Zitto: Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema...

Status
Not open for further replies.
Tumesha jua kumbe Mzee baba Dishi lake huwa linayumbaga na kuleta Chenga tuu, ni afadhali hata ya E.L. Twenty twenty atatueleza Moshi aliuonaje na je umezimika?
 
Zitto ndio alikuwa mstari wa mbele kupost picha ya Makamu wa Rais huku akishangilia hahahahaha

Leo hii unaandika unafikiri hatukumbuki?

Unakumbuka hii
View attachment 1239294
Nakumbuka yule mama mbunge marehemu maskini mama Betty Shelukindo aliwahi mwambia wewe Zitto unajua kuongea sana lakini unafiki wako utakufanya mwisho wako usiwe mzuri naona maneno ya mama yanataka kutumia,haya maneno alimwambia bungeni kwenye vipaza sauti
 
Salaam ndugu,

Kwa muda wa siku kama mbili au tatu tumeona namna taarifa kuhusiana na mheshimiwa rais zikisambaa kwa kasi kama moto katika nyasi kavu. Kasi ya taarifa hizi ilichochewa zaidi na nguvu ya mitandao ya kijamii.

Kuna ambao walisimama kidete katika kushabikia jambo hili huku kila mmoja akijifanya kujua jambo fulani kwa kuwa ni mwana connection au labda ana connection. Habari zilikua ni nyingi lakini zikibeba maudhui yale yale. Katika tukio hili imenifanya nitafakari sana matumizi ya mitandao na nguvu na ushawishi wake katika jamii.

Watumiaji wengi (siyo wote) wa mitandao ni watu wenye akili nyepesi ambazo hazina uwezo wa katafiti au kuichimba zaidi taarifa wanazotumiwa, wao kila walichotumia ni sahihi kwa 100%. Huu ni aina fulani ya ugonjwa sababu unashusha sana uwezo wa watu kutafakari na kufanya maamuzi. Watumiaji wengi wa mitandao yetu wamekuwa ni watu wa kupokea taarifa na ku forward tu, au ku download, screechot na ku share bila ya kutafakari athari ya picha au ujumbe uliomo.

Mitandao ya kijamii imepata kundi kubwa sana la watumiaji ambao huitumia bila ya tija yoyote ile, kundi hili limekua ni mhanga mkubwa sana wa taarifa na matukio yanayoanzishwa mitandaoni na vikundi vya watu wachache wenye malengo yao.
Binafsi pamoja na mara ya kwanza kupinga kwa nguvu zote namna serikali ilivyoweka mbinyo katika maswala ya mitandao, sasa hivi nimelazimika kutafakari upya na kusema ule mbinyo wa awali hautoshi, sasa hivi tunahitaji kuweka restrions nyingi na ngumu sana kwa lengo la kuiokoa jamii yetu. Kuna ugonjwa mkubwa tutaengenezewa huku mitandaoni na tutakapo kuja kustuka itakua tumeshachelewa.

Mpaka nikawaza kiwendawazimu kuwa ifike mahali taratibu za kumiliki smart phones ziwe sawa na zile za kumiliki bastora. Ninatafakari na kuogopa sana kile kinachokwenda kutupata.

Nguvu ya mitandao ya kuipuuza, inaweza ikavunja na kuvuruga amani na mshikamano ndani ya n hi, unaweza ikakugeuza kuwa mchawi wa njia ya mitandao, inaweza ikadumaza watu ndani ya jamii, inaweza kusaidia kupaza sauti, na mambo mengine mengi tu mabata na mazuri.

Niwashukuru sana Mods wa Jamii Forums kwa jinsi walivyjitahidi kudhibiti habari hizi, walitoa muda wa kutosha kwa habari kuwepo hewani kabla ya kuiondoa, hii ilitupatia wengine fipursa ya kuendelea kusoma na kujua jamii yetu imefika wapi kupitia comments zao. Hakika hali inasikitisha, tumefikaje hapa hili siyo jambo la mtu mmoja kumlaumu mwingine bali ni jambo la kila mmoja wetu kujitafakari na kuchukua hatua za kujibadilisha. Kuna watu kwa nafasi zao wana wajibu mkubwa zaidi wa kuturudisha pamoja ili tuishi kama binaadam wenye utu ndani yetu.
Hao ndio vijana wa kitanzania wanaojiita wasomi,ni aibu sana
 
Nakumbuka yule mama mbunge marehemu maskini mama Betty Shelukindo aliwahi mwambia wewe Zitto unajua kuongea sana lakini unafiki wako utakufanya mwisho wako usiwe mzuri naona maneno ya mama yanataka kutumia,haya maneno alimwambia bungeni kwenye vipaza sauti
Na bahati mbaya Zitto hawezi omba msamaha kwa kuwa mama yupo mbele za haki
 
Kwahiyo we boya unataka watu wazuiwe kumiliki smartphone
Nimejaribu tu kuwaza kiwendawazimu, maana hizi smart phone kwanza tumesha ambiwa kuwa ni 'simu janja'/zenye akili hivyo ni hatari sana kumilikiwa na mtu ambaye hana uwezo wa kuzitawala au kuzitumia akili zake. Pia simu hizi ni hatari zaidi ya bastora
 
Vipi kwa Lisu...Azorry na Benny

Kama una ushahidi si uweke? Wacha majungu! Seriali hii kama alivyosema msemaji wa serikali imeamua kuwafanyia kazi Watanzania na kuwaletea maendeleo ya kweli, wewe peleka ushahidi wako uone kama hawataufanyia kazi.
 
Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:

Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.

Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.

Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.

Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.

Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
ww zitto ndiyo chanzo cha unachokiita taharuki,,,,,,kubali kuwa umejishushia hadhi yako na umejiaibisha kama kiongozi wa chama chako kushangilia uvumi wa kifo cha binadamu mwenzio,ulifika mbali sana sana,bora ungetudanganya kuwa walidukua akaunti yako
 
bastora?.....naona kigezo kikubwa cha umiliki wa simu janja iwe uwezo wa kusoma na kuandika kwanza
 
Salaam ndugu,

Kwa muda wa siku kama mbili au tatu tumeona namna taarifa kuhusiana na mheshimiwa rais zikisambaa kwa kasi kama moto katika nyasi kavu. Kasi ya taarifa hizi ilichochewa zaidi na nguvu ya mitandao ya kijamii.

Kuna ambao walisimama kidete katika kushabikia jambo hili huku kila mmoja akijifanya kujua jambo fulani kwa kuwa ni mwana connection au labda ana connection. Habari zilikua ni nyingi lakini zikibeba maudhui yale yale. Katika tukio hili imenifanya nitafakari sana matumizi ya mitandao na nguvu na ushawishi wake katika jamii.

Watumiaji wengi (siyo wote) wa mitandao ni watu wenye akili nyepesi ambazo hazina uwezo wa katafiti au kuichimba zaidi taarifa wanazotumiwa, wao kila walichotumia ni sahihi kwa 100%. Huu ni aina fulani ya ugonjwa sababu unashusha sana uwezo wa watu kutafakari na kufanya maamuzi. Watumiaji wengi wa mitandao yetu wamekuwa ni watu wa kupokea taarifa na ku forward tu, au ku download, screechot na ku share bila ya kutafakari athari ya picha au ujumbe uliomo.

Mitandao ya kijamii imepata kundi kubwa sana la watumiaji ambao huitumia bila ya tija yoyote ile, kundi hili limekua ni mhanga mkubwa sana wa taarifa na matukio yanayoanzishwa mitandaoni na vikundi vya watu wachache wenye malengo yao.
Binafsi pamoja na mara ya kwanza kupinga kwa nguvu zote namna serikali ilivyoweka mbinyo katika maswala ya mitandao, sasa hivi nimelazimika kutafakari upya na kusema ule mbinyo wa awali hautoshi, sasa hivi tunahitaji kuweka restrions nyingi na ngumu sana kwa lengo la kuiokoa jamii yetu. Kuna ugonjwa mkubwa tutaengenezewa huku mitandaoni na tutakapo kuja kustuka itakua tumeshachelewa.

Mpaka nikawaza kiwendawazimu kuwa ifike mahali taratibu za kumiliki smart phones ziwe sawa na zile za kumiliki bastora. Ninatafakari na kuogopa sana kile kinachokwenda kutupata.

Nguvu ya mitandao ya kuipuuza, inaweza ikavunja na kuvuruga amani na mshikamano ndani ya n hi, unaweza ikakugeuza kuwa mchawi wa njia ya mitandao, inaweza ikadumaza watu ndani ya jamii, inaweza kusaidia kupaza sauti, na mambo mengine mengi tu mabata na mazuri.

Niwashukuru sana Mods wa Jamii Forums kwa jinsi walivyjitahidi kudhibiti habari hizi, walitoa muda wa kutosha kwa habari kuwepo hewani kabla ya kuiondoa, hii ilitupatia wengine fipursa ya kuendelea kusoma na kujua jamii yetu imefika wapi kupitia comments zao. Hakika hali inasikitisha, tumefikaje hapa hili siyo jambo la mtu mmoja kumlaumu mwingine bali ni jambo la kila mmoja wetu kujitafakari na kuchukua hatua za kujibadilisha. Kuna watu kwa nafasi zao wana wajibu mkubwa zaidi wa kuturudisha pamoja ili tuishi kama binaadam wenye utu ndani yetu.
Una mawazo ya kidwanzi sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom