Zitto: Mtu sahihi wa kumjibu Prof. Kabudi ni Lissu

Zitto: Mtu sahihi wa kumjibu Prof. Kabudi ni Lissu

Kama ni kura tumempa za kutosha, hilo hatuna shaka nalo. Ila hatukuwa na kura za kwenye mabeg kama ccm, wala hatuna makundi yenye silaha kama ccm ili kupata kura za wizi. Maandamano bado watu ni waoga, ila huko tutafika tu.
Bila shaka wewe usie muoga uliandamana! Ahahahahahaha na bado unaandamana. Si maandamano hayana kikomo? Ahahahahahahahahahah!!!!
 
Binafsi niliwahi sema kupitia hapa JF kuwa, Lissu ni muumini mzuri wa historia, na kwamba wakati wengi tumesoma historia kama hadithi tu, Lissu anaitumia historia kama kioo cha maisha yake, na hii ni moja ya sababu ya Lissu kuonekana ni mtu mwenye kuona mbali kwani katika dunia ya leo, hakuna jipya zaidi ya teknolojia tu.
Tatizo lenu wana Ufipa mnamchukulia Lissu kama Nabii fulani hivi, kila kitu anakijua yeye. Sheria anaijua yeye, masuala ya utawala anayajua yeye, masuala ya kimataifa anayajua yeye, Diplomasia anaijua yeye na sasa amekua mwanahistoria. Kuna siku mtasema Lissu pia ni Daktari ndo maana ameweza kupona zile risasi 16. Yaani wale madaktari wa ubelgiji walikua wanamtibia kwa maelekezo yake yeye.
 
Hapa cha Mhimu ni Kurudisha Pesa ya Watu. Maana Sept, 2020 tayari nchi ilikuwa CORONA free sasa zilitumika wapi hizo hera uau ndo ile Uchaguzi TUMETUMIA FEDHA YETU kumbe ya WAZUNGU. Jibuni na rudisheni Pesa za Watu ili waendelee Kutuletea ARV na Vyandarua.
 
Huyu nae aje atwambie aliko jasusi mbobezi wa kikanda na kimataifa
 
Binafsi niliwahi sema kupitia hapa JF kuwa, Lissu ni muumini mzuri wa historia, na kwamba wakati wengi tumesoma historia kama hadithi tu, Lissu anaitumia historia kama kioo cha maisha yake, na hii ni moja ya sababu ya Lissu kuonekana ni mtu mwenye kuona mbali kwani katika dunia ya leo, hakuna jipya zaidi ya teknolojia tu.
Wakati wa kampeni Lissu alipita kwenye eneo moja la pembezoni la nchi yetu. Hakuwa na mkutano hapo lakini alisimama kusalimiana na wananchi waliokuwa wakimsubiri barabarani. Eneo hilo linayo historia kubwa ya mgogoro mkubwa kati ya wenyeji na serikali tangu wakati wa ukoloni mpaka sasa. Katika mazungumzo yake na hao wamanchi wachache aliosalamiana nao, tofauti na watu wemgine wengi hapa nchini wakiwepo wanasiasa, Lissu alionyesha kuifahamu vizuri sana hiyo historia na jinsi ambavyo viongozi wa kisiasa wa eneo hilo wameshindwa kuwawakilisha wananchi wenzao ipasavyo. Lissu ni mfano mzuri wa mtu aliyesoma na kuelimika. Tatizo moja kubwa la nchi yetu ni kuwa na watu wengi katika nafasi za uongozi ambao wanadhaniwa wamesoma lakini kumbe hawajaelimika.
 
Back
Top Bottom