Unajua tofauti baina ya wanasiasa nchi za Magharibi na kwetu ni kwamba wao hufiikiria siasa ktk kukidhi Mahitaji.. Na wasomi huumiza vichwa kutafuta njia mbadala za kukidhi mahitaji hayo kulingana na uwezo uliopo...Kwa mfano, Hitler pamoja na ubaya wake wote lakini atakumbukwa kwa mafanikio ya Germany. yeye alikuwa akiona mahitaji ya kitu hutoa amri kwa wasomi waumize vichwa kutafuta solution na kulikuwa hakuna excuse ama neno haiwezekani kwani kama ilikuwa haiwezekani Hitler huwajibu - Hakuna kitu kisichowezekana maadam kinahitajika - Fanya iwezekane!. Na ajabu, iliwezekana.
Leo hii sisi wanasiasa wetu na wasomi wanazungumzia zaidi madhara yatokanayo na kutoweza kukidhi mahitaji hadi imefikia hali ya hatari kwa maisha yetu. Ni sawa na kutafuta solution ya hali ya maisha ya Somalia kiuchumi baada ya vita vya miaka 30, na ndio maana ktk fikra za mwanadamu hata yule msomi hufikiria zaidi tutaweza vipi kuwasaidia Wasomali watokane na adha ya Umaskini, njaa na maradhi wakati tunashindwa kutafuta the core problem ya umaskini na dha zote zimetokana na Vita.. Ukiweza kusimamisha vita itakuwa rahisi kwa Somalia kurudi ktk hali yake lakini in due time misaada isisimame..
Tatizo la Tanzania ni UFISADI mkubwa unaofanywa na viongozi wetu, hakuna sababu nyingine yoyote na hakika inasikitisha sana tunapojivunia maendeleo ya kusambaza umeme toka asilimia 1 hadi 14 wakati mahitaji ya umeme kiuchumi kwa nyakati hizo mbili ni tofauti kabisa. Hiyo asilimia 1 mwaka 1961 iliweza kukidhi asilimia 80 ya mahitaji ya umeme tulowekeza ktk uchumi wakati ule, tofauti na leo tunaposambaza kwa asilimia 14 wakati mahitaji yanayokidhiwa kiuchumi ni chini ya asilimia 50 ya uwekezaji. Ndio maana tuna mgao wakati haikuwa hivyo mwaka 1861.
Kwa hiyo tunashindwa kuitazama picha kubwa ya mahitaji (demand) badala yake tunatazama zaidi kusambazwa kwa umeme nchini kama vile chakula cha watu watano kinavyoweza kusambazwa ktk sahani 10 za walaji na tukachukulia hizo sahani kumi kama toshelezo la mahitaji ya chakula kwa watu 10..Kisha watu wakitoka pale hawakushiba tunajiuliza imekuwaje wakati tumeweza kutoa sahani 10 tofauti na mwaka jana walikuwepo watu 5 walikula ktk sinia moja! - iliwezekana vipi wakashiba?...
Kwa hiyo kwa kila ongezeko la Megawatts nchini haliwezi kuhesabiwa kama maendeleo ikiwa mahitaji ya megawatts ni kubwa kuliko mwaka 1961. Kaa leo tunahitaji megawatts 2000 ili kuendesha shughuli zetu basi inabidi tuwe na uwezo wa kuzalsha megawatts 2000 za umeme! Huwezi kulazimisha mahesabu na kusema leo hii tunazalisha Megawatts 600 bila kujali kiwango cha mahitaji kwani mwaka 1961 pengine tulihitaji megawatts 60 tu ktk uzalshaji wa uchumi, hivyo megawatts 45 zilizozalishwa enzi hizo ni sehemu kubwa sana kiasilimia ktk maendeleo ya uzalishaji kuliko 600 tunazozalisha leo chini kabisa ya kiwango cha mahitaji.
Maadam tuko nyuma na tunazidi kurudi nyuma ya mahitaji - Umeme ni tatizo kubwa, ni adha inayopatiwa ufumbuzi wa dharura kama tunavyowasaidia Wasomali, bado kabisa hatuna mipango ya kutazama kasoro zetu. Siku tutakapoweza kukapambana na the core problem ya umaskini wa Mtanzania kwa kuelea kwamba tunajenga sera za kiuchumi zinazotafuta suluhu ya MATATIZO yanayotukabiri, sera za dharura kuepuka lawama kubwa za wananchi ktk ukosekanaji wa umeme, basi tutajikuta tukiendelea kuweka mikataba mibovu, haraka ya kujenga hata miradi chini ya kiwango kaa tulivyofanya ktk ELIMU, AFYA na BARABARA..kote huko hakuna maendeleo isipokuwa ni sawa na kupeleka misaada ya mahema, chakula, madawa na maji huko Somalia...Tunawapunguzia matatizo ya umaskini, njaa na maradhi.