Zitto Mshauri OMO kuwa Pragmatist,Acheni Ujinga Pelekeni Majina ya SUK, Kususa Hakusaidii KITU

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya Jumapili ya leo
Screenshot_20260111_091431_com.easy.abroad_edit_24364534014714.jpg

Naomba kuanza kwa declaration of interest,mimi na Zitto ni marafiki wa intake moja UDSM,namfahamu kwa karibu na huwa tunataniana,hivyo namfahamu ni mtu pragmatist anayefuata siasa za pragmatism Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"
View: https://youtu.be/RPpcwlnNJ0A?si=K5K-9oEDKsbVQUm4

Pili nimetumia neno la kuudhi,waache ujinga,wapeleke majina ya chama chao kuunda SUK kule Zanzibar!. Ujinga hapa ni kufanya jambo lile lile katika mazingira yale yale na kutegemea matokeo tofauti!
View: https://youtu.be/4AWaU_8FYhQ?si=TCb3xSJiXdcuuaZ8

ACT ya sasa kule Zanzibar, tangu wakiwa Cuf, wamekuwa wakishiriki chaguzi za Zanzibar na matokeo ni yale yale, wanafanyiwa kitu kile kile, hivyo hata walipokubali kushiriki wa uchaguzi huu, walijua nini kitatokea, sasa wanasusa nini?

Tangu ule uchaguzi wa 1995 ni mimi nikiwa DTV ndio nilitangaza matokeo ya kweli ya uchaguzi wa Zanzibar,na 2015 ikajirudia GE2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda hivyo hakuna kitu ambacho ACT Wazalendo,hawakukijua!

Kesho ni siku ya kumbukumbu ya miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ya January 12, Mwaka 1964, kwa vile Tanzania ni nchi ya muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, na iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kuungana kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ile April 26, Mwaka 1964. Kuna yatu wanasherehekea Mapinduzi Matukufu huku kuna yatu wamenuna, wamesusa kushiriki Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kwanza nijiunge na Watanzania wenzangu, kumpongeza Rais wa JMT, Rais Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dr, Husein Mwinyi, kwa Zanzibar kutimiza miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku waliopindua wakiyaenzi na kuyaita ni Mapinduzi Matukufu, huku waliopinduliwa wakisema Mapinduzi yale hayana utukufu wowote kwasababu yaliandamana na umwagaji wa damu, kila uchaguzi Zanzibar kuna shangwe waliopindua na kushinda uchaguzi, kuna kununa na kususa kwa waliopinduliwa ambao wameshindwa uchaguzi.
Bahati nzuri mimi nilikuwepo Zanzibar ule uchaguzi wa 1995 na ni mimi ndiye niliyetangaza yale matokeo halisi on DTV, Uchaguzi,wa 2015 nikawepo tena Zanzibar,

Kuna Watanzania wengi, hawaujui umuhimu wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hivyo wanaiona kama hii ni sikukuu ya Zanzibar, umuhimu pekee wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ndio kiini cha kuasisiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo Watanzania wapenda muungano na wazalendo wote wanchi hii, , tunapaswa kuwashukuru sana, Wazanzibari, haswa wale mashujaa wa mapinduzi, ni kupitia kwenye mapinduzi hayo, ndio kumepelekea Tanganyika na Zanzibar zikaungana kuunda Tanzania.

Asili ya Tanganyika na Zanzibar
Wakati wa uumbikaji wanchi, Zanzibar na Tanganyika lilikuwa ni eneo moja, likamegeka, ndipo visiwa vya Zanzibar, Pemba na visiwa vingine vyote vya bahari zote, huwa vinakuwa vinamegeka kutoka eneo la bara, hivyo, eneo lote la Zanzibar ni limemegeka kutoka katika eneo la Tanganyika miaka milioni nyingi huko nyuma wakati wa kuumbika, hivyo muunghano wetu adhimu ni jambo jema la kuirejesha Zanzibar kwenye asili yake kabla haijamegeka na kuwa visiwa.

