Zitto Mshauri OMO kuwa Pragmatist,Acheni Ujinga Pelekeni Majina ya SUK, Kususa Hakusaidii KITU

Zitto Mshauri OMO kuwa Pragmatist,Acheni Ujinga Pelekeni Majina ya SUK, Kususa Hakusaidii KITU

Pasco, sio uungwana unawashauri watu halafu unasema aache "aache ujinga". Wewe toa mawazo yako tuu, kila mtu anatazama mambo kwa "angle" yake.
Mkuu Chivu, Chivundu , ni kweli hii sio lugha ya kiungwana, na nimeiombea msamaha kabla pale mwanzo kwenye angalizo

Lugha hii ya ujinga, hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliitumia sana, na hata kutufundisha kuntofautisha mjinga na mpumbavu

Hiki ACT wanachofanya kwa mujibu wa Nyerere ni ujinga!.

P
 
Acha tupate contents za maana sio udaku wenu mnaanzisha uzi una sentensi moja. Halafu jifunzeni kuheshimu wakongwe kama Pascal wametoka mbali na JF
 
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya Jumapili ya leo
View attachment 3528415

Naomba kuanza kwa declaration of interest,mimi za Zitto ni marafiki wa intake moja UDSM,namfahamu kwa karibu na huwa tunataniana,hivyo namfahamu ni mtu pragmatist anafuata siasa za pragmatism,Thread 'Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"' Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"
View: https://youtu.be/RPpcwlnNJ0A?si=K5K-9oEDKsbVQUm4

Pili nimetumia neno la kuudhi,waache ujinga,wapeleke majina ya SUK, Ujinga hapa ni kufanya jambo lile lile katika mazingira yale yale na kutegemea matokeo tofauti!

ACT tangu Cuf, wamekuwa wakishiriki chaguzi za Zanzibar na matokeo ni yale yale, wanafanyiwa kitu kile kile, hivyo hata walipokubali kushiriki uchaguzi huu, walijua nini kitatokea, sasa wanasusa nini?

Tangu ule uchaguzi wa 1995 ni mimi nikiwa DTV ndio nilitangaza matokeo ya kweli ya uchaguzi wa Zanzibar,na 2015 ikajirudia GE2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda hivyo hakuna kitu ambacho ACT Wazalendo,hawakukijua!

Kesho ni siku ya kumbukumbu ya miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ya January 12, Mwaka 1964, kwa vile Tanzania ni nchi ya muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, na iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kuungana kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ile April 26, Mwaka 1964. Kuna yatu wanasherehekea Mapinduzi Matukufu huku kuna yatu wamenuna, wamesusa kushiriki Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kwanza nijiunge na Watanzania wenzangu, kumpongeza Rais wa JMT, Rais Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Zanzibar, Dr, Husein Mwinyi, kwa Zanzibar kutimiza miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku waliopindua wakiyaenzi na kuyaita ni Mapinduzi Matukufu, huku waliopinduliwa wakisema Mapinduzi yale hayana utukufu wowote kwasababu yaliandamana na umwagaji wa damu, kila uchaguzi Zanzibar kuna shangwe waliopindua na kushinda uchaguzi, kuna kununa na kususa kwa waliopinduliwa ambao wameshindwa uchaguzi.
Bahati nzuri mimi nilikuwepo Zanzibar ule uchaguzi wa 1995 na ni mimi ndiye niliyetangaza yale matokeo halisi on DTV, Uchaguzi,wa 2015 nikawepo tena Zanzibar,

Kuna Watanzania wengi, hawaujui umuhimu wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hivyo wanaiona kama hii ni sikukuu ya Zanzibar, umuhimu pekee wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ndio kiini cha kuasisiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo Watanzania wapenda muungano na wazalendo wote wanchi hii, , tunapaswa kuwashukuru sana, Wazanzibari, haswa wale mashujaa wa mapinduzi, ni kupitia kwenye mapinduzi hayo, ndio kumepelekea Tanganyika na Zanzibar zikaungana kuunda Tanzania.

