midahalo ni sehemu ya kazi yao, kwa kupitia midahalo tunapata taarifa nyingi. Kumbuka Kipindi kiko usiku ni baada ya kazi ya mchana kutwa na hapa wanapata nafasi ya kutuharifu, vilevile wataulizwa maswali na muandaaji wa huu mdahalo... Ni kwanjia ya midahalo hii ndo tumeweza kujua mambo mengi.

Mdahalo maana yake nini? Toka lini mdahalo ukafanywa juu ya tatizo linahitaji suluhisho na tiba sahihi? au una maana hawajui la kufanya juu ya hayo matatizo au kama wanayajuwa kwanini wasifanye!

Kukiwa na matatizo basi tufanye mdahalo ndio njia sahihi ya kutatua matatizo yaliopo? Duh we kweli mtaalam.
 
Zitto wa 2007 alikuwa bora kuliko Zitto wa 2010/11. Kuna kila dalili ya 'uswaiba' kati ya Zitto na January Makamba. Na kwa kiasi kikubwa huu uswaiba hauna manufaa kwa watanzania wa kawaida waliopigika kimaisha, ni wa 'ki-mtandao zaidi. Kwenye sherehe za Sudan ya Kusini Zitto alikuwa kwenye msafara na niliuliza kwa nini yeye na sio 'waziri kivuli'? Sasa kwenye mjadala wa nishati kwa nini yeye na sio waziri kivuli? Kamaliza kuchunguza UDA? Huu mng'aro wa Zitto CCM haujakaa vizuri hata kidogo!

Pili, Zitto ni waziri kivuli wa fedha, shilingi ya Tanzania inashuka thamani kila kukicha, uchumi unashuka bei za bidhaa zinapanda. Kwa nini Zitto asijishughulishe na mambo yanayomsuhu yeye moja kwa moja badala ya kuingiza pua kwenye ofisi za wengine? Zitto ana ujuzi gani wa ziada kwenye mambo ya umeme? kasomea umeme? Mnyika alialikwa kwenye huu mjadala akakataa?


Yeye alikaribishwa na Mwakitwange, afanyeje sasa? mbona mwapenda kuhukumu tu kila wakati?
 
Mara baada ya ufisadi huu mkubwa wa DOWANS unaomkera kila Mtanzania leo, kuna uwezekano mkubwa sana ufisadi mwingine mkubwa zaidi tena utakaogharimu taifa mpaka vitukuu endapo HAWA WABUNGE VIJANA WANAOUTUMIA UDHAIFU WA CCM hivi sasa watakapoachiwa maswala hasa ya mradi wa gesi na madini kuchezea wapendavyo kwenye kujipeleka nazo kama mali binafsi kwa makampuni ya kimataifa.

Tusipoziba ufa leo juu ya mikataba zaidi na hasa itakayosaidiwa kuingiwa na January Makamba na pengine kuchangi KUMPOFUSHA KABISA huyu Zitto Kabwe na huku kucharaza ndimimbili kwake,
UFISADI UTAKAOFWATIA hasa juu ya MAJADILIANO JUU YASIODHIBITIWA NA WADAU WENGI JUU YA MIRADI ITAKAYOTOKANA NA GESI NCHINI, watu tujiandae kulia na kusaga meno zaidi.

Onyo langu ndio hilo hapo, hutaki basi!!
Kweli mkuu umenena kuna kitu nyuma yake, nani amefadhiri huo mndahalo, nani beneficially wa outcome yake???????? Sio mbinu chafu ya kufanya ufisadi mwingine wa DOWANS NO 10?????????Hapa watu wafanye utafiti wasifuate mkumbo, kuburuzwa kama RICHMOND tukaja kulia na kusaga meno!!!!!!!!!!
 