Historia ya Zanzibar.
Historia ya Zanzibar ninayoiweka hapa ni ya kuanzia mwaka 1734 wakati ujio wa Sultan Seyyid Said, alipohamishia sultani yake kutoka Oman kuja Zanzibar, hakuna taarifa ya aliipataje Zanzibar, ila wenyeji wa Zanzibar kabla ya ujio wa Waarabu ni Wakwezi na Wahadimu na mkuu wao alikuwa ni Mwinyi Mkuu. Hakuna mikataba yoyote ya mauziano ya Kisiwa cha Zanzibar na Pemba kati ya Mwinyimkuu na Sultan Seyyid Said, kama mikataba ya Wajerumani kuimiliki Tanganyika, ile mikataba ya Karl Peters na Mtemi Magungo wa Msovero, au Hassan Bin Amiri kukinunua kisiwa cha Kilwa kwa gharama ya kitambaa cha kukikzunguka kisiwa chote cha Kilwa kutoka kwa wenyeji.

Kwenye ule mkutano wa Berlin wa mwaka 1884, Sultan wa Zanzibar alitambuliwa kama mmiliki halali wa Zanzibar, Pemba, na ukanda wa maili 10 ya pwani yote ya Bahari ya Hindi, hivyo Zanzibar kutoka kwa wenyewe kuwa mali ya Sultani wa Zanzibar, huku Tanganyika ikikabidhiwa kwa Wajerumani.

Baada ya Ujerumani kushindwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, WW1, mwaka 1918, Ujerumani ilinyanganywa makoloni yake yote, Tanganyika na Zanzibar zikakabidhiwa kwa Waingereza, ila Tanganyika ndio lilikuwa koloni la wakfu, trustee, na Zanzibar lilikuwa ulizi tuu, yaani protectorate ambapo Sultan ataendelea kulindwa.

Sisi Tanganyika tukapata uhuru wetu kwa Waingereza, Desemba 9, 1961, Zanzibar ikapata uhuru wake Desemba 10, 1963, kutoka kwa Waingereza, ila wakiendelea kuitambua Zanzibar ni mali ya Sultan of Zanzibar, wajibu wao ni kumlinda.

Baada ya Wazalendo wa Zanzibar kufanya mapinduzi matukufu, ambayo yalimpindua Sultani, alikimbilia Mombasa na kuomba msaada kwa Waingereza waje kumsaidia kuurejesha utawala wake visiwani Zanzibar na Waingereza wakamkubalia, wakatuma meli vita kuja kuikomboa Zanzibar.

Ndipo shujaa wa Mapinduzi, Abedi Amani Karume akaja Tanganyika kuomba msaada wa ulinzi kuyalinda Mapinduzi, ndipo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere akamshauri Karume dawa ni kuungana, kuziunganisha nchi kuwa nchi moja, Karume alikubali pale pale, “wewe rais, mimi makamo”, ndipo taratibu za muungano zikafuata, hivyo Mapinduzi ya Zanzibar, ni tukio muhimu lililopelekea muungano wetu adhimu na uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zanzibar ni nchi ya mapinduzi, mpaka sasa, siasa za Zanzibar bado zinatawaliwa na mwangwi wa yale Mapinduzi,hivyo kuna aliyepindua, CCM anayetamalaki kwa shangwe, nderemo, vifijo na shamra shamra zote kusherehehekea miaka 62 ya Mapinduzi, lakini pia yupo aliyepinduliwa, ACT, huyu amenyamaza kimya akiumia chini kwa chini na ndani kwa ndani kila akikumbuka kilichotokea kwenye uchaguzi na yatokanayo na mapinduzi hayo, na hata baada ya uchaguzi mkuu, bado wamesusa kujiunga na GNU.

Natoa wito kwa Uongozi wa ACT Wazalendo, hakuna chochote msichokijua kuhusu siasa za Zanzibar, wekeni silaha chini, teuweni wawakilishi wenu kwenye GNU, pelekeni majina, rejeeni kwenye SUK, uchaguzi mwingine ni 2030.