Asili ya Tanganyika na Zanzibar
Wakati wa uumbikaji wanchi, Zanzibar na Tanganyika lilikuwa ni eneo moja, likamegeka, ndipo visiwa vya Zanzibar, Pemba na visiwa vingine vyote vya bahari zote, huwa vinakuwa vinamegeka kutoka eneo la bara, hivyo, eneo lote la Zanzibar ni limemegeka kutoka katika eneo la Tanganyika miaka milioni nyingi huko nyuma wakati wa kuumbika, hivyo muunghano wetu adhimu ni jambo jema la kuirejesha Zanzibar kwenye asili yake kabla haijamegeka na kuwa visiwa.

Historia ya Zanzibar.
Historia ya Zanzibar ninayoiweka hapa ni ya kuanzia mwaka 1734 wakati ujio wa Sultan Seyyid Said, alipohamishia sultani yake kutoka Oman kuja Zanzibar, hakuna taarifa ya aliipataje Zanzibar, ila wenyeji wa Zanzibar kabla ya ujio wa Waarabu ni Wakwezi na Wahadimu na mkuu wao alikuwa ni Mwinyi Mkuu. Hakuna mikataba yoyote ya mauziano ya Kisiwa cha Zanzibar na Pemba kati ya Mwinyimkuu na Sultan Seyyid Said, kama mikataba ya Wajerumani kuimiliki Tanganyika, ile mikataba ya Karl Peters na Mtemi Magungo wa Msovero, au Hassan Bin Amiri kukinunua kisiwa cha Kilwa kwa gharama ya kitambaa cha kukikzunguka kisiwa chote cha Kilwa kutoka kwa wenyeji.

Kwenye ule mkutano wa Berlin wa mwaka 1884, Sultan wa Zanzibar alitambuliwa kama mmiliki halali wa Zanzibar, Pemba, na ukanda wa maili 10 ya pwani yote ya Bahari ya Hindi, hivyo Zanzibar kutoka kwa wenyewe kuwa mali ya Sultani wa Zanzibar, huku Tanganyika ikikabidhiwa kwa Wajerumani.

Baada ya Ujerumani kushindwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, WW1, mwaka 1918, Ujerumani ilinyanganywa makoloni yake yote, Tanganyika na Zanzibar zikakabidhiwa kwa Waingereza, ila Tanganyika ndio lilikuwa koloni la wakfu, trustee, na Zanzibar lilikuwa ulizi tuu, yaani protectorate ambapo Sultan ataendelea kulindwa.

Sisi Tanganyika tukapata uhuru wetu kwa Waingereza, Desemba 9, 1961, Zanzibar ikapata uhuru wake Desemba 10, 1963, kutoka kwa Waingereza, ila wakiendelea kuitambua Zanzibar ni mali ya Sultan of Zanzibar, wajibu wao ni kumlinda.

Baada ya Wazalendo wa Zanzibar kufanya mapinduzi matukufu, ambayo yalimpindua Sultani, alikimbilia Mombasa na kuomba msaada kwa Waingereza waje kumsaidia kuurejesha utawala wake visiwani Zanzibar na Waingereza wakamkubalia, wakatuma meli vita kuja kuikomboa Zanzibar.

