Zitto, Makamba na mwakilishi wa TANESCO ndani ya mdahalo wa Star Tv

Zitto, Makamba na mwakilishi wa TANESCO ndani ya mdahalo wa Star Tv

KAMISAA, usipige kelele hapa jukwani hata kama ndio Makamba mwenyewe - jibizane na HOJA hapo juu na ukaridhishe Wana-JF ili tukaamini vinginevyo mkuu acha kupiga kelele JF kalete data tu au kapinge hiyo barua hapo juu kwa.
 
Kwani lazima iwe CCM vs CDM? What about watanzania wakijadiliana kama watanzania?

kweli kabisa hii ndio approach nzuri zaidi.
Hakuna mpiganaji asiye na weakness. Lakini udhaifu wake haupunguzi au kuondoa element ya upinai wake. Zitto ni muhimu sana ktk vita hii na Mnyika pia. Makamba pia ni muhimu. Tusishau lengo letu wananchi. Sio kuwa na viongozi wazuri.hio ni approach au plan yetu. Lengo letu ni kuwa na maendeleo ya kweli, amani, uhuru, haki na furaha kwa kuwatumia viongozi wote wa aina zote kutupeleka huko all the zittos, mremas, slaas, makambas and the rest will come and go lakini lengo letu liko pale pale.
 
KAMISAA, usipige kelele hapa jukwani hata kama ndio Makamba mwenyewe - jibizane na HOJA hapo juu na ukaridhishe Wana-JF ili tukaamini vinginevyo mkuu acha kupiga kelele JF kalete data tu au kapinge hiyo barua hapo juu kwa.

Kwahiyo kwako wewe hii sentensi ya "set to turn discussion into action" maana yake ni kwamba anaenda kuingia mkataba kwa niaba ya Serikali? LOL Duuh kweli kazi tunayo.
 
Kwavile pengine ni Threads za majungu na za kuchafuana zisizokuwa na ukweli wowote. Umeshatafakari hilo?

We kumbe ndiye January Makamba mwenyewe ndio maana upata na presha kiasi hiki?????????? Sasa ukiendelea kubisha basi utashangaa uvundo woooote ule mzito zaidi ukimwagwa hapa. Nimekusoma kwenye hizo THREADS hapo juu na umeeleweka.
 
Logic unayotumia ni nyepesi sana. Hata mimi naweza ku-pull kila ulichopost. Haelezei kila kitu kuhusu mimi, tena haimaanishi kwamba mimi ni Makamba. Jaribu tena.
 
Katika soma soma ya hii thread muhimu sana kwa sie ambao hatukuuona mdahalo live. Naomba kuuliza nadhani nimepitwa na kitu.
Je lengo lake lilikuwa nini? Je wahusika walioitwa kuongea na kuchangia walikidhi mahitaji ya kufikia lengo? Je hatimaye lengo lilifik? Yani pale mwisho wa 'debate'.
Mimi kama engineer lakini nje ya mfumo unaoendesha decisions Tanzania bado napenda kupanga mawazo yangu kwas kusolve problems hivyo kwa hapa nahisi kiu yangu bado kushibishwa.
 
Haya yametimia Zitto sikuona jipya alosema, nilichoona ni kojipendekeza sana kwa Makamba na ubinafsi wa kutetea mambo yake, hajaiwakilisha cdm ni vyema ingesemwa wazi kuwa ameenda kama zitti na cdm isihusishwe na maoni yake hayo sio ya chama. Bora makamba ambaye alizungumzia masuala ya Tanesco na kuyahusisha na scandal, Kutokuwajibika na uwaziri wa aibu usio na ahadi za utekelezaji. Zitto hafai cdm ahamie ccm, upuuzi mtupu
 
umeona hee!!!sijuui wanaongea nini,sioni challenge,wanaongea kama watoto wa baba mmoja


kwa akili yako ulitaka zitto aongee kwa kumshambulia makamba......hukuelewa madhumuni ya mdahalo wewe
 
Hakika ni maswali yenye mashiko sana kwamba mara baada yo huo mdahlo wa Star TV then WHAT NEXT????

Katika soma soma ya hii thread muhimu sana kwa sie ambao hatukuuona mdahalo live. Naomba kuuliza nadhani nimepitwa na kitu.
Je lengo lake lilikuwa nini? Je wahusika walioitwa kuongea na kuchangia walikidhi mahitaji ya kufikia lengo? Je hatimaye lengo lilifik? Yani pale mwisho wa 'debate'.

Mimi kama engineer lakini nje ya mfumo unaoendesha decisions Tanzania bado napenda kupanga mawazo yangu kwas kusolve problems hivyo kwa hapa nahisi kiu yangu bado kushibishwa.
 
Nashukuru jana nimefanikiwa kuangalia mjadala huo moja kwa moja hapa Mbweni zanzibar kupitia star TV. Tathmini yangu ni kuwa Mjadala ulitawaliwa na wana siasa zaidi kuliko mtaalamu ambaye aliyekuwa mwakilishi wa Tanesco.