Na ikitokea kama OMO yeye ametosheka na ving'ora, sio lazima awe yeye, wampe hata Jussa, Dimani au hata Ally Saleh Albeto.

Natoa wito kwa Rais Samia, na rais Mwinyi, kufanyia application ya zile 4R za Rais Samia kuinusuru SUK. Japo SUK imeleta mshikamano, lakini bado kuna changamoto mbalimbali zikiwemo Changamoto za muungano ambazo zamani zilikuwa zikiitwa kero za muungano, kule Pemba wanaziita makero

Hongera Zanzibar kwa Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mungu Ibariki Zanzibar

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya Jumapili ya leo
View attachment 3528415

Naomba kuanza kwa declaration of interest,mimi za Zitto ni marafiki wa intake moja UDSM,namfahamu kwa karibu na huwa tunataniana,hivyo namfahamu ni mtu pragmatist anafuata siasa za pragmatism,Thread 'Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"' Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"

Uliposema unampongeza huyu mwizi wa uchaguzi na muuwaji nikaishia hapohapo sikuona haja ya kuendelea kuusoma huu uchafu
 
Utakuwa ni uzuzu wa hali ya juu kwa ACT kujiingiza tena kwenye Serikali ya umoja wa kitaifa kwa mara nyengine.

Walikosea tangu mwanzo kwa maridhiano ya kilaghai. CCM waendelee kuiba kura halafu wawape umakamo ambao hata tarishi kwenye ofisi za Serikali hauheshimu. Kuingia ni kujidhalilisha tu.

Kwani si ni mwezi wa tatu sasa mambo yanakwenda bila ya wao.

Na mabadiliko yako njiani. Yataanzia bara.
 
Huu muungano wa lazima kwa ajili ya hizo maili kumi za ukanda wa Pwani kuwa ni za Zanzibar zitawatesa ccm sana. Mtalazimisha kupora kila uchaguzi ili kutunza siri ambayo haina ulazima wowote. Na tunavyoendelea umwagaji mkubwa wa damu lazima ufanyike ili ccm itoke madarakani. Na mbegu ya umwagaji huo wa damu imepandwa rasmi mo29. Watu watauana, kisha ccm ikitoka madarakani ndio siri ya muungano itawekwa wazi kuwa hizo 10miles za ukanda wote wa Pwani zilizikuwa ni za Zanzibar. Hapo vita nyingine itaanza rasmi.

Ni vyema nyie wanaccm muambiane ukweli, kuwa zama za ccm zimefikia mwisho. Kutunza siri ambazo zinafahamika na wanaccm tu, hilo haliwezekani tena kwa sasa. Mtaliacha taifa hili kwenye matatizo makubwa kwa miungano ya kilaghai. Kila kitu kiwekwe mezani, na kila mtu achukue 50 zake. Hao ACT wameshakubali siasa za kikondoo kwa ccm, wataingia kwenye hiyo SUK au wataacha hilo ni juu yao, maadamu wamekubali kushiriki uchaguzi ww kishenzi, ni aidha wakubali kumalizia ng'ombe mzima, ama waendelee kususa, lakini kisiasa chama chao kimeshakuwa kama TLP.
 
Zanzibar ni nchi ya mapinduzi, mpaka sasa, siasa za Zanzibar bado zinatawaliwa na mwangwi wa yale Mapinduzi,hivyo kuna aliyepindua, CCM anayetamalaki kwa shangwe, nderemo, vifijo na shamra shamra zote kusherehehekea miaka 62 ya Mapinduzi, lakini pia yupo aliyepinduliwa, ACT, huyu amenyamaza kimya akiumia chini kwa chini na ndani kwa ndani kila akikumbuka kilichotokea kwenye uchaguzi na yatokanayo na mapinduzi hayo, na hata baada ya uchaguzi mkuu, bado wamesusa kujiunga na GNU.
Nikupongeze kwa kutumia haki yako ya kutoa maoni. Pili, nikukumbushe tu kwamba wewe ni mwandishi wa habari. Taaluma inakutaka kuandika ukweli na utafanya hivyo iwapo tu utatafuta ukweli ( you would verify) kwa unachoandika.