Ndipo shujaa wa Mapinduzi, Abedi Amani Karume akaja Tanganyika kuomba msaada wa ulinzi kuyalinda Mapinduzi, ndipo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere akamshauri Karume dawa ni kuungana, kuziunganisha nchi kuwa nchi moja, Karume alikubali pale pale, “wewe rais, mimi makamo”, ndipo taratibu za muungano zikafuata, hivyo Mapinduzi ya Zanzibar, ni tukio muhimu lililopelekea muungano wetu adhimu na uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zanzibar ni nchi ya mapinduzi, mpaka sasa, siasa za Zanzibar bado zinatawaliwa na mwangwi wa yale Mapinduzi,hivyo kuna aliyepindua, CCM anayetamalaki kwa shangwe, nderemo, vifijo na shamra shamra zote kusherehehekea miaka 62 ya Mapinduzi, lakini pia yupo aliyepinduliwa, ACT, huyu amenyamaza kimya akiumia chini kwa chini na ndani kwa ndani kila akikumbuka kilichotokea kwenye uchaguzi na yatokanayo na mapinduzi hayo, na hata baada ya uchaguzi mkuu, bado wamesusa kujiunga na GNU.

Natoa wito kwa Uongozi wa ACT Wazalendo, hakuna chochote msichokijua kuhusu siasa za Zanzibar, wekeni silaha chini, teuweni wawakilishi wenu kwenye GNU, pelekeni majina, rejeeni kwenye SUK, uchaguzi mwingine ni 2030.

Natoa wito kwa Rais Samia, na rais Mwinyi, kufanyia application ya zile 4R za Rais Samia kuinusuru SUK. Japo SUK imeleta mshikamano, lakini bado kuna changamoto mbalimbali zikiwemo Changamoto za muungano ambazo zamani zilikuwa zikiitwa kero za muungano, kule Pemba wanaziita makero

Hongera Zanzibar kwa Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mungu Ibariki Zanzibar

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali

Unatumika wewe
 
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya Jumapili ya leo
View attachment 3528415

Naomba kuanza kwa declaration of interest,mimi na Zitto ni marafiki wa intake moja UDSM,namfahamu kwa karibu na huwa tunataniana,hivyo namfahamu ni mtu pragmatist anayefuata siasa za pragmatism Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"
View: https://youtu.be/RPpcwlnNJ0A?si=K5K-9oEDKsbVQUm4

Pili nimetumia neno la kuudhi,waache ujinga,wapeleke majina ya chama chao kuunda SUK kule Zanzibar!. Ujinga hapa ni kufanya jambo lile lile katika mazingira yale yale na kutegemea matokeo tofauti!
View: https://youtu.be/4AWaU_8FYhQ?si=TCb3xSJiXdcuuaZ8

ACT ya sasa kule Zanzibar, tangu wakiwa Cuf, wamekuwa wakishiriki chaguzi za Zanzibar na matokeo ni yale yale, wanafanyiwa kitu kile kile, hivyo hata walipokubali kushiriki wa uchaguzi huu, walijua nini kitatokea, sasa wanasusa nini?

Tangu ule uchaguzi wa 1995 ni mimi nikiwa DTV ndio nilitangaza matokeo ya kweli ya uchaguzi wa Zanzibar,na 2015 ikajirudia GE2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda hivyo hakuna kitu ambacho ACT Wazalendo,hawakukijua!

Mungu Ibariki Zanzibar

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali

Wanabodi,
nimelikumbuka bandiko hili leo, baada ya kuisoma headiline ya lead story ya gazeti la Nipashe la leo
SUK NJIA PANDA.jpg

Mpaka sasa tunaelekea mwezi June, hawa jamaa, bado wamekomaa hawataki kupeleka majina yao ya kujumlishwa kwenye SUK, hivyo bandiko hili bado ni very valid, namshauri ZZK amshauri OMO waache huu ujinga!, kama SMZ bila SUK inadunda miezi 8, ikifika mwaka bila SUK, then SMZ itaendelea miaka 5 yote bila SUK, na uchaguzi wa 2030, ZEC watajifunza kwa INEC, matokeo yatakuwa CCM Bara ushindi ni kishindo cha asilimia 99%, CCM Zanzibar asilimia 99%!.

Ukipata kidogo, uwe na shukrani kwa hicho kidogo, ili ujaaliwe kikubwa, kumbuka ni kanuni ya Mwenyeezi Mungu kwa mwenyenacho, ataongezewa, na asienacho, atanyan'gnywa hata kile kidogo alichonacho.

