Zitto: Msaidizi wa Maalim Seif alinipigia simu mara 4 kutaka kunijulisha msiba sikupokea ndipo akanipigia Rais Mwinyi nikapokea kwa mujibu wa sheria

Zitto: Msaidizi wa Maalim Seif alinipigia simu mara 4 kutaka kunijulisha msiba sikupokea ndipo akanipigia Rais Mwinyi nikapokea kwa mujibu wa sheria

Mleta mada unachekesha.
"Eti zitto anatajwa kugombea urais 2025."
urais wa nchi gani?
 
Zitto bhana, sasa alipokea simu kwa mujibu wa Sheria kwani Mwinyi alikuwa akimuona kwamba amekataa kupokea ama la, hawa wanasiasa wana mambo kweli
 
Haikuwa daharau mkuu kutokana na hal aliyokuwa nayo maalim lazma hofu ingemjaa..
Kwa umri na majukumu makubwa ya kitaifa utayari wa kupokea jambo na ukomavu wa akili ni muhimu na lazima, kuogopa kusema anaogopa kupokea sim sababu ya ugonjwa ni utoto sana.

Mimi kwa umri wangu na nafasi yangu kijamii nikiwa na mgonjwa katika hali yoyote napiga sim na napokea sim tena naweka sauti ya juu nisikose kupokea
 
My take; Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.


Roho yako ni ngumu kama jiwe wala huwezi kushikwa na huzuni ya kifo cha mtu.
 
Masikini wewe Johnthebabtist, yaani hata humjui mtu mwoga kabisa wewe...

Alichokifanya Zitto Kabwe wala sio woga. Bali ni hali ambayo iko na inaweza kumtokea kila mtu ukowemo wewe..

Alichofanya Zitto Kabwe ni Ku - avoid jambo fulani kwa muda ukijiandaa kuwa tayari kulipokea...

Ni kawaida kabisa hili. Na usifikiri kuwa hata Rais Mwinyi alilipokea hili na kulikubali kwa urahisi tu. Siyo hivi...

I am sure, it took him several time to accept this...
 
Ingawa ZZK Sio chaguo langu, lakini hii sio kwamba alikuwa muuoga wa uoga, bali kuto penda au kuwa tayari kusikia Habari mbaya kwa Wakati huo.

Nakumbuka Kuna kiongozi moja aliwahi kuongea "kuogopa" na bado ni kiongozi
 
My take; Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.

Mbona kuna jamaa huwa haendi kabisa kwenye misiba, yeye kazi yake kutuma rambi rambi
Hili la kuogopa kupokea sim ni ujinga mwingine wa watanzania. Wengi tunachagua simu za kupokea
 
Kajinga haka! Hata msiba anataka umpe sifa ya kisiasa.
Kwa nini hakuogopa kupokea simu ya rais Mwinyi? Kwa mujibu wa sheria ipi anayosema inamlazimisha kupokea simu ya Rais Mwinyi? Rubbish!
 
Back
Top Bottom