Zitto, Makamba na mwakilishi wa TANESCO ndani ya mdahalo wa Star Tv



Wakuu mimi nadhani ZITTO baada ya hadithi zao zisizokuwa na tija kwa sisi walala hoi,tuta muomba aje kujibu maswali ya wanajamvi,juu ya uhalali wake wa kuwepo katika mdahalo na si waziri kivuli MNYIKA????????????????????????? Na pia mnyika nadhani yupo jamvini sasa anaweza tujuza juu ya hili,maana linatutatiza sisi wafuja jasho.
 
zitto aje hapa jamvini aseme ni kwann aende yeye wakati waziri kivuli yupo? Hiki kitakuwa kimbele mbele na uroho wa madaraka. Km kwenye midahalo tu anakuwa mroho hv je akipata huo urais si atakuwa anaenda hadi kwenye midahalo ya kata

urais wa kuongoza nani? Zitto hana charisma ya kuwa rais kwani lengo lake ni kupata ujiko na kutimiza malengo binafsi zaidi na siyo kuwaletea watanzania maendeleo wanayotaka. Zitto yuko tayari kuwasaliti wenzake tu ili kupata nafasi ya urais kwa maana hiyo mtazamo wake uko very myopic kwenye cheo zaidi kuliko outputs ya kazi yake . Akigombea labda wamchague huko huko kwao kwani is very unfit for presidential post now and in the future
 
Mpango wa Dharura wa kumaliza tatizo la umeme haukuwa realistic - zitto
 
umeona hee!!!sijuui wanaongea nini,sioni challenge,wanaongea kama watoto wa baba mmoja
 

asante ndugu yangu.
 

hivi mkuu una background ya zito??hivi alizaliwa wapi na kukulia wapi??ningefurahi sana kumjua huyu mtu
 
Umeme umekatika wakuu, mwanangu wa miaka minne ananiuliza, je, ni luku imeisha au mgao wa umeme?...
 
Mpango wa tanesco ilikuwa kufikia 500MG za umeme toka August had Disemba, 2011, lakini hadi leo hatuoni kitu, - makamba
 
licha ya mwakilish wa tanesco kudai mikoa ambayo haiko kwenye grid hawana mgao, upo na kwa taarifa leo hi umeme ulikatka kwa zaid ya sa 4 sumbawanga na mida hii ninapoandika umekatika na hivo mdahalo huku basi. licha ya kuwa rukua iko kwenye grid ya zambia
 
kuto kuwepo kwa uwakilishi wa wizara ya nishati na madini , sidhani kama tutapata suluhisho juu ya maswali kama lini hii miradi itakamilika na mgao utaisha lini maana zimekuwa ni kama hadithi za paukwa pakawa.
 
Ndugu Chacha, anauliza swali kwa Mwakilishi wa TANESCO: Nani unamwogopa kusema ukweli ili sisi wananchi tukusaidie??
 
Mh! Mwakilishi wa tanesco hovyo kabisa !

siohajiwezi ndio uwezo wake alio nao kama anaumwa vile,sasa ngoja apigwe maswali na vijana wenye uchungu wa nchi,wanao fikiri 100000000000000 times,atajuta kutumwa kuwakishi wajinga wenzake
 
sijawahi ona mdahalo unaboa kama huu,zito na january ni kama wametumwa kuongea pale,sioni tofauti ya zito na january,nimekubali zito yupo kwenye payrol ya ccm,nimezima tv
umezima tv ya hotelini nani kakuruhusu,wewe si umesema upo rombo green view sasa nyumbani umefikaje? ukiwa muongo uwe na kumbukumbu Director
 
kuto kuwepo kwa uwakilishi wa wizara ya nishati na madini , sidhani kama tutapata suluhisho juu ya maswali ya msingi juu ya lini hii miradi itakamilika na mgao utaisha lini maana zimekuwa ni kama hadithi za paukwa pakawa.

Mkuu, kwa mjibu wa TANESCO, wanasema wao ni Independent Firm hawafanyi kazi kwa maelekezo ya wanasiasa... Wizara kwa mjibu wake haiwasaidii......May be.....
 
Mwita Naunga mkono hoja yako. Hoja nyingi hapa hazina msingi, hii ni nchi yetu, kila mwnchi anahaki ya kusimama na kutoa mwanga kwa wengine, swala la umaaru, ni uswahili na upofu wa fikra.

Mpira wa miguu kila mchezaji kwa nafasi yake eti inapotokea beki kufunga refa huwa analikataa bao, kwa nini beki atoke ktk nafasi yake na kuingilia nasi ya mshambuliaji. Sijaona, Bila kuwa kama timu inayoitaji ushindi wa dhati tukaleta malumbano ambayo si kwa nia ya kizalendo
 
umezima tv ya hotelini nani kakuruhusu,wewe si umesema upo rombo green view sasa nyumbani umefikaje? ukiwa muongo uwe na kumbukumbu Director

Mie nilikuwa namwangalia akanitia hata uvivu kumjibu huyu director 1. Saizi anataka kujua background ya Zitto. Kazi anayo!m
 
umezima tv ya hotelini nani kakuruhusu,wewe si umesema upo rombo green view sasa nyumbani umefikaje? ukiwa muongo uwe na kumbukumbu Director
Nilitaka kumuuliz swali hilo.
 
Hili ndio tatizo la wabongo; yaani badala ya kujadili issues, sis tunajadili watu! hoja hapa ni nishati na Tanzania Tunayoitaka, hii ndio hoja ya kujadiliwa na sio zitto wala januari hapa! anayeandaa mjadala ana haki ya kumualika mtu yeyote yule ambayae kwa fikira zake yeye anaona kuwa ataweza kufanikisha hoja yake ieleweke kwa wananchi.

Pia naomba muelewe kuwa kila mtu anahaki ya kukutana na watu wengine; na pia anauwezo wa kutoa maoni yake popote pale na kwa kutumia chombo chochote kile, kwa hiyo si lazima zito apate ruhusa kutoka kwenye chama chake kwa ajili ya kutoa maoni yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…