Inasikitisha sana kuona mjadala huu unakuwa wa kisiasa zaidi kuliko kitaalamu zaidi. Kwa kuwajuza kuwa Mh Zito alitumia dakika 17.36 na Makamba alitumia Dakika 14.53. Na Eng Maneno (mwakilishi wa Tanesco) pamoja na kubaniwa na kukatishwa katishwa na moderator (Mwakitwange) alitumia dakika 7.36.

Kwa mustakabali huo utaona ulikuwa mjadala wa kisiasa zaidi na sio kitaaluma na huu ni msiba mkubwa sana kwa Wa Tanzania kusimamia siasa hata kwenye mambo sensitive ya kiuchumi..
 
This is paranoia at its best. Hivi nani kakuambia anaenda kuingia mkataba kwa niaba ya Serikali? Mamlaka ya aina hiyo hana. Hawezi kuwakilisha Wizara wala TANESCO kwa vile yeye sio mtendaji, ni Mbunge wa kawaida na sio mwakilishi wa Serikali. Sioni wapi ni dhambi kwa yeye kuhudhuria mkutano, mdahalo au panel discussion kwa niaba yake binafsi au kwa ruhusa ya Ofisi ya Spika ndani au nje ya nchi.

Paranoia? Naomba tafsiri sahihi ya hiyo sentence hapa chini especially kwenye underline! Na kwenye list ya participants so far sioni law makers kwa maana ya wabunge or if you like wenyeviti wa kamati za bunge toka nchi nyingine except Makamba! Huo uenyekiti unatumika kiujanja sana. Kuna mtu katukumbusha humu jamvini kuwa huyu dogo huwa hataji neno ufisadi' kabisa. I wonder why?

"JANUARY MAKAMBA, Chair of Tanzania's Parliamentary Committee for Energy and Minerals is set to turn discussion into action"
 
Nashukuru jana nimefanikiwa kuangalia mjadala huo moja kwa moja hapa Mbweni Zanzibar kupitia star TV. Tathmini yangu ni kuwa Mjadala ulitawaliwa na wana siasa zaidi kuliko mtaalamu ambaye aliyekuwa mwakilishi wa Tanesco.
Inasikitisha sana kuona mjadala huu unakuwa wa kisiasa zaidi kuliko kitaalamu zaidi. Kwa kuwajuza kuwa Mh Zito alitumia dakika 17.36 na Makamba alitumia Dakika 14.53. Na Eng Maneno (mwakilishi wa Tanesco) pamoja na kubaniwa na kukatishwa katishwa na moderator (Mwakitwange) alitumia dakika 7.36.katika mjadala mzima


Nilizidi kusikitishwa na wasomi tena pasi na shaka wanaheshimika katika Tanzania wanapojikita katika siasa na kuuliza masuala ya kisiasa badala masuala ya kiuchumi. Mfano Dr Mkumbo aliuliza suala la kitoto ya kutaka kubadilisha gari baada ya miaka 50 pasi na kufahamu kuwa uongozi ni kazi na hakuna mwenye uwezo wa kubadilisha wa Tz kwa hulka zenu. Nashukuru Mh Makamba alivomjibu suala lake la kitoto na nafikiri mwenyewe aliona aibu kubwa.

Nilisikitika sana kuona Bi Mtema alipoona akina Zitto na makamba walivyobainisha ukweli kuhusu lost electricity kutoka kwenye transmission lines za Tanesco. Sasa yeye alitaka wakina zitto wasitoe ukweli huo hadharani ili watu wajue. Hii inaonyesha kiongozi kama huyo anaficha ukweli siku zote na kupenda watu waseme uongo.

Ninatoa pongezi sana kwa Zitto na makamba kwa ufafanuzi mzuri sana, ila sikupenda moderator Raso Mwakitwange kwa kuufanya mjadala ule kuwa wa kisiasa zaidi na sio kitaaluma kwa kumnyima fursa hiyo mwakilishi wa Tanesco ambaye wengi tulitegemea angetumia muda mwingi sana kutoa ufafanuzi kutokana na mada husika.

Hakika huu ni msiba mkubwa sana kwa Wa Tanzania kuwa na moderator wa kisiasa hata katika mambo sensitive ya kiuchumi..

Nawapa pole wa Tz kwa hilo.
 
Haya yametimia Zitto sikuona jipya alosema, nilichoona ni kojipendekeza sana kwa Makamba na ubinafsi wa kutetea mambo yake, hajaiwakilisha cdm ni vyema ingesemwa wazi kuwa ameenda kama zitti na cdm isihusishwe na maoni yake hayo sio ya chama. Bora makamba ambaye alizungumzia masuala ya Tanesco na kuyahusisha na scandal, Kutokuwajibika na uwaziri wa aibu usio na ahadi za utekelezaji. Zitto hafai cdm ahamie ccm, upuuzi mtupu

Ndugu yangu wazungumzaji wakuu kwa upande wa wabunge hawakua wanawakilisha vyama vyao,walikua wanawakilisha kamati za bunge. Kama ingekua ni CCM vs CDM basi tungewaona Ngeleja na Mnyika wakipambana ktk mdahalo wa leo.
 
jaman jana wakati zitto anatoa msimamo wake kuhusu malipo ya dowans star tv walikata matanagazo yao kwa upande wa sauti sijui ni kwa nn mawazo yenu wajenwn
 
Jamani mnyika ni form six leaver kama Dj mbowe sasa ataongea nini zaidi ya kwamba solution ni kuandamana.tatizo la wanaJF chanzo chao cha habari ni mwanahalisi pekee.
 