Kwa Zanzibar, CCM ndie mwenye nacho, mwenye kingi, na ACT ni mwenye kidogo, ACT wakiendelea kususia kupeleka majina SUK, SMZ Zanzibar, itaendelea bila ACT, wakiendelea bila ACT, uchaguzi wa 2030, Wazanzibari, watakifanya kile Watanzania walichofanya uchaguzi wa 2025, waliwakataa wapinzani na vyao vyao shikizi 16, wakaichagua CCM kwa kishindo cha ushindi wa asilimia 98%.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Zanzibar!.

Paskali
 
SUK ni utapeli uliofanywa na CCM kuendelea kutawala kwa ulaghai. Kukubali kushiriki kwenye utapeli huo ndio ujinga.

CCM iendelee kunajisi chaguzi na wapinzani wapewe makamo wa kwanza wa raisi ceremonial. Ni uzuzu.
 
Wanabodi,
nimelikumbuka bandiko hili leo, baada ya kuisoma headiline ya lead story ya gazeti la Nipashe la leo
View attachment 3586449
Mpaka sasa tunaelekea mwezi June, hawa jamaa, bado wamekomaa hawataki kupeleka majina yao ya kujumlishwa kwenye SUK, hivyo bandiko hili bado ni very valid, namshauri ZZK amshauri OMO waache huu ujinga!, kama SMZ bila SUK inadunda miezi 8, ikifika mwaka bila SUK, then SMZ itaendelea miaka 5 yote bila SUK, na uchaguzi wa 2030, ZEC watajifunza kwa INEC, matokeo yatakuwa CCM Bara ushindi ni kishindo cha asilimia 99%, CCM Zanzibar asilimia 99%!.

Ukipata kidogo, uwe na shukrani kwa hicho kidogo, ili ujaaliwe kikubwa, kumbuka ni kanuni ya Mwenyeezi Mungu kwa mwenyenacho, ataongezewa, na asienacho, atanyan'gnywa hata kile kidogo alichonacho.

Kwa Zanzibar, CCM ndie mwenye nacho, mwenye kingi, na ACT ni mwenye kidogo, ACT wakiendelea kususia kupeleka majina SUK, SMZ Zanzibar, itaendelea bila ACT, wakiendelea bila ACT, uchaguzi wa 2030, Wazanzibari, watakifanya kile Watanzania walichofanya uchaguzi wa 2025, waliwakataa wapinzani na vyao vyao shikizi 16, wakaichagua CCM kwa kishindo cha ushindi wa asilimia 98%.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Zanzibar!.

Paskali

Yaani unashabikia wizi? Hivi wewe una dini gani i yokubaliana na wizi?
 
Yaani unashabikia wizi? Hivi wewe una dini gani i yokubaliana na wizi?
Kuna vitu vingi Watanzania wengi wewe ukiwemo huvijui!. Hii katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni katiba ya CCM, hivyo kwa katiba hii, hii ni nchi ya CCM!, hivyo kila kitu ni cha CCM, ikiwemo watu, kura na kila kilichomo!, kwa muktadha huu, huwezi kuiba kitu ambacho ni mali yako, ni unachukua tuu. Hivyo inachofanya CCM, ni kuchukua tuu kilicho chake!. Angalia tarehe ya bandiko hili GE2020 - Mwana JF, be the first to know kuwa CCM ndio mshindi wa jumla wa Uchaguzi huu

P.
 
Kama ni hivyo Huo uchaguzi ni wa kazi gani ? Kuibiana.? Pascal unazeeka vibaya jiangalie vizuri
 
Kuna vitu vingi Watanzania wengi wewe ukiwemo huvijui!. Hii katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni katiba ya CCM, hivyo kwa katiba hii, hii ni nchi ya CCM!, hivyo kila kitu ni cha CCM, ikiwemo watu, kura na kila kilichomo!, kwa muktadha huu, huwezi kuiba kitu ambacho ni mali yako, ni unachukua tuu. Hivyo inachofanya CCM, ni kuchukua tuu kilicho chake!. Angalia tarehe ya bandiko hili GE2020 - Mwana JF, be the first to know kuwa CCM ndio mshindi wa jumla wa Uchaguzi huu

P.