Kweli sisi watanzania ni mabingwa wa kuongea na kulalamika, kwa staili hii sisi tutakuwa na maendeleo ya kulalamika na kuongea tu, ukija kwenye vitendo mmmmmmmh!
 
wakubwa ule mwaliko tu, mlitaka akatae mbona ngeleja na malima mjamlilia awepo
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Zitto, January wamkalia kooni Ngeleja [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 17 October 2011 21:41 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

WASEMA KAMA AMESHINDWA KAZI YA UWAZIRI AACHIE NGAZI, SERIKALI YAINGIA MITINI
Mwandishi Wetu
Mwananchi

WENYEVITI wa Kamati za Bunge za Nishati na Madini, January Makamba na Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe wamesema ikiwa hali ya umeme itaendelea kuwa mbaya nchini, itamlazimu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kujiuzulu.Kadhalika, wenyeviti hao wamesema hakutakuwa na uhalali wa Serikali kuzilipa kampuni zilizopewa jukumu la kuzalisha umeme wa dharura ikiwa umeme huo hautapatikana katika muda uliotarajiwa.

Wakizungumza Dar es Salaam juzi usiku kwenye mdahalo kuhusu ‘Hali ya Umeme nchini na Tanzania tunayoitaka’ ulioandaliwa na Kampuni ya Vox Media, wabunge hao waliuponda mpango wa dharura wa Serikali wa kukabiliana na mgawo wa umeme wakisema hautekelezeki.Katika mdahalo huo uliorushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha Star, January alisema: “Bora kutokuwa Waziri kuliko kuwa waziri ambaye kauli zake haziaminiki kwa umma.”

Alisema kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake za kuondoa mgawo wa umeme, lazima waziri husika awajibike kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika nchi za magharibi.

Hata hivyo, January ambaye ni pia Mbunge wa Bumbuli (CCM) na Katibu wa Mambo ya Nje na Siasa wa CCM, alisema suala la kujiuzulu kwa waziri linategemea zaidi uadilifu wake na mamlaka iliyomteua kushika wadhifa huo.

Kwa upande wake, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) alisema: “Niliwahi kusema bungeni kwamba kila waziri aandike barua ya kujiuzulu ‘in advance’ (mapema) ili pale anaposhindwa kutekeleza wajibu wake, kazi ya Spika inakuwa ni kuchukua ile barua na kumkabidhi Rais.”

Alisema katika hali ya sasa, Serikali imeshindwa kutimiza ahadi iliyoitoa bungeni kuhusu utekelezaji wa mpango wa dharura wa kuzalisha umeme ili kuwezesha nchi kuondokana na mgawo na kwamba hilo tu linatosha kumfanya waziri ajiuzulu wadhifa wake.

Mpango wa dharura Wabunge hao walisema kuna kila dalili kwamba huenda mpango wa dharura wa kukabiliana na giza nchini ambao uliwasilishwa na Serikali bungeni usitekelezeke.

Mpango huo ni ule uliowasilishwa bungeni na Waziri Ngeleja Agosti 13, mwaka huu akiliomba Bunge liidhinishe kiasi cha Sh523 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wake. Mpango huo unaonyesha kuwa kutokana na dharura hiyo, Tanesco lilitarajiwa kukusanya kiasi cha Sh115 bilioni kutoka kwa wateja wake, hivyo kubakisha pengo la Sh408 bilioni ambazo Serikali iliahidi kwamba ingezitafuta katika vyanzo vingine.

Zitto alisema kutokana na hali hiyo, wabunge wanatarajia kuhoji katika Mkutano wa Tano wa Bunge la 10 unaotarajiwa kuanza Novemba 8, mwaka huu mjini Dodoma na kuitaka Serikali iwe na majibu.

“Kuna masuala ya ‘procurement’ (ununuzi), sheria lazima ifuatwe sasa ukiangalia mfano watu wa NSSF (Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii) ambalo linatakiwa kuzalisha megawati 150, hadi sasa bado hawajaanza kuingiza umeme kwenye gridi ya taifa, lakini Serikali ilileta mpango wake na wakasema wana uwezo wa kuutekeleza, kazi yetu ni kusubiri majibu,” alisema Zitto.

