Zanzibar 2020 Zitto na Maalim Seif, Mkijiunga na Serikali ya Kitaifa huko Zanzibar nyinyi ni wasaliti!

Kila mtu ana Uhuru na Haki ya kujiunga na chama anachotaka ni haki ya kikatiba.
Tatizo kukipeleka chama kizima huko CCM hilo ndio halikubaliki kama wanaenda waende wao kama wao.
Mbona mashujaa wanazaliwa kila siku.
Huwezi kumzuia mtu asijiunge na chama anachotaka
 
Tukisema vijana kuweni makini msitumike kama Condom muwe mnaelewa

Hakuna Mwanasiasa wa kujitoa kwa ajili yako, huku Halima na Ester nao heka heka
 
Tukisema vijana kuweni makini msitumike kama Condom muwe mnaelewa

Hakuna Mwanasiasa wa kujitoa kwa ajili yako, huku Halima na Ester nao heka heka
Hakuna anayemuomba mwanasiasa ugali, tunataka wawe committed kupigania nchi. Kama wewe unawajua wanasiasa njaa kama majority ya walioko CCM hilo lisikufanye uamini kuwa lazima kila mwanasiasa lazima aweke mbeke tumbo lake kabla ya nchi!
 
ACT mkiunga mkono udhalimu basi zile dua na visomo mbalimbali walivyovifanya watu wa Zanzibar dhidi ya madhalimu na nyie vitawarudia.

Achaneni na hii kitu haina afya kwenu na kwa Zanzibar na pia itaipa ahueni serikali ya Jiwe inayopata mashambulizi kutoka kila kona ya dunia juu ya ubinywaji mkubwa wa haki za binadamu!
 
Hakuna hata Mwanasiasa mmoja asieweka mbele maslahi yake Tanzania
Hakuna anayemuomba mwanasiasa ugali, tunataka wawe committed kupigania nchi. Kama wewe unawajua wanasiasa njaa kama majority ya walioko CCM hilo lisikufanye uamini kuwa lazima kila mwanasiasa lazima aweke mbeke tumbo lake kabla ya nchi!
 
yaani nyie ndo majoka kuliko hata CCM heri kukabidhi nchi kwa CCM kuliko majambazi yanayotaka kutuuza kwa mabeberu
 
Maalim seif kashasema zamani mara hii hataki uhanithi wao, hizi wanazofanya CCM Zanzibar ni Propaganda wanataka kuchanganya watu tu.
 
Maoni yangu baada ya kutafakari sana.

ACT ipendekeze mashekhe watano wa uamsho ndio washike nafasi tano za juu za sherikali ya umoja Zanzibar
 
Wacha porojo, weka uthibitisho. Hivi kwa akili yako, umeona Zitto na Maalim Seif kuwa wanasiasa wazuri na wanaaminika, shauri yako.
 
Maalim Seif kweli unataka kujiunga na watesi wenu ili tu uenjoy ving'ora, saluti na kulala Serena hotel ukija Dar es Salaam?
 
Ujuha ni pale unapothamini kitu badala ya utu. Kisa uchumi "ukuwe" tu basi tumwage damu za watu? Au wewe ndio wale mnaotoa watoto zenu kafara ili mukuwe kiuchumi?
 
Mara ya mwisho nilisikia Babake (mwenyekiti wa kamati ya roho mbaya) "rais" alimwita Maalim na kumuomba ashirikiane na mwanawe akakataa. Labda za maskani izi
 
Kuliko kusaliti wazanzibari, Maalim Seif ni heri astaafu siasa kwa heshima, aandike kitabu cha harakati za kisiasa. Hilo lina maana zaidi kwa Zanzibar na Wazanzibari kuliko kushiriki karamu moja na watesi wa Wazanzibari.

Akiingia humo kwenye hiyo serikali iliyopatikana kwa kumwaga damu za wadio na hatia hiyo itakuwa ni kwa maslahi yake binafsi na genge lake na si kwa faida ya Wazanzibari
 
Tanzania = Tanganyika + Zanzibar
Zanzibar = Pemba + Unguja
Pemba = ?
Unguja = ?
 
Utajiungaje na serikali iliyosababisha kifo cha mjumbe wako wa kamati kuu, kumteka katibu wako mkuu wa Zanzibar wiki ya pili sasa, Kumtesa mgombea wako wa uwakilishi na kumvunja mwili sehemu Tisa za Mwili?
Viongozi watakaokubali hayo ni wasaliti wakubwa hawastahili heshima yoyote ya Mtanzania!

 

Yaani katika kitu tutawadharau hao viongozi ni kukubali kujiunga na hiyo Serikali. Watu wapigwe, kuuwawa na hata wizi mkubwa wa kura, kisha ushiriki kwenye huo ushetani kisa pesa?
 
Kusarenda pia ni njia ya moja ya kumshinda adui kama hakuna namna huwezi kujidai una msimamo wakati wafuasi wako wanaumizwa kinyma na sasa ni giza totoro hakuna mwanga wowote. watajipanga upya baadae utawala ukibadilika.
 
Hao mashehe kama kweli wanataka umoja kwanini hawaanzii kwa mashehe wenzao wanaoozea jela! Siwapendi mashehe, mitume na manabii wa CCM.
Unafiki ulioje,mnawaacha mashehe wanaozea jela mnajifanya kutetea amani.Nonsence!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…