Pascal namna CCM wanavyoiendesha nchi wanaipeleka kwenye maangamizi makubwa . Damu wameshaimwaga sana tu , iliyobaki kwa mwendo wao huyu ni kuangamiza nchi kwenye machafuko makubwa sana. Mungu atuepushe nayo lakini kiza ni kikubwa sana.
 
Usiwe na wasiwasi, tunakwenda kwenye katiba mpya, kilakitu kitakuwa sawa!.
P
 
Hayo wanayojifanya wanayaigiza ni petroli na kuni ya hilo giza linalokuja. Nchi inaelekezwa kubaya sana .
Hatutafika huko, katiba mpya inakuja, tutarekebisha mambo yote na yatakaa sawa.
P
 
Wanabodi
Hii ni makala yangu kwenye Nipashe ya Jumapili ya leo
View attachment 3528415

Naomba kuanza kwa declaration of interest,mimi na Zitto ni marafiki wa intake moja UDSM,namfahamu kwa karibu na huwa tunataniana,hivyo namfahamu ni mtu pragmatist anayefuata siasa za pragmatism Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"
View: https://youtu.be/RPpcwlnNJ0A?si=K5K-9oEDKsbVQUm4

Pili nimetumia neno la kuudhi,waache ujinga,wapeleke majina ya chama chao kuunda SUK kule Zanzibar!. Ujinga hapa ni kufanya jambo lile lile katika mazingira yale yale na kutegemea matokeo tofauti!
View: https://youtu.be/4AWaU_8FYhQ?si=TCb3xSJiXdcuuaZ8

ACT ya sasa kule Zanzibar, tangu wakiwa Cuf, wamekuwa wakishiriki chaguzi za Zanzibar na matokeo ni yale yale, wanafanyiwa kitu kile kile, hivyo hata walipokubali kushiriki wa uchaguzi huu, walijua nini kitatokea, sasa wanasusa nini?

Tangu ule uchaguzi wa 1995 ni mimi nikiwa DTV ndio nilitangaza matokeo ya kweli ya uchaguzi wa Zanzibar,na 2015 ikajirudia GE2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda hivyo hakuna kitu ambacho ACT Wazalendo,hawakukijua!

Natoa wito kwa Uongozi wa ACT Wazalendo, hakuna chochote msichokijua kuhusu siasa za Zanzibar, wekeni silaha chini, teuweni wawakilishi wenu kwenye GNU, pelekeni majina, rejeeni kwenye SUK, uchaguzi mwingine ni 2030.

Na ikitokea kama OMO yeye ametosheka na ving'ora, sio lazima awe yeye, wampe hata Jussa, Dimani au hata Ally Saleh Albeto.

Natoa wito kwa Rais Samia, na rais Mwinyi, kufanyia application ya zile 4R za Rais Samia kuinusuru SUK. Japo SUK imeleta mshikamano, lakini bado kuna changamoto mbalimbali zikiwemo Changamoto za muungano ambazo zamani zilikuwa zikiitwa kero za muungano, kule Pemba wanaziita makero

Hongera Zanzibar kwa Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mungu Ibariki Zanzibar

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali

Wito huu leo ndio umetekelezwa!, hongera Zitto kumshauri OMO kuacha ujinga, hongera OMO kukubali matokeo, hongera Rais Samia na rais Mwinyi kuukubali ushauri wa bandiko hili, hongera vyama vya CCM na ACT, hongera Wazanzibari, Wazanzibara na Watanzania.

Big up sana for this step

P
 
Back
Top Bottom