Uamuzi wa kupokea wakimbizi kutoka Burundi, Rwanda na Congo haukuwahi kuamuliwa na wenyeji wa Kigoma ambao ni Abhaha, ni uamuzi wa Serikali ya JMT ikishirikiana na jumuia ya kimataifa na hasa kwa Tanzania kutimiza wajibu wake kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa, iko hivyo kote Duniani na ndio sababu Kigoma imesheheni Makambi ya wakimbizi....Kuwaita wenyeji wa Kigoma kuwa ni wakimbizi wakati wakimbizi wenyewe wakiwa kwenye Makamba katika wilaya zote za mkoa wa Kigoma, kunaashiria mambo yafuatayo, ushabiki tu wa kisiasa, chuki Binafsi tu, kutoelimika na zaidi sana mtindo wa akili ... Ambapo wewe kwenye kundi hili unaingia bila kupingwa.
..Kigoma mna HAKI zote za kulalamika kuwa mkoa wenu uliachwa nyuma.
..Msipoteze muda kujibizana na watu wenye ubaguzi na chuki miongoni mwetu Watz.
..Mtu anapokukabili kwa chuki, na matusi, wewe mkabili kwa upendo na busara.
..Ni matumaini yangu kwamba serikali ya awamu ya 6 itautendea haki mkoa wa Kigoma, na maeneo yote ya pembezoni.
..Ni matumaini yangu vilevile kuwa hayo yote yatafanyike huku tukihimiza umoja, upendo,na mshikamano, wa Watz.