Niseme tu kwa bahati mbaya hukufanya hivyo na matokeo yake umeandika habari ambayo ina ukweli ukachanganya na uongo. Hivi ACT alipinduliwa? Hivi kabla ya mfumo huu wa vyama vingi kulikuwa na ACT? Hili la ACT kunyamaza kwa kupinduliwa kwenye uchadmguzi uliopita ni sawa lakini kuiuhusisha na mapinduzi yaliyopita si sawa na ni uongo na uchonganishi mkubwa. Wewe kama mwandishi jukumu lako ni kuhabarisha na tu/wa naosoma wa/tu tafanya maamuzi yetu. Umejisahau na unaitia aibu tasnia ya habari. Unapaswa kujipambanua na wanaoandika humu JF kwa mihemko wakiwa sio WAANDISHI WA HABARI.
Natoa wito kwa Uongozi wa ACT Wazalendo, hakuna chochote msichokijua kuhusu siasa za Zanzibar, wekeni silaha chini, teuweni wawakilishi wenu kwenye GNU, pelekeni majina, rejeeni kwenye SUK, uchaguzi mwingine ni 2030.
Huu wito kwa kuwa ni wito hakuna tatizo. Naunga mkono ACT kutokujiunga na SUK kwa hali iliyotokea. Kumbuka huko upande wa pili hata uchaguzi kuna ch/vy ama hakiku/haviku shiriki na mwisho wa siku wakaandamana, seuze huku ambako wananchi walipiga kura kwa amani halafu wakafanyiwa uhuni.

Naunga mkono ACT Wazalendo kisidhiriki SUK hadi kieleweke.
 
Mbona MADAI ya ACT chini ya Mwenyekiti OMO yapo very clear.. unayafahamu Wakili Msomi?..yametekelezwa?..kwa kiasi gani?..kama hayatekelezeki sababu ni nini?...
Mama Tanzania ni mkubwa kuliko yeyote Tanganyika na Zanzibar,ALINDWE
Paskali anasema ACT hakuna wasichofahamu kuhusu siasa za Zanzibar. Yaani huko Zanzibar ccm ndio lazima watangazwe washindi kwa vyoyote ili kulinda muungano. Kwa maneno marahisi huko uchaguzi ni zoezi la hadaa, lakini mshindi ameshapangwa. Inaonekana chama kingine kiingia madarakani lazima kitavunja muungano. Na sababu za huu muungano zinasema kuwa 10miles za ukanda wote wa Pwani ya bahari ya Hindi ni sehemu ya Zanzibar. Hivyo bila muungano inasemekana Wazanzibar wataidai sehemu yao huko Umoja wa Mataifa. Na hapo ndio Tanganyika itakuwa landlocked country!

Paskali yeye ni muumini wa hiki kitisho maana ni mtu wa zamani, hivyo ni muathirika wa siasa hizo za karne iliyopita. Hivyo huu ushauri wake unatokana na kilema cha muuangano alichokipata toka akiwa mtoto.
 
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya Jumapili ya leo
View attachment 3528415

Naomba kuanza kwa declaration of interest,mimi za Zitto ni marafiki wa intake moja UDSM,namfahamu kwa karibu na huwa tunataniana,hivyo namfahamu ni mtu pragmatist anafuata siasa za pragmatism,Thread 'Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"' Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"
View: https://youtu.be/RPpcwlnNJ0A?si=K5K-9oEDKsbVQUm4

Pili nimetumia neno la kuudhi,waache ujinga,wapeleke majina ya SUK, Ujinga hapa ni kufanya jambo lile lile katika mazingira yale yale na kutegemea matokeo tofauti!

ACT tangu Cuf, wamekuwa wakishiriki chaguzi za Zanzibar na matokeo ni yale yale, wanafanyiwa kitu kile kile, hivyo hata walipokubali kushiriki uchaguzi huu, walijua nini kitatokea, sasa wanasusa nini?

