Zitto: Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema...

Zitto: Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema...

Status
Not open for further replies.
Huyu kigogo ni mpumbafuu kumbe et sasa hv huko twitter anacheka cheka tu yaan anajibu ujinga mara et atakufa tu mara recorded anaonyesha alipanga kuzusha uongo kabisa ila ndo mwsho wake huu haaminiki tena
 
Mheshimiwa Zitto, nimeona picha uliyorusha na kuleta tafsi mbaya kwa jamii, kwa wewe kama kiongozi naona uliteleza sana.
Nimekusamehe kwasababu umeomba radhi lakini ujifunze kuwa na subiri japo natambua kuwa hali halisi ya kisiasa inawasukuma wengi lkn tuuheshimu utu wa kila mtu hata kama ana roho mbaya kama fulani
Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:

Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.

Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.

Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.

Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.

Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
 
Shida sio mitandao ni watu..Mtu kama Maria Sarungi anapotaka kuuaminisha umma kuwa rais yupo ICU tunabaki tunashangaa lengo haswa ni nini??

Wanatengeneza uzushi, wanalazimisha watu wauamini kisha wanasema serikali itoke kuukanusha uzushi wao...Hizi ni akili??

Tumewadharau sana na Tanzania yao ya kufikirika ya mitandaoni..Kwenye ground hali ni tofauti sana watu wanampenda rais wao.
 
Chukulia hili in a positive way.
Watu wana mengi mioyoni mwao.
Mitandao itumike kama sehemu ya kusahihisha na kujipima na kujua jamii yako ina mtazamo gani.
 
Ila kiuhalisia hii taharuki ilikuwa huku JF na Twitter mitaani huko watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida hawajui hata huu uvumi ulioanzishwa huko twitani.

Binafsi naichukia CCM lakini hii haikuwa habari nzuri na sijapendezwa na baadhi ya viongozi wa upinzani kuonyesha chuki kwa nguvu kubwa ingawa wanapigia kelele madhalimu yanayofanywa na utawala.

Alichofanya zitto ni kusafisha mkojo kwa kutumia kinyesi.
 
Syo uzushi aliumwa alipokuwa huko mtwara, ila ka recover
Kamanda Lema na mwenzie KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe siyo watu wa kuwatilia maanani kabisa watawapotezea muda wenu bure

Mungu ni mwema
Nawatakia Jumapili yenye furaha.

Maendeleo hayana vyama!
 
awaachie mafisadi na kutokemea wazembe
naunga mkono ujinga huu..
ila JPM songa mbele usawa wa kati
Chukulia hili in a positive way.
Watu wana mengi mioyoni mwao.
Mitandao itumike kama sehemu ya kusahihisha na kujipima na kujua jamii yako ina mtazamo gani.
 
Salaam ndugu,

Kwa muda wa siku kama mbili au tatu tumeona namna taarifa kuhusiana na mheshimiwa rais zikisambaa kwa kasi kama moto katika nyasi kavu. Kasi ya taarifa hizi ilichochewa zaidi na nguvu ya mitandao ya kijamii.

Kuna ambao walisimama kidete katika kushabikia jambo hili huku kila mmoja akijifanya kujua jambo fulani kwa kuwa ni mwana connection au labda ana connection. Habari zilikua ni nyingi lakini zikibeba maudhui yale yale. Katika tukio hili imenifanya nitafakari sana matumizi ya mitandao na nguvu na ushawishi wake katika jamii.

Watumiaji wengi (siyo wote) wa mitandao ni watu wenye akili nyepesi ambazo hazina uwezo wa katafiti au kuichimba zaidi taarifa wanazotumiwa, wao kila walichotumia ni sahihi kwa 100%. Huu ni aina fulani ya ugonjwa sababu unashusha sana uwezo wa watu kutafakari na kufanya maamuzi. Watumiaji wengi wa mitandao yetu wamekuwa ni watu wa kupokea taarifa na ku forward tu, au ku download, screechot na ku share bila ya kutafakari athari ya picha au ujumbe uliomo.

Mitandao ya kijamii imepata kundi kubwa sana la watumiaji ambao huitumia bila ya tija yoyote ile, kundi hili limekua ni mhanga mkubwa sana wa taarifa na matukio yanayoanzishwa mitandaoni na vikundi vya watu wachache wenye malengo yao.
Binafsi pamoja na mara ya kwanza kupinga kwa nguvu zote namna serikali ilivyoweka mbinyo katika maswala ya mitandao, sasa hivi nimelazimika kutafakari upya na kusema ule mbinyo wa awali hautoshi, sasa hivi tunahitaji kuweka restrions nyingi na ngumu sana kwa lengo la kuiokoa jamii yetu. Kuna ugonjwa mkubwa tutaengenezewa huku mitandaoni na tutakapo kuja kustuka itakua tumeshachelewa.

Mpaka nikawaza kiwendawazimu kuwa ifike mahali taratibu za kumiliki smart phones ziwe sawa na zile za kumiliki bastora. Ninatafakari na kuogopa sana kile kinachokwenda kutupata.

Nguvu ya mitandao si ya ya kuipuuza, inaweza ikavunja na kuvuruga amani na mshikamano ndani ya nchi, inaweza ikakugeuza kuwa mchawi wa njia ya mitandao, inaweza ikadumaza watu ndani ya jamii, inaweza kusaidia kupaza sauti, na mambo mengine mengi tu mabaya na mazuri.

Niwashukuru sana Mods wa Jamii Forums kwa jinsi walivyjitahidi kudhibiti habari hizi, walitoa muda wa kutosha kwa habari kuwepo hewani kabla ya kuiondoa, hii ilitupatia wengine fipursa ya kuendelea kusoma na kujua jamii yetu imefika wapi kupitia comments zao. Hakika hali inasikitisha, tumefikaje hapa hili siyo jambo la mtu mmoja kumlaumu mwingine bali ni jambo la kila mmoja wetu kujitafakari na kuchukua hatua za kujibadilisha. Kuna watu kwa nafasi zao wana wajibu mkubwa zaidi wa kuturudisha pamoja ili tuishi kama binaadam wenye utu ndani yetu.

Afweeeeeee kabisa!
 
Endapo ni kweli hili jumba bovu likimwangukia Zitto kama anavyodai huyo aliyezusha hizi habari, namhurumia sana.
 
Ila kuna watu wanafiki sana na zito ni mmoja wao... hivi JPM akipatwa na mabaya wewe utafaidikaje?
Zitto alijua mapema kwamba kuna watakao tafsiri kama ulivyofanya ndio maana amewaombea msamaha ukiwemo na wewe. M/mungu amjalie rais afya njema ili aweze kutekeleza majukumu yake.
 
Ulikuwa wapi kusema haya kabla Rais hajatokea? Yaani baada ya #ConnectionError ndo unaibuka na kuwasaliti wenzako, He he
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom