Zitto: Siogopi kubambikiziwa uhujumu uchumi, Utakatishaji fedha (USD 2M), nakuja!

Duh!
Imenikumbusha mbali sana wakati nikiwa kijana mdogo!
 
Mungu amlinde tu
Ila daah watanzania yetu macho tu kwa kweli
 
Siku ya Zitto kutua nchini mapokezi makubwa yanaandaliwa
 
Nimefurahishwa/kusikitishwa na hiyo aya ya English alioiweka, sasa sijui bila ya hiyo asingeeleweka? Kwa maana utafikiri yoote alioyaandika kwa Kiswahili ni ujinga mpaka hapo kwenye Kiingereza.
Kaandika kiingereza kwa ajili ya wasomaji wa nje na ndani ya Tanzania ambao hawaongei au kuelewa kiswahili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona huyu kachanganya majini ya Kigoma na pemba, haogopi wala hashtushwi, naona na majini yanamfanyia kazi kumpatia ushahidi na siri.

Yetu macho na masikio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefurahishwa/kusikitishwa na hiyo aya ya English alioiweka, sasa sijui bila ya hiyo asingeeleweka? Kwa maana utafikiri yoote alioyaandika kwa Kiswahili ni ujinga mpaka hapo kwenye Kiingereza.
Mbavu, andika uliyoyaandika kwa kingereza tukuone
 
Haya sasa, ile mada na hoja zote zilizomo, alizoweka Zitto, eti hili ndio jibu lake!

Na watu wanamwagika kwa 'likes'; hata hawana subira ya tafakari juu yake!

God have mercy on us!
 
Haya sasa, ile mada na hoja zote zilizomo, alizoweka Zitto, eti hili ndio jibu lake!

Na watu wanamwagika kwa 'likes'; hata hawana subira ya tafakari juu yake!

God have mercy on us!
Ile nyimbo ya ''hakuna tume huru ya uchaguzi na CCM wanaiba kura'' imebadilika na kuwa ''wanataka kunizuia kushiriki kwenye uchaguzi'' (kama wanaiba kura kwa nini wahangaike kukukamata tena ili usishiriki uchaguzi?)
 
Sina hakika na hilo la kubadilika, kwa sababu sioni popote wanapokubali kwamba sasa kuna tume huru, au?

Yote si yanaweza kwenda kwa pamoja?
 
Jamani tuwe wakweli, chama changu cha CCM, kinafanya mambo yasio sawa penye siasa za ushindani. Hebu tujaribu kupinga uovu wowote unaotendwa viongozi wetu wa wachama pamoja na serekali ya chama chetu. Tukiendelea kutetea dhulma kwa wapinzani wetu, mwishowe tutarudiwa sisi wenyewe.

Kuna vilio vingine vya akina Zitto ni machozi ya mamba, lakini kuna mengine ni ya ukweli, tuyakemee, kuliko wapinzani wayatumie kama fimbo.

Ushindani mmoja wapo katika siasa za vyama vingi, ni kuunga mkono mazuri ya chama chako na kipinga kwa ukali na wingi wa wanachama maovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…