Zanzibar 2020 Zitto na Maalim Seif, Mkijiunga na Serikali ya Kitaifa huko Zanzibar nyinyi ni wasaliti!

Zanzibar 2020 Zitto na Maalim Seif, Mkijiunga na Serikali ya Kitaifa huko Zanzibar nyinyi ni wasaliti!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kwako ndugu Zitto
Kwako ndugu Maalim

Wazanzibari wameona!
Afrika imeona!
Dunia Imeona!

Dhulma ya kutisha waliyofanyiwa Wazanzibari, torture, mauaji, uporaji wa dhahiri haki ya wazanzibari kuchagua viongozi wao.

Halafu leo hii kwa sababu ya vyeovyeo na maslahi yatokanayo na vyeo hivyo nasikia mnafikiria kujiunga kwenye meza ya waliofanya udhalimu?

Ndugu Zitto, Dunia ikisikia itawaona nyie ni Wasaliti!. Heshima ya Maalimu itaporomoka kama barafu kiangazi.

Kujiunga kwenye meza ya udhalimu maana yake mmekubaliana na udhalimu huo, na mibarua yote mliyoandika kwenye mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu haina maana yoyote. Na kibaya zaidi mtawapa ujasiri watawala dhalimu kufanya udhalimu wao tena na tena kwa staili ileile kwa sababu wanajua at the end of the day watawapoza kwa fedha na vijimadaraka madaraka!

I know it, I know at one point or another watataka kumitigate athari za udhalimu wao kupitia fedha!. Wanajua individually mna hali ngumu ya kifedha, watakuja kwa kuweka mpunga mezani mkae atleast mkae kimya. Sasa Fedha si kila kitu, Judas Escariot alikuja kulijua hili wakati keshamsaliti Yesu!

Zitto, ACT Mkijiunga na Serikali ya Zanzibar ile tag ya usaliti uliyowekwa haitofutika kamwe, na wananchi hawatokupa heshima ambayo kwa kweli kutokana na kazi yako nzuri katika siasa unaideserve!

Maalim Ukijiunga na hiyo serikali, Heshima yako ya miaka zaidi ya 35 ya kuipigania Zanzibar itafutika, na utaonekana kuwa zile dhana za kuwa wewe ni mtu wa CCM ni kweli na Ukifanya hivyo zile ndoto za kuikomboa Zanzibar zitapotea. Ni heri ustaafu, uwaachie vijana waendeleze harakati kuliko kula haramu

Najua, Masheikh, Wastasfu wazito, Watu wakubwa kedekede wanakuja kwenu, au kukupigiani simu ili mlainike, hao ni wanafiki, walikuwa wapi wakati kuna uharamia wa waziwazi.

Pia najua kuna wanasiasa pengine wako blackmailed kuwa ni lazima wawe onboard, Nakuelezeni ni heri ACT ife kuliko kukubali kuendorse dhulma, Mkikubaliana na dhulma kwa sababu ya vijipesapesa hivi na hofu ya mtaishije basi ni heri Tubaki na chama kimoja nchini au tutawaliwe kifalme, otherwise Msigeuke Wasaliti!

Mkiingia kwenye serikali hiyo ni kwa ajili ya matumbo yenu tu na si kwa ajili ya watu wa Zanzibar.
 
Kwani lengo lao hasa lilikuwa lipi? Watakuwaje wasaliti katika kipindi ambacho wamepewa fursa ya kuwa sehemu ya Serikali?

Au mlipanga kuwahujumu wazanzibari? Tuache ujuha, tuijenge Tanzania iwe nchi yenye uchumi Imara Kama nchi za Asia ambazo zimechukua hatua na kuingia kwenye uchumi mkubwa kuliko kuhangaika na siasa zenye kudhoofisha uchumi wetu!
 
Maalim alisema safari hii hawataki Ukhanithi
Sasa akiingia humo atakuwa ameukubali Ukhanithi rasmi, hatoheshimika kamwe!
Lakini hatma ya siasa za kule Zanzibar ni ipi hasa ukiangalia mwenendo wa yanayotokea ???
Maana kila Uchaguzi ni lazima ugubikwe na vifo na vitisho vya majeshi kutoka Tanganyika.
Wataendelea kuishi chini ya hili kongwa la unyonyaji na unyanyasaji mpaka lini ???
 
Img-1605046541634.jpg
 
Lakini hatma ya siasa za kule Zanzibar ni ipi hasa ukiangalia mwenendo wa yanayotokea ???
Maana kila uchaguzi ni lazima ugubikwe na vifo na vitisho vya majeshi kutoka Tanganyika.
Wataendelea kuishi chini ya hili kongwa la unyonyaji na unyanyasaji mpaka lini ???

