Wana jf,mheshimiwa Zitto anasema wanasiasa wanaingilia tanesco,na kama nilimuelewa vizuri moja ya sababu ya kusema hivyo ni sakata zima la richmond.
Ninachojiuliza hivi ni wanasiasa ndio waliingia mkataba kati ya tanesco na richmond na baadaye dowans au ni tanesco wenyewe, na kama kuna wanasiasa ambao mh Zitto anaamini wanaingilia tanesco awataje kwa majina kuliko kutoa madai kwa ujumla tu. Mh Zitto namwamini kwa ujasili alionao, hivyo namuomba awataje kwa majina hao wanaoingilia utendaji wa tanesco.
Naomba kuwasilisha