Zitto Mshauri OMO kuwa Pragmatist,Acheni Ujinga Pelekeni Majina ya SUK, Kususa Hakusaidii KITU

Pasco, sio uungwana unawashauri watu halafu unasema aache "aache ujinga". Wewe toa mawazo yako tuu, kila mtu anatazama mambo kwa "angle" yake.
Mkuu Chivu, Chivundu , ni kweli hii sio lugha ya kiungwana, na nimeiombea msamaha kabla pale mwanzo kwenye angalizo

Lugha hii ya ujinga, hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliitumia sana, na hata kutufundisha kuntofautisha mjinga na mpumbavu

Hiki ACT wanachofanya kwa mujibu wa Nyerere ni ujinga!.

P
 
Acha tupate contents za maana sio udaku wenu mnaanzisha uzi una sentensi moja. Halafu jifunzeni kuheshimu wakongwe kama Pascal wametoka mbali na JF
 
Unatumika wewe
 
Wanabodi,
nimelikumbuka bandiko hili leo, baada ya kuisoma headiline ya lead story ya gazeti la Nipashe la leo

Mpaka sasa tunaelekea mwezi June, hawa jamaa, bado wamekomaa hawataki kupeleka majina yao ya kujumlishwa kwenye SUK, hivyo bandiko hili bado ni very valid, namshauri ZZK amshauri OMO waache huu ujinga!, kama SMZ bila SUK inadunda miezi 8, ikifika mwaka bila SUK, then SMZ itaendelea miaka 5 yote bila SUK, na uchaguzi wa 2030, ZEC watajifunza kwa INEC, matokeo yatakuwa CCM Bara ushindi ni kishindo cha asilimia 99%, CCM Zanzibar asilimia 99%!.

Ukipata kidogo, uwe na shukrani kwa hicho kidogo, ili ujaaliwe kikubwa, kumbuka ni kanuni ya Mwenyeezi Mungu kwa mwenyenacho, ataongezewa, na asienacho, atanyan'gnywa hata kile kidogo alichonacho.

Kwa Zanzibar, CCM ndie mwenye nacho, mwenye kingi, na ACT ni mwenye kidogo, ACT wakiendelea kususia kupeleka majina SUK, SMZ Zanzibar, itaendelea bila ACT, wakiendelea bila ACT, uchaguzi wa 2030, Wazanzibari, watakifanya kile Watanzania walichofanya uchaguzi wa 2025, waliwakataa wapinzani na vyao vyao shikizi 16, wakaichagua CCM kwa kishindo cha ushindi wa asilimia 98%.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Zanzibar!.

Paskali
 
SUK ni utapeli uliofanywa na CCM kuendelea kutawala kwa ulaghai. Kukubali kushiriki kwenye utapeli huo ndio ujinga.

CCM iendelee kunajisi chaguzi na wapinzani wapewe makamo wa kwanza wa raisi ceremonial. Ni uzuzu.
 

Yaani unashabikia wizi? Hivi wewe una dini gani i yokubaliana na wizi?
 
Yaani unashabikia wizi? Hivi wewe una dini gani i yokubaliana na wizi?
Kuna vitu vingi Watanzania wengi wewe ukiwemo huvijui!. Hii katiba ya JMT ya mwaka 1977, ni katiba ya CCM, hivyo kwa katiba hii, hii ni nchi ya CCM!, hivyo kila kitu ni cha CCM, ikiwemo watu, kura na kila kilichomo!, kwa muktadha huu, huwezi kuiba kitu ambacho ni mali yako, ni unachukua tuu. Hivyo inachofanya CCM, ni kuchukua tuu kilicho chake!. Angalia tarehe ya bandiko hili GE2020 - Mwana JF, be the first to know kuwa CCM ndio mshindi wa jumla wa Uchaguzi huu

P.
 
Kama ni hivyo Huo uchaguzi ni wa kazi gani ? Kuibiana.? Pascal unazeeka vibaya jiangalie vizuri
 

Pascal namna CCM wanavyoiendesha nchi wanaipeleka kwenye maangamizi makubwa . Damu wameshaimwaga sana tu , iliyobaki kwa mwendo wao huyu ni kuangamiza nchi kwenye machafuko makubwa sana. Mungu atuepushe nayo lakini kiza ni kikubwa sana.
 
Pascal namna CCM wanavyoiendesha nchi wanaipeleka kwenye maangamizi makubwa . Damu wameshaimwaga sana tu , iliyobaki kwa mwendo wao huyu ni kuangamiza nchi kwenye machafuko makubwa sana. Mungu atuepushe nayo lakini kiza ni kikubwa sana.
Usiwe na wasiwasi, tunakwenda kwenye katiba mpya, kilakitu kitakuwa sawa!.
P
 
Hayo wanayojifanya wanayaigiza ni petroli na kuni ya hilo giza linalokuja. Nchi inaelekezwa kubaya sana .
Hatutafika huko, katiba mpya inakuja, tutarekebisha mambo yote na yatakaa sawa.
P
 
Wito huu leo ndio umetekelezwa!, hongera Zitto kumshauri OMO kuacha ujinga, hongera OMO kukubali matokeo, hongera Rais Samia na rais Mwinyi kuukubali ushauri wa bandiko hili, hongera vyama vya CCM na ACT, hongera Wazanzibari, Wazanzibara na Watanzania.

Big up sana for this step

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…