Zitto: Siogopi kubambikiziwa uhujumu uchumi, Utakatishaji fedha (USD 2M), nakuja!

Zitto: Siogopi kubambikiziwa uhujumu uchumi, Utakatishaji fedha (USD 2M), nakuja!

Tumekuwa taifa la kipuuzi sana, ndio maana tunachezewa na CCM kila siku, badala ya kujadili hoja ya Zitto aliyozungumzia, kama ni ya kweli, kama aliyoyasema yanaukweli, wapumbavu wanakwambia " amenikumbusha nilipokuwa mtoto, na pumbavu jingine lina quote upumbavu wa mwenzie eti hata mimi" bullshit all u bad asses!

Je, ni kweli TAKUKURU hawakaguliwi na CAG?

Je, ni kweli Rais anawalinda TAKUKURU?

Jibuni hayo maswali sio mnamjadili Zitto, halafu mnajiita GT!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
He is also systematically digging his own grave ! Would he had had a chance he could have asked Morgan Tsvangirai on what had befallen of him in the course of betraying his country believing delivering his country to the west! He was dumped by the very Americans and died in SA
Imani za ajabu ajabu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kelele za nini ndugu ukiwa huko nje?
Hiyo ni sawa na Mwanamke aliyemfungia mme wake ndani ya nyumba halafu akaanza kuporomosha matusi akimtukana mmewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suphian Juma, Mwami mimi ndugu yako nakushauri, rudi nyumbani tubishanie huku, tutishiane huku na ikibidi tufungane huku nyumbani.

Unachokifanya alikifanya Tundu Lissu alafu hakukuwa na impact yoyote. N wewe unajua na dunia nzima inajua kutumia njia hiyo hiyo ukitegemea matokeo tofauti huo ndio UMAMA ULIOPEA.

Dr. Magufuli hatishiki wala hatatishika wala hafikirii kutishwa na unachokifanya. Kwakua yeye ndiye Amir jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, pia yeye ndiye aliyepewa idhini ya kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura halali zaidi ya milioni 7.

Aidha Tanzania inayo mamlaka ya kuamua Mambo yake ya ndani yenyewe bila kuingiliwa na yeyote. Hivyo mwami achana na huo ujuha na rudi nyumbani tubishanie huku.

Ahsnte

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cherenganya,
Mtu yuko huru kuelezea hisia zake unless mkiri kuwa sasa nchi inatawaliwa kiimla na kwa nini akiwa huko mnaumia sana?

Kumbe huko ndiko kuzuri kutapikia maneno maanake huku hamchelewi kumbambikia kesi feki ya kuhujumu uchumi.
 
Kwa hiyo sisi kama mashabiki tunasemaje
Apewe ML mpaka uchaguzi au aachwe?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Rubbish. Mtu yuko huru kuelezea hisia zake unless mkiri kuwa sasa nchi inatawaliwa kiimla na kwa nini akiwa huko mnaumia sana?

Kumbe huko ndiko kuzuri kutapikia maneno maanake huku hamchelewi kumbambikia kesi feki ya kuhujumu uchumi.
Nyanjomigire,

To forwasee is to rule, naomba urudie tena kuusoma mchango wangu kisha labda kuna kitu inaweza kujikosoa kwa hili povu unalonirushia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duku duku langu ni hili: Kama CCM ina uwezo wa kuiba kura kwanini wahangaike ili kumzulia Zitto kesi ili asishiriki uchaguzi? Si wana uwezo wa kungojea wakati wa uchaguzi wakaiba?
Mwizi haachi kutumia mbinu zote anazoweza kurahisisha kazi yake.
 
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa Twitter ameandika;

Aprili 2019 nilihoji Bungeni “TAKUKURU ndio taasisi ambayo tumeipa dhamana ya kupambana na rushwa. Bajeti ya 2019/2020 tunawaombea Sh 75 bilioni LAKINI hesabu zake hazijawahi kukaguliwa na mkaguzi yeyote yule.”

“Ni kwanini hawakaguliwi wala hawafungi hesabu?

Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa inataka TAKUKURU kukaguliwa mahesabu yake. Lakini kwa kujificha mgongo wa Ofisi ya Rais ambayo Bajeti ya Taasisi hii hupitishwa, TAKUKURU wanakwepa Ukaguzi. Prof. Assad alipotaka kuikagua alizuiwa na Rais. Kwanini?

Ni kwa sababu TAKUKURU inatumika kisiasa. Kama ilivyo Ofisi ya DPP na kwa kushirikiana, TAKUKURU hutumiwa na Dola kusumbua, kutisha au kubambikia watu Kesi iwapo wanakwenda kinyume na watawala. Wanasiasa wa CCM wanaopingana na utawala wa Magufuli na wa upinzani wakosoaji hulengwa.

Mwezi Machi mwaka 2017 niliitwa na TAKUKURU kuhojiwa kuhusu kilichoitwa kupokea Fedha kutoka Benki ya Standard Chartered Hong Kong ili kuwasaidia katika uchunguzi wa uporaji wa Fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.

Nilipowauliza TAKUKURU nani kawaeleza upuuzi huo wakasema kuwa wameletewa barua na Mbunge mmoja wa zamani (hivi sasa ni RAS). Nikawaambia Mbunge huyo kawadanganya na mlipaswa kujiridhisha kwanza kwani Standard Chartered ni Benki kubwa na haiwezi kujiingiza kwenye upuuzi

Niliomba kumwona Bwana Mlowola Wakati huo akiwa Mkuu wa Taasisi na kumwambia uso kwa uso kuwa taasisi yake inatumika kisiasa. Narudia kumwambia Kaimu Mkurugenzi wa sasa hadharani kuwa taasisi yake inatumika kisiasa na yeye kakubali kutumika

Baada ya kuwaelimisha namna uchunguzi wa Tegeta Escrow ulivyofanywa na kuwaambia wawakamate waliochota Fedha Benki Kuu na kwamba nilifanya kazi yangu pamoja na wajumbe wa PAC kwa weledi wa hali ya juu sana, hawakuniita tena kuhusu hilo.

Mwaka 2018 wakaniita kuhusu tuhuma nilizowapa Watendaji wa Serikali kuhujumu Mradi wa Mchuchuma na Liganga. Nikawapa maelezo yangu ya kutosha. Ulikuwa usumbufu maana hawajachukua hatua yeyote dhidi ya wahujumu ambao ni pamoja na Rais Magufuli

Sasa TAKUKURU wanarudi tena kwenye Tegeta Escrow kwa tuhuma zingine za kubumba zenye lengo la kuniweka ndani muda mrefu ili nisishiriki Uchaguzi Mkuu. Ninawaambia tena, SIOGOPI. TAKUKURU Waache kufanya kazi kama Jumuiya ya Nne ya CCM - Wazazi, Wanawake, Vijana na TAKUKURU

Wala wasidhani kuwa nitaogopa kurudi Tanzania. Nitarudi mchana kweupe. Nitakuwa Mahakamani kusikiliza hukumu ndogo ya Kesi yangu ya uchochezi na pia kesi yangu dhidi ya Rais Magufuli kuvunja katiba ya nchi kwa kumfuta kazi CAG. Zote siku ya Jumanne tarehe 18/2/2020

- Zitto Kabwe Ruyagwa
 
Cherenganya,
Usijidanganye na maguvu ya majeshi na dola unadhani ni maguvu ya Magufuli. Kuna wakati yanachoka kama yalivyomchoka Omar Bashir wa Sudan au Yahya Jammeh wa Gabon.

Siku yake ipo atakapochomolewa Ikulu kama panya buku
 
Back
Top Bottom