Bandiwe
JF-Expert Member
- Oct 19, 2013
- 9,530
- 3,556
Kabakisha level moja tu, akiengeneza uzushi mwingine ndo atakuwa ana graduate !Mimi nahisi kama ni mchawi vil[emoji2][emoji2]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabakisha level moja tu, akiengeneza uzushi mwingine ndo atakuwa ana graduate !Mimi nahisi kama ni mchawi vil[emoji2][emoji2]
Ila kuna watu wanafiki sana na zito ni mmoja wao... hivi JPM akipatwa na mabaya wewe utafaidikaje?
Tukuulize wewe ! Maana uhusiano wa hao na uzushi wa Zito sijui ni upi ?!Vipi kwa Lisu...Azorry na Benny
Daah kwa kweli waliharibu jmapili yangu sana ! Mpaka rafiki zangu wa Kenya wamenipigia wakidai ufafanuzi.Nitashangaa kama ataendelea kurandaranda mtaani. Kwasababu kuna watu tunampemda rais hadi tunaumwa. Kasababisha tumepata heart [emoji813] attacks pasipo sababu.
Kamanda Lema na mwenzie KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe siyo watu wa kuwatilia maanani kabisa watawapotezea muda wenu bure
Mungu ni mwema
Nawatakia Jumapili yenye furaha.
Maendeleo hayana vyama!
Wewe ndie Daktari wake?Huyo Magu ni mgonjwa kweli muda utasema
Zitto, ulitoka chadema na ulipoteza imani kwa watu. Umepambana, watu wanaanza kurudisha imani kwako unakuja na upuuzi wa rais kafa na unasherehekea kuwa kuna hope.Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:
Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.
Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.
Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.
Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.
Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.
Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
Ila ukivyojuha kila mwaka unapiga kuraHakuna box la kura nchi hii, bali kuna tendo la kuwasimika wanaccm kupitia hadaa ya box la kura.
2015 mwamnyange naye mlidai muda utasema..Huyo Magu ni mgonjwa kweli muda utasema
Huyu Zitto si ndio anatumbia kila siku Magufuli mwisho wake ni uchaguzi mkuu 2020!
Ila ukivyojuha kila mwaka unapiga kura
Kwa hiyo anasubili wananchi wamuulize juu ya afya yake, kama yeye anavyouliza afya ya rais? Yeye atueleze tu bossmaana ni siku nyingi. Tangu yule binti aliyetutoka!Ww utakuwa mwendawazimu, afike aanze kuwaambia wananchi kuhusu afya bila wao kumuuliza!? Utakuwa ni mkutano au ni siku ya chanjo na vipimo?
Mbona na baba na mama yako ni follower wake!
VVU a.k.a Vyama Vya Upinzani sasa vimefirisika kabisa.
Hata kiongozi kubwa kabisa wa chama anacheza MDUNDIKO(anaogelea bwawa moja na wazushi mitandaoni)
Kwa hakika sikutarajia kabisa.
Mh. Ziro Zushi Kafiri unatakiwa kuomba radhi bila kukosa.
Hiii siielewi jomba..hivi mawakala was vyama huwa hawapo au wapi..kwa hiyo hizo hadaa zinatumia miundo ganiHakuna box la kura nchi hii, bali kuna tendo la kuwasimika wanaccm kupitia hadaa ya box la kura.
Hiii siielewi jomba..hivi mawakala was vyama huwa hawapo au wapi..kwa hiyo hizo hadaa zinatumia miundo gani
Dah ....[emoji2960]Zitto wewe si ndio Kigogo,leo mnakwenda kuaibika.