Mara nyingi huyu Ndg.Zitto alikuwa anasema ataacha siasa na kwenda kufundisha je mtani wangu umefikia wapi?.Mbona naona kama ndoto yako hiyo imeyoyoma?.Mimi bado nakushauri kuwa heri rudi kafundishe/ka shike chaki.Siasa hizi za kiswahili na waswahili si size yako.Nasikia umeanzisha chama chako cha wahaa.Sasa wewe sijui yaani unakaribia kufika mwisho wa safari halafu unaamua kurudi karibu na ulipoanzia safari hauoni hilo kama hasara.Je mvua,ugonjwa,wanyama wakali wakifanya ushindwe kufika si utajilaumu kuwa tayari ningeshafika lakini hapa nimeingia choo cha kike.
Pale chadema ulikuwa mtu mzito,mheshimiwa.Yaani ulikuwa na kama miaka 3 tu hakika ungekuwa mtu mkubwa sana pale chadema lakini wewe inaonyesha haujui kula na baba.Badala ya kujipendekeza upewe minofu wewe unashindana na baba wakati yeye mifupa yake migumu,meno magumu,tumbo kubwa.Ona sasa atafaidi minofu na wewe umetemwa out.
Siasa inatakiwa uvumilivu,wewe ungekuwa mgombea bora wa Urais 2020.Lakini kwa sasa utapotea maana unatumia pesa zako kuendesha chama na hapo utapoteza tu.