GE2025 Zitto: Wafanyabiashara zamani waliichangia CCM kisirisiri kwa hofu ya kashfa zao kuibuliwa Bungeni

GE2025 Zitto: Wafanyabiashara zamani waliichangia CCM kisirisiri kwa hofu ya kashfa zao kuibuliwa Bungeni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Zitto Kabwe kupitia mtandao wa X, amesema kuwa baada ya CCM kuua bunge 2020 wafanyabiashara sasa hawajifichi tena kuchangia chama hicho hadharani tofauti na zamani ambapo bunge lilikuwa nguvu hivyo walilazimika kuvichangia vyama vyote kisirisiri ili kuhakikisha wanalinda maslahi yao.

----

CCM inapata kiburi cha ku parade wafanyabiashara kukusanya fedha kwa sababu WALIUA Bunge. Miaka ya nyuma wafanyabiashara walichangia CCM lakini sio hadharani kwa sababu walijua kuwa kashfa zao zitaibuliwa Bungeni.

Wafanyabiashara ilibidi wachangie vyama vyote kisiri ili kuhakikisha wanalinda maslahi yao.

Baada ya kupata Bunge Kibogoyo mwaka 2020 CCM inaamini kuwa itaendelea kuwa na Bunge kibogoyo tena na hivyo imejenga kiburi cha ajabu kabisa na wafanyabiashara nao bila kujali sensitivities za wateja wao wamejawa na kibri.

Watanzania wanayo nafasi ya kuwaonyesha Watawala kuwa wao ndio wenye nchi. Tafrija ya jana Mlimani City ya MONEY LAUNDERING inapaswa kuwa TURNING POINT ya Siasa zetu.

View attachment 3439995
Kwa mara ya kwanza naunga hoja ya Mh Zitto, sikutegemea kuyaona haya katika siku zangu za mwishoni!
 
Kama nimeelewa sehemu ya ujumbe wa ZZK, kuwa na bunge lisilo kibogoyo si kusaidia nchi na wanachi bali kuvisaidia vyama vyote/vingi vya siasa kupata michango toka kwa wafanyabiashara. Hii ni kwa sababu wakichangia vyama vyote sisi wanachi hatutajua kashfa zao maana bunge lote litakuwa kibogoyo kupitia michango ya wafanyabiashara kwa vyama vya siasa. Kwa maelezo mengine ZZK anaumia kuona ccm inachangiwa peke yake bila vyama vingine kuchangiwa.
Akili kubwa,nimeelewa hivi pia
 
Ndiyo hivyo.
 
Zitto Kabwe kupitia mtandao wa X, amesema kuwa baada ya CCM kuua bunge 2020 wafanyabiashara sasa hawajifichi tena kuchangia chama hicho hadharani tofauti na zamani ambapo bunge lilikuwa nguvu hivyo walilazimika kuvichangia vyama vyote kisirisiri ili kuhakikisha wanalinda maslahi yao.

----

CCM inapata kiburi cha ku parade wafanyabiashara kukusanya fedha kwa sababu WALIUA Bunge. Miaka ya nyuma wafanyabiashara walichangia CCM lakini sio hadharani kwa sababu walijua kuwa kashfa zao zitaibuliwa Bungeni.

Wafanyabiashara ilibidi wachangie vyama vyote kisiri ili kuhakikisha wanalinda maslahi yao.

Baada ya kupata Bunge Kibogoyo mwaka 2020 CCM inaamini kuwa itaendelea kuwa na Bunge kibogoyo tena na hivyo imejenga kiburi cha ajabu kabisa na wafanyabiashara nao bila kujali sensitivities za wateja wao wamejawa na kibri.

Watanzania wanayo nafasi ya kuwaonyesha Watawala kuwa wao ndio wenye nchi. Tafrija ya jana Mlimani City ya MONEY LAUNDERING inapaswa kuwa TURNING POINT ya Siasa zetu.

View attachment 3439995
Natamani tuwe na mabunge mawili.la ukawa na mafisi maji tuone nani ataatutoa hapa.Haiwezekani yule bibi kaaxhia Uranium kwa kipande cha pweza na nyie wahenga old School mpo tuu
 
CCM imeshaaharibu karibu kila

Bunge tayari
Administration ya serikali
Mahakama tayari
TISS tayari
Jeshi la polisi (sehemu kubwa)

Bado Magereza, Uhamiaji na JWTZ

Miaka mitano ijayo watamaliza hiyo kazi ndio wanachoweza ni kuharibu

Sio muda mrefu utasikia wauza madawa wametoroka jela

Utoaji wa uraia kiholela ili waarabu wa Oman na wengineo wapate ardhi kirahisi

Huko JWTZ na kwenyewe maafande watapeleka watoto, kupanda rank haraka. Lije kuwa kama jeshi la Nigeria au Congo; hawawezi pigana hata na vikundi vya wanamgambo.

Ni mwendo wa hela inaongea popote na tamaa ya watumishi kotę-kote.

It’s heading towards a fail state
Tunaenda Kubaya sana Congo DRC wenye pesa watanunua jeshi
 
Hapa ndio ujuha wa sisi watanzania ulipo.
Huwa hatupendi kujadili hoja, tunamjadili mtoa hoja.
Kama kuna mwanasisa ambaye hatakiwi kabisa kutiliwa maanani wala kuaminiwa mahala popote anapoongea nchi hii basi ni huyo muha kiongozi wa wasaliti.

Zitto ni mpuuzi sana hana tena credibility alijifanya mzalendo na jasiri sana enzi ya awamu ya tano, ukimtoa Lisu mtu mwingine aliyekuwa anaikosoa serikali ya JPM mara kwa mara alikuwa ni Zitto

Lakin sasa hivi awamu ya samia kuna mambo mengi sana ya ovyo yanafanyika ila yuko kimyaa, utafikiri hayupo nchini.. halafu anakuja kuongelea jambo ambalo linahusu maslahi ya vyama vya siasa, sasa ni akili hiyo.

Huyu Zitto hana tofauti na yule Fatima Karume aneyejiita shangazi, na yeye alijifanya sana ana uchungu na nchi hii enzi za awamu ya Magu, hakuna ambacho alikiacha kipite bila kukitolea neno.. ila sasa nchi inaharibiwa na Mzanzibar mwenzake yuko kimyaa utafikiri hayupo.

Hakuna mtu mwenye akili timamu atamchukulia serious zitto kabwe kwa sasa, haijalishi anachokiongea kina uongo au ukweli kiasi gani.
 
Back
Top Bottom