Wazanzibar bila kuchoka wamobilize international community isikie kilio chao.

Waendelee na harakati za kudai haki zao ndani ya nchi kwa kupinga kwa kauli na vitendo vyovyote kuresist dhulma na ukandamizaji wanaofanyiwa. Siyo rahisi, it may take years but they will reach a point sauti ya mwananchi wa Zanzibar siku moja itaheshimika huko.
Udhalimu hustawi pale unapokubaliana nao!
 
Kwani lengo lao hasa lilikuwa lipi? Watakuwaje wasaliti katika kipindi ambacho wamepewa fursa ya kuwa sehemu ya Serikali?

Au mlipanga kuwahujumu wazanzibari? Tuache ujuha, tuijenge Tanzania iwe nchi yenye uchumi Imara Kama nchi za Asia ambazo zimechukua hatua na kuingia kwenye uchumi mkubwa kuliko kuhangaika na siasa zenye kudhoofisha uchumi wetu!
Uhai wa watu hauna maana kwenu kuliko hicho kitu 'so called' uchumi?

Nani kawapa mamlaka ya kuwauwa wenzenu kisa matumbo yenu?

Ina maana mlishaongea na Mungu kuwa msipokuwa watawala basi hatowapa tena riziki zenu?

Kumbukeni kuwa kuna maisha baada ya kufa. Nyie teseni, umizeni na ueni pia ila mwisho wa siku mtakuja kulipwa kwa mnayoyafanya bila shaka.

Hizi ni nasaha zangu kwenu, mkitaka mtazifanyia kazi laa hamtaki basi tukutane kwa Mungu.
 
Ukisoma hii makala ya gazeti la Mwananchi, inaonyesha dhahiri Maalim hana msimamo thabiti wa kutoutambua Uchaguzi wa dhulma huko Zanzibar.

Hebu msome hapa kwenye hii makala ya gazeti la mwananchi!

 
kwenye Uchaguzi uliopita tuliona maiti nyingi za vijana wa Zanzibar waliouwawa kikatili kabisaa tena kwa kudhulumiwa haki zao za kikatiba na za msingi zikitapakaa mitaani, sasa basi ikitokea Maaalim Seif akakubali uteuzi wa aina yoyote kwenye hiyo kundi la wadhalimu kama alivyo wahi fanya huko nyuma umma wa Watanzania hatutamwelewa kwa namna yoyote ile, nasikia wameisha mtengea ndoano (umakamu wa Rais ….)

Maalim seif na chama chake wakijichanganya kukaa mezani na wauaji na wazurumati safari hii tutarudi mabara barani kushugulika naye, tunasikia kuna offer kapewa!
 
Mtazamo wako uko hivyo lakini fahamu kwamba kuna mateka kibao kina Mazrui naibu wa ACT wazalendo kahamishiwa Dar yasemekana watambambikizia kesi za ugaidi sasa kama picha zipo hivyo kwanini Maalim asikubali kuunda
Serikali ya shirikisho ili kuweka masharti hawa wanaoumizwa waachiwe huru na hao mafatani wa demokrasia
 
Sasa ndo mtajua kama Lipumba ndo msaliti au huyo babu yenu kipenzi na mshirika wenu.

Kama CUF ilikuwa CCM-B kwa kushiriki SUK, basi awamu hii ACT ikifanya hivyo itabidi iitwe CCM-B na mshirika wao CHADEMA itakuwa CCM-C.
 
Mtazamo wako uko hivyo lakini fahamu kwamba kuna mateka kibao kina mazrui naibu wa ACT wazalendo kahamishiwa dar yasemekana watambambikizia kesi za ugaidi sasa kama picha zipo hivyo kwanini maalim asikubali kuunda
Serikali ya shirikisho ili kuweka masharti hawa wanaoumizwa waachiwe huru na hao mafatani wa demokrasia
Yaani Akina Mazrui ndo wafanywe bargaining chip ya ACT kukubali udhalimu halafu na wao ACT wakubali? - Hoja yako ni sawa na kudema askari akikamatwa na adui basi kikosi chake nacho kisarende kwa adui ili asiuliwe!.

Kama kufa wameshakufa makumi ya Wazanzibari wasio na hatia, kwa hiyo maisha ya Mazrui hayana thamani kushinda wote hao waliokufa!.

Mi heri Mazrui afe Shahidi kuliko kusaliti wananchi wa Zanzibar
 
Back
Top Bottom