Zitto: T249 CMV limemteka Nondo, mmiliki ni Deo Beda

Zitto: T249 CMV limemteka Nondo, mmiliki ni Deo Beda

Hapo kwenye kusema gari inadaiwa parking amekosea. Kamwe hautakiwi kusema mbinu unazotumia kupata taarifa. Next time hutozipata taarifa tena kwa njia hiyo, wahusika wataziba huo mwanya.
 
Hapo kwenye kusema gari inadaiwa parking amekosea. Kamwe hautakiwi kusema mbinu unazotumia kupata taarifa. Next time hutozipata taarifa tena kwa njia hiyo, wahusika wataziba huo mwanya.
Ni sawa tu na wewe ukipigiwa na Simu ngeni unavyotumia Tigopesa/mpesa kujua Jina la Muhusika 😂😂
 
Daah wahuni wameweka namba yeyote ili wateke mtu aisee mbaya sana hii kinachotakiwa ni raia kuwa na siraha za moto kama SA tu bila hivyo mtaisha wote kizembe maana watu wanakuja kukuteka wakijua hauna siraha yeyote ila ukiwa vitani hata akija mtu na nguo za kazi zao watwange risasi tu itajulikana huko mbele kuliko kwenda kufa kijinga..


Mkuu hii itakuwa hatari sana, Mungu asaidie tusifike huku
 
Ila Rais wetu kama haoni haya yanayotendeka basi atakuwa ni sehemu ya tatizo. Ili uongoze unahitaji watu, sasa kama watu wanatekwa mchana kweupe lakini hakuna kukemea nini maana ya kuwa kiongozi?
 
Kuna uwezekano minja hahusiki, wahuni wamecopy namba yake. Nivema kua makini katika kumshutumu mwenye gari.
 
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema gari namba T 249 CMV inayotajwa na Jeshi la Polisi kuwa imetumika na Watekaji kumteka Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa wa ACT, Abdul Nondo, inamilikiwa na Mtu anayeitwa Deogratius Beda Minja.

Zitto amesema “Tunataka Abdul Nondo aachiwe mara moja akiwa mzma wa afya, tafadhali sana, gari inadaiwa parking na tumejua kila mahala gari hiyo inapaki, mwacheni Nondo haraka iwezekanavyo Wapumbavu wakubwa nyie”

Jeshi la Polisi limesema leo December 01,2024 majira ya saa 11.00 alfajiri katika eneo la stendi ya Magufuli Mbezi Louis Dar es salaam kuna Mtu mmoja Mwanaume amekamatwa kwa nguvu na kuchukuliwa na Watu waliokuwa wakitumia gari lenye usajili wa namba T 249 CMV aina ya Landcruiser rangi nyeupe na kwamba ilielezwa na Mashuhuda kuwa katika purukushani za ukamataji begi dogo lilidondoshwa na baaadhi ya vitu vilivyokuwemo vimetambuliwa ni vya Abdul Omary Nondo.

Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “Ufuatiliaji wa tukio hilo ulianza mara tu baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo Polisi, sambamba na kufungua jalada”
T 249 CMV hii namba ni ya mchongo!
Utakuta gari hilo lipo Kilimanjaro,Tena kijijini na halijawahi kufika Dar.
 
Hapo kwenye kusema gari inadaiwa parking amekosea. Kamwe hautakiwi kusema mbinu unazotumia kupata taarifa. Next time hutozipata taarifa tena kwa njia hiyo, wahusika wataziba huo mwanya.
ni njia inayojulikana, alafu wale jamaa ni mabingwa wakutumia namba za zamani chuma ya mwaka huu kutoka kiwandani ila number C ni kawaida. hivo mimi natilia shaka hata hiyo namba yenyewe
 
Lengo ni kutuhamisha katika mjadala wa rafu za uchagizi wa serikali za mitaa
 
Back
Top Bottom