Kesho ni siku ya kumbukumbu ya miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ya January 12, Mwaka 1964, kwa vile Tanzania ni nchi ya muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, na iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kuungana kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ile April 26, Mwaka 1964. Kuna yatu wanasherehekea Mapinduzi Matukufu huku kuna yatu wamenuna, wamesusa kushiriki Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kwanza nijiunge na Watanzania wenzangu, kumpongeza Rais wa JMT, Rais Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dr, Husein Mwinyi, kwa Zanzibar kutimiza miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku waliopindua wakiyaenzi na kuyaita ni Mapinduzi Matukufu, huku waliopinduliwa wakisema Mapinduzi yale hayana utukufu wowote kwasababu yaliandamana na umwagaji wa damu, kila uchaguzi Zanzibar kuna shangwe waliopindua na kushinda uchaguzi, kuna kununa na kususa kwa waliopinduliwa ambao wameshindwa uchaguzi.
Bahati nzuri mimi nilikuwepo Zanzibar ule uchaguzi wa 1995 na ni mimi ndiye niliyetangaza yale matokeo halisi on DTV, Uchaguzi,wa 2015 nikawepo tena Zanzibar,

Kuna Watanzania wengi, hawaujui umuhimu wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hivyo wanaiona kama hii ni sikukuu ya Zanzibar, umuhimu pekee wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ndio kiini cha kuasisiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo Watanzania wapenda muungano na wazalendo wote wanchi hii, , tunapaswa kuwashukuru sana, Wazanzibari, haswa wale mashujaa wa mapinduzi, ni kupitia kwenye mapinduzi hayo, ndio kumepelekea Tanganyika na Zanzibar zikaungana kuunda Tanzania.

Asili ya Tanganyika na Zanzibar
Wakati wa uumbikaji wanchi, Zanzibar na Tanganyika lilikuwa ni eneo moja, likamegeka, ndipo visiwa vya Zanzibar, Pemba na visiwa vingine vyote vya bahari zote, huwa vinakuwa vinamegeka kutoka eneo la bara, hivyo, eneo lote la Zanzibar ni limemegeka kutoka katika eneo la Tanganyika miaka milioni nyingi huko nyuma wakati wa kuumbika, hivyo muunghano wetu adhimu ni jambo jema la kuirejesha Zanzibar kwenye asili yake kabla haijamegeka na kuwa visiwa.

Historia ya Zanzibar.
Historia ya Zanzibar ninayoiweka hapa ni ya kuanzia mwaka 1734 wakati ujio wa Sultan Seyyid Said, alipohamishia sultani yake kutoka Oman kuja Zanzibar, hakuna taarifa ya aliipataje Zanzibar, ila wenyeji wa Zanzibar kabla ya ujio wa Waarabu ni Wakwezi na Wahadimu na mkuu wao alikuwa ni Mwinyi Mkuu. Hakuna mikataba yoyote ya mauziano ya Kisiwa cha Zanzibar na Pemba kati ya Mwinyimkuu na Sultan Seyyid Said, kama mikataba ya Wajerumani kuimiliki Tanganyika, ile mikataba ya Karl Peters na Mtemi Magungo wa Msovero, au Hassan Bin Amiri kukinunua kisiwa cha Kilwa kwa gharama ya kitambaa cha kukikzunguka kisiwa chote cha Kilwa kutoka kwa wenyeji.

Kwenye ule mkutano wa Berlin wa mwaka 1884, Sultan wa Zanzibar alitambuliwa kama mmiliki halali wa Zanzibar, Pemba, na ukanda wa maili 10 ya pwani yote ya Bahari ya Hindi, hivyo Zanzibar kutoka kwa wenyewe kuwa mali ya Sultani wa Zanzibar, huku Tanganyika ikikabidhiwa kwa Wajerumani.

