Zitto Mshauri OMO kuwa Pragmatist,Acheni Ujinga Pelekeni Majina ya SUK, Kususa Hakusaidii KITU

Zitto Mshauri OMO kuwa Pragmatist,Acheni Ujinga Pelekeni Majina ya SUK, Kususa Hakusaidii KITU

Wanabodi

Pili nimetumia neno la kuudhi,waache ujinga,wapeleke majina ya chama chao kuunda SUK kule Zanzibar!. Ujinga hapa ni kufanya jambo lile lile katika mazingira yale yale na kutegemea matokeo tofauti!
View: https://youtu.be/4AWaU_8FYhQ?si=TCb3xSJiXdcuuaZ8

ACT ya sasa kule Zanzibar, tangu wakiwa Cuf, wamekuwa wakishiriki chaguzi za Zanzibar na matokeo ni yale yale, wanafanyiwa kitu kile kile, hivyo hata walipokubali kushiriki wa uchaguzi huu, walijua nini kitatokea, sasa wanasusa nini?

Natoa wito kwa Uongozi wa ACT Wazalendo, hakuna chochote msichokijua kuhusu siasa za Zanzibar, wekeni silaha chini, teuweni wawakilishi wenu kwenye GNU, pelekeni majina, rejeeni kwenye SUK, uchaguzi mwingine ni 2030.

Mungu Ibariki Zanzibar

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali


YAH: UTEUZI WA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR

Tafadhali husikeni na mada iliyotajwa hapo juu.

Ofisi ya Baraza la Mapinduzi inapenda kutoa taarifa kwa Vyombo vya Habari na Umma kwa ujumla kuwa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemteua tena Mhe. Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Uteuzi huu umeanza rasmi tarehe 18 Septemba, 2026.

Hali kadhalika, Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais ataapishwa siku ya Jumanne, tarehe 22 Septemba, 2026, majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ikulu ya Zanzibar.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,

Pia soma: ACT Wazalendo yateua Jina la Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Huu ndio mwisho wa huu ujinga nilio uzungumzia hapa.
Asante ZZK for doing the needful kama nilivyo shauri hapa
P
 
Back
Top Bottom