Ni dhahiri kuwa JPM hakua Mbaya bali alizunguka na watu wenye siasa za kibabe kama makamu wake wakati huo ambaye alikopi siasa za Zanzibar chini ya kauli mbiu ya mapinduzi daima .
Dr. Bashiri Ali chini ya siasa za CUF za mapanga shaa.
Kama mwenyekiti wa sasa wa CCM angekua sio tatizo bado angesimamia kauli zake lakini anaonekana hata wakati ule alikua ni mzuri mbele ya macho ya watu lakini nyuma yake ameshika kilipuzi. Ndio maana Dr. Bashite ni rafiki yake wa karibu . Bird with the same wings fly together.
Kwa hiyo dikteta ni yule anayeona kifo kama vile ni jambo la kawaida na kutoa tahadhari kuwa watu ajiandae tu maana kifo ni kifo tu wasione ajabu . Ndio maana wanaofurahia vifo na uhuni mwingi kama akina Shehe Mwaipopo wanakua salama na wanashangiliwa sana na watawala kuliko Taasisi yenye waumini wengi kwa wasomi wa hii mifumo yote duniani kama kanisa katoliki walikemea mauaji na uhuni ,wanaotukanwa matusi makubwa sana kwenye mitandao na polisi chini ya CP Awadhi hawajawahi kumkamata mtu kuwa amewatukana maaskofu na viongozi wa dini . Yaani kuwakosoa watendaji wa asiofuata sheria limekua ni kosa la kuuawa lakini uhalifu mwingine limekua ni suala linalokingiwa kifua na haki jinai . Leo mbakaji ,mlawiti, muuza madawa , n.k wanakinga kubwa sana kwenye kesi kuliko wakipinga mauaji na utekaji.
Hawata acha maovu yao kama wanaoyafanya wanapongezwa na kupandishwa vyeo .