Baada ya Ujerumani kushindwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, WW1, mwaka 1918, Ujerumani ilinyanganywa makoloni yake yote, Tanganyika na Zanzibar zikakabidhiwa kwa Waingereza, ila Tanganyika ndio lilikuwa koloni la wakfu, trustee, na Zanzibar lilikuwa ulizi tuu, yaani protectorate ambapo Sultan ataendelea kulindwa.

Sisi Tanganyika tukapata uhuru wetu kwa Waingereza, Desemba 9, 1961, Zanzibar ikapata uhuru wake Desemba 10, 1963, kutoka kwa Waingereza, ila wakiendelea kuitambua Zanzibar ni mali ya Sultan of Zanzibar, wajibu wao ni kumlinda.

Baada ya Wazalendo wa Zanzibar kufanya mapinduzi matukufu, ambayo yalimpindua Sultani, alikimbilia Mombasa na kuomba msaada kwa Waingereza waje kumsaidia kuurejesha utawala wake visiwani Zanzibar na Waingereza wakamkubalia, wakatuma meli vita kuja kuikomboa Zanzibar.

Ndipo shujaa wa Mapinduzi, Abedi Amani Karume akaja Tanganyika kuomba msaada wa ulinzi kuyalinda Mapinduzi, ndipo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere akamshauri Karume dawa ni kuungana, kuziunganisha nchi kuwa nchi moja, Karume alikubali pale pale, “wewe rais, mimi makamo”, ndipo taratibu za muungano zikafuata, hivyo Mapinduzi ya Zanzibar, ni tukio muhimu lililopelekea muungano wetu adhimu na uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zanzibar ni nchi ya mapinduzi, mpaka sasa, siasa za Zanzibar bado zinatawaliwa na mwangwi wa yale Mapinduzi,hivyo kuna aliyepindua, CCM anayetamalaki kwa shangwe, nderemo, vifijo na shamra shamra zote kusherehehekea miaka 62 ya Mapinduzi, lakini pia yupo aliyepinduliwa, ACT, huyu amenyamaza kimya akiumia chini kwa chini na ndani kwa ndani kila akikumbuka kilichotokea kwenye uchaguzi na yatokanayo na mapinduzi hayo, na hata baada ya uchaguzi mkuu, bado wamesusa kujiunga na GNU.

Natoa wito kwa Uongozi wa ACT Wazalendo, hakuna chochote msichokijua kuhusu siasa za Zanzibar, wekeni silaha chini, teuweni wawakilishi wenu kwenye GNU, pelekeni majina, rejeeni kwenye SUK, uchaguzi mwingine ni 2030.

Natoa wito kwa Rais Samia, na rais Mwinyi, kufanyia application ya zile 4R za Rais Samia kuinusuru SUK. Japo SUK imeleta mshikamano, lakini bado kuna changamoto mbalimbali zikiwemo Changamoto za muungano ambazo zamani zilikuwa zikiitwa kero za muungano, kule Pemba wanaziita makero

Hongera Zanzibar kwa Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mungu Ibariki Zanzibar

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali

Tangu nifahamu wewe ni vyeo oriented nikakuignore.
 
Na sababu za huu muungano zinasema kuwa 10miles za ukanda wote wa Pwani ya bahari ya Hindi ni sehemu ya Zanzibar. Hivyo bila muungano inasemekana Wazanzibar wataidai sehemu yao huko Umoja wa Mataifa. Na hapo ndio Tanganyika itakuwa landlocked country!
Hayo umeandika tu. Ikiwa ni hivyo unayodai wewe, Zanzibar siyo itadai maili 10 Tanganyika tu, bali pia itaidai Mombasa hadi Kismayu. Silioni hilo likitokea.
 
Pumba tupu
 
Wewe ni kibaka tu wa siasa!!ndio mliomshauri aingie kwenye uchaguzi wakati reform zilikuwa zinahitajika!sasa kadhulumiwa jimbo na halipat tena!

Maisha hayana janja janja, ukitaka janja hizo lazima uwe kibaka kama wewe na mwenzako madelu!
 
Back
Top Bottom