Paranoia? Naomba tafsiri sahihi ya hiyo sentence hapa chini especially kwenye underline!

Na kwenye list ya participants so far sioni law makers kwa maana ya wabunge or if you like wenyeviti wa kamati za bunge toka nchi nyingine except Makamba!

Huo uenyekiti unatumika kiujanja sana. Kuna mtu katukumbusha humu jamvini kuwa huyu dogo huwa hataji neno ufisadi' kabisa. I wonder why?

"JANUARY MAKAMBA, Chair of Tanzania's Parliamentary Committee for Energy and Minerals is set to turn discussion into action"

Dear Colleague

We would like to draw your attention to the following executive dialogues. Please see the attached flyer for more information.

Powering Africa: the Gas Option (PAGO 2) to be held at Serena Beach and Spa, Mombasa 7 - 9 November

Join Africa's decision-makers to share experiences and explore solutions with Government officials, utilities and energy agencies at this high-level, interactive dialogue examining the future of Africa's gas.
Latest PAGO and PAFO confirmed organisations include:

  • January Makamba, Parliamentary Committee for Energy and Minerals, Tanzania
  • Ministry of Electricity and Dams, South Sudan
  • Ministry of Energy and Mining, South Sudan
  • Nigerian Electricity Regulatory Commission
  • World LP Gas Association
  • International Finance Corporation
  • Kenya Electricity Generating Company
JANUARY MAKAMBA, Chair of Tanzania's Parliamentary Committee for Energy and Minerals is set to turn discussion into action. Makamba confirms participation and attendance at this senior level debate on the development of gas and power across Africa. With stakeholders from Kenya, Mozambique, Namibia, Nigeria, the UNEP, IFC as well as major international players from Siemens, GE and Cummins this is a major opportunity for your organisation to join this important 'call for action'.
Powering Africa: the Financial Options (PAFO 5) to be held at Serena Beach & Spa, Mombasa, 9 - 11 November
Meet and engage with a range of Government officials, power executives and utilities from the public and private sector to discuss and act on investment opportunities across Africa. Please contact Amy Offord at [email protected] for more information or to receive a programme.
Yours sincerely,

Amy Offord
EnergyNet Limited
London
[email protected]
+44 (0)20 7370 8704

HOJA YANGU:

Je, kuna usahihi gani January Makamba, Mwenye kiti tu wa Kamati ya Bunge kuhusu Nishati na Madini, kwenda kuwakilisha Tanzania kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu maswala ya gasi yetu hapa nyumbani na pengine kuingia kwenye mikataba mengine ndoano zaidi wakati yeye si waziri na Waheshimiwa Ngeleja na John Mnyika wao wapo tu????

Na kapata wapi baraka za kwenda kuingia kwenye mikataba kwa niaba yetu (he is going to turn dialogue INTO ACTION)?

Nielewavyo mimi Kamati yoyote ya Bunge letu kazi yake ni WATCHDOG (Legislative arm of the government) wa wananchi kwa niaba ya bunge ili kuhakiki kila walitendalo SERIKALI kama Executive arm of the government hivyo watendaji ni Ngeleja na John Mnyika. Hao ndio Executive hapa nchini kuhusu masuala ya nishati na madini full STOP.

Sasa kwa kuwa tu kuna harufu ya pesa kukopwa kwa jina letu kutoka IFC na vile vile kwa mkono mwingine kuna utitiri wa mikampuni ama inayojenga miundombinu ya gesi, inayosafisha, inayosafirisha na inayouza - tena haya mambo mazito ya kuingi mikataba ya miaka nenda rudi apewe tu huyu kimya kimya hivi halafu kushirishwa kulia baadaye??????

Everyone watch out!!!
 
Mhmm kweli Tanzania inaongozwa na vipofu na viziwi, hivi kazi ya viongozi ni kufanya midahalo au kutenda kazi zionekane?

Kama si wapuuzi hawa watu basi ni wajinga nadhani mdahalo ungeweza kufanywa na academia na si watendaji! Umeme haupo na wao ndio viongozi mdahalo wanini badala ya kuleta umeme? Enyi Watanzania mtaendelea kuchaguwa hawa viongozi mbumbumbu hadi lini? Viongozi wa tume na uchunguzi na midahalo! Vipi nyie hamuoni aibu kulipwa kwa kodi za Watanzania kufanya kazi msiyoijuwa wala kuiweza?
Hii nimeshindwa kujizuia ikabidi ni log in ku ilike kabla sijaendelea na shughuli zangu.Well said!
 
Back
Top Bottom