Alisema katika mchakato wa kutafuta mashine za kuzalisha umeme, NSSF lilinusurika kutapeliwa pale wataalamu wake walipofika Marekani na kubaini kwamba mtu waliyekuwa wakiwasiliana naye kwa ajili ya kupata mtambo huo, hakuwa na mashine wala kampuni ya aina hiyo.

Kauli hiyo iliungwa mkono na January aliyesema: “Kwanza ukiangalia mpango wenyewe wa dharura, vyanzo vyote ni vya mafuta au mafuta mazito ya dizeli au ya ndege. Huu umeme ni ‘very expensive’ (ghali mno), kwa nchi ambayo ni tajiri wa makaa ya mawe, gesi asilia na rasilimali nyingine.

Ni ‘scandal’ (kashfa) kutumia umeme huu,” alisema January na kuongeza: “Nasema ni ‘scandal’ (kashfa) kwa sababu kitaalamu umeme unaotokana na makaa ya mawe gharama yake ni senti 10 hadi 12 za Marekani kwa megawati moja, gesi ni kati ya senti za 8 hadi 12 za Marekani wakati umeme wa mafuta ni senti kama 42 za Marekani, sasa mtaona jinsi tunavyopoteza fedha nyingi kwa sababu zisizo za msingi.”

Alisema ukodishaji wa mitambo ya umeme wa dharura inayotumia mafuta ni mzigo kwa walipa kodi ambao ni maskini na kwamba fedha zinazotumika zingeweza kugharamia shughuli nyingine za maendeleo.

Alisema kwa taarifa alizonazo, kampuni ambazo tayari zimeingiza umeme wa dharura ni Symbion (megawati 37), IPTL (megawati 80) na Agrreko (megawati 50) na kwamba kiasi hicho cha umeme hakifikii nusu ya kile kilichoahidiwa na Serikali bungeni ambazo ni megawati 572 hadi Desemba mwaka huu.

Mbunge huyo alisema ikiwa umeme huo wa dharura hautapatikana wote ifikapo Desemba, basi hakutakuwa na maana ya dharura na kwamba hapo Serikali itabidi ipitie upya suala la malipo kwa kampuni husika.

“Dharura maana yake ni kutupatia umeme ‘within’ (kati ya) sasa na Desemba, sasa kama hadi leo NSSF hawajaweza kutupa zile megawati 50 tulizoahidiwa kwamba zitakuwa tayari Septemba na tunawadai na hizi nyingine za Oktoba, sidhani kama wanaweza kutimiza ahadi hiyo, hivyo lazima hili tuliangalie na hii ni kazi yetu sisi wabunge,” alisema January.

Chini ya mpango wa dharura, NSSF wanatarajiwa kuingiza katika gridi ya taifa megawati 150 za umeme, Symbion megawati 205, Agrreko megawati 100 na IPTL megawati 80 ambazo tayari zimeingizwa baada ya kupatikana kwa mafuta mazito.

Vyanzo mbadala Kutokana na athari za mgawo wa umeme, wabunge hao waliitaka Serikali kuchukua hatua za kutekeleza ushauri ambao umekuwa ukitolewa na wabunge na wataalamu wa nishati.

Katika matamshi yao, wabunge hao kutoka kambi mbili tofauti bungeni, walikubaliana kwamba kimsingi suala la matumizi ya gesi na makaa ya mawe ndiyo suluhisho la matatizo ya nishati ya umeme nchini lakini wakaiponda Tanesco kwamba haina uwezo wa kusimamia sekta hiyo peke yake.

Kwa mujibu wa takwimu za kitaalamu, miradi ya makaa ya mawe ya Ngaka mkoani Ruvuma, Kiwira mkoani Mbeya na Mchuchuma mkoani Iringa, ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,500 za umeme kwa miaka 150, hivyo kulisaidia taifa kuondokana na giza.

Zitto alisema suala la Tanesco kufanyiwa marekebisho kwa maslahi ya Taifa halina mjadala ili kuliwezesha kufanya kazi kwa ufanisi tofauti na sasa ambako limeshindwa kukidhi matakwa ya umma.

“Shirika hili linaweza kugawanywa sehemu mbili, kukawa na uzalishaji peke yake na sehemu ya usafirishaji na usambazaji nazo zikawa peke yake maana hivi sasa haliwezi kufanya kazi yake ipasavyo,” alisema Zitto.

Hata hivyo Naibu Kiongozi huyo wa upinzani Bungeni na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, aliwalaumu wanasiasa kwa kuingilia utendaji wa Tanesco na kwamba matatizo mengi ya shirika hilo la umma, yamechangiwa na kutolewa kwa maelekezo ya kisiasa yanayopingana na utaalamu.

“Lazima sasa kila mtu atekeleze wajibu wake, Tanesco tuwaachie wataalamu, Serikali ibaki na masuala ya kisera na sisi wabunge tubaki na ‘role’ (nafasi) ya usimamizi, hapo tutasonga mbele,” alisisitiza Zitto.

Katika maoni yake, January alisema Tanesco haiwezi kumudu kusimamia miradi mikubwa ya umeme na kwamba ipo haja ya kugawanywa katika sehemu tatu kwa maana ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ili kuongeza ufanisi wake.

Alisema kugawanywa kwa shirika hilo kutapunguza upotevu wa umeme ambao kwa takwimu za mwaka jana, ulipotea kwa asilimia 25, kiwango ambacho ni sawa na umeme wote uliotumiwa viwandani au asilimia 75 ya umeme wote unaozalishwa na kampuni ya Songas.

“Kuna matatizo mengi sana ambayo yanapaswa kutatuliwa, kwani upotevu wa umeme mwingi kwa kiasi hiki na ni hatari sana, nadhani marekebisho yatakayofanywa yanaweza kusaidia kuondoa matatizo hayo,” alisema.

Ngeleja, Tanesco Katika mdahalo wa juzi, viongozi wa Serikali waliingia mitini kwa maelezo kwamba Waziri pamoja na watendaji wote wa sekta ya umeme katika Wizara ya Nishati na Madini wako safarini.

Mwenyekiti wa Mdahalo huo, Rosemary Mwakitwange alisema, Waziri Ngeleja alikuwa amealikwa na kwamba kulikuwa na ahadi kwamba lazima Serikali ingewakilishwa lakini akashangazwa na kutoshiriki kwao katika tukio hilo.
Kwa upande wake, Tanesco liliwakilishwa na Mkurugenzi wake wa Uwekezaji, Katyega Maneno ambaye alipata wakati mgumu pale alipotakiwa kujibu hoja za washiriki wa mdahalo huo.

Katyega alisema Tanesco linafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa umeme wote wa dharura unaanza kuzalishwa kabla ya Desemba mwaka huu kama Serikali ilivyoahidi.

“Tumeshajiandaa hata kama itatokea kampuni moja ikashindwa kutimiza mahitaji yetu, basi tuko tayari kila kitu kitakwenda sawa. Hata sasa kuna unafuu kwani makali ya mgawo yamepungua,” alisema Katyega.
Jana, gazeti hili lilimtafuta Ngeleja kupitia simu zake mbili za kiganjani ili kufahamu msimamo wake kuhusu kuelekea kushindwa kwa mpango wa dharura bila mafanikio.

Hata hivyo, waziri huyo aliwahi kukaririwa akisema hayupo tayari kujiuzulu kwa maelezo kwamba yeye si chanzo cha matatizo ya umeme nchini.
Alisema hayo Julai 19, mwaka huu mjini Dodoma, siku moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuondoa bungeni bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ili iandaliwe upya baada ya kuwa imekataliwa na wabunge.

Kukataliwa huko ndiko kulikozaa mpango wa dharura ambao sasa unaonekana kutotekelezeka hivyo kumweka waziri huyo kwenye wakati mgumu zaidi Bunge litakapokutana tena mwezi ujao.

Ngeleja katika maelezo yake, alisema tatizo la nishati ya umeme ni la Serikali nzima na si yeye peke yake anayepaswa kulaumiwa.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Back
Top Bottom