Salaam ndugu,
Kwa muda wa siku kama mbili au tatu tumeona namna taarifa kuhusiana na mheshimiwa rais zikisambaa kwa kasi kama moto katika nyasi kavu. Kasi ya taarifa hizi ilichochewa zaidi na nguvu ya mitandao ya kijamii.
Kuna ambao walisimama kidete katika kushabikia jambo hili huku kila mmoja akijifanya kujua jambo fulani kwa kuwa ni mwana connection au labda ana connection. Habari zilikua ni nyingi lakini zikibeba maudhui yale yale. Katika tukio hili imenifanya nitafakari sana matumizi ya mitandao na nguvu na ushawishi wake katika jamii.
Watumiaji wengi (siyo wote) wa mitandao ni watu wenye akili nyepesi ambazo hazina uwezo wa katafiti au kuichimba zaidi taarifa wanazotumiwa, wao kila walichotumia ni sahihi kwa 100%. Huu ni aina fulani ya ugonjwa sababu unashusha sana uwezo wa watu kutafakari na kufanya maamuzi. Watumiaji wengi wa mitandao yetu wamekuwa ni watu wa kupokea taarifa na ku forward tu, au ku download, screechot na ku share bila ya kutafakari athari ya picha au ujumbe uliomo.
Mitandao ya kijamii imepata kundi kubwa sana la watumiaji ambao huitumia bila ya tija yoyote ile, kundi hili limekua ni mhanga mkubwa sana wa taarifa na matukio yanayoanzishwa mitandaoni na vikundi vya watu wachache wenye malengo yao.
Binafsi pamoja na mara ya kwanza kupinga kwa nguvu zote namna serikali ilivyoweka mbinyo katika maswala ya mitandao, sasa hivi nimelazimika kutafakari upya na kusema ule mbinyo wa awali hautoshi, sasa hivi tunahitaji kuweka restrions nyingi na ngumu sana kwa lengo la kuiokoa jamii yetu. Kuna ugonjwa mkubwa tutaengenezewa huku mitandaoni na tutakapo kuja kustuka itakua tumeshachelewa.
Mpaka nikawaza kiwendawazimu kuwa ifike mahali taratibu za kumiliki smart phones ziwe sawa na zile za kumiliki bastora. Ninatafakari na kuogopa sana kile kinachokwenda kutupata.
Nguvu ya mitandao si ya ya kuipuuza, inaweza ikavunja na kuvuruga amani na mshikamano ndani ya nchi, inaweza ikakugeuza kuwa mchawi wa njia ya mitandao, inaweza ikadumaza watu ndani ya jamii, inaweza kusaidia kupaza sauti, na mambo mengine mengi tu mabaya na mazuri.
Niwashukuru sana Mods wa Jamii Forums kwa jinsi walivyjitahidi kudhibiti habari hizi, walitoa muda wa kutosha kwa habari kuwepo hewani kabla ya kuiondoa, hii ilitupatia wengine fipursa ya kuendelea kusoma na kujua jamii yetu imefika wapi kupitia comments zao. Hakika hali inasikitisha, tumefikaje hapa hili siyo jambo la mtu mmoja kumlaumu mwingine bali ni jambo la kila mmoja wetu kujitafakari na kuchukua hatua za kujibadilisha. Kuna watu kwa nafasi zao wana wajibu mkubwa zaidi wa kuturudisha pamoja ili tuishi kama binaadam wenye utu ndani yetu.