Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Akiwa huko Mihambwe Zitto amewataka wananchi wachague mtu mwenye uwezo wa kumshinda Magufuli.
Ndugu Zitto amewaambia wananchi kuwa lengo kuu ni kumshinda Magufuli na amewataka wananchi wasigawe kura, maana wakifanya hivyo Magufuli atapita katikati kiulainii.
Katika mahesabu makali ya upinzani namna ya kushirikiana ni dhahiri kwa muda mrefu ACT wazalendo wako na Tundu Lissu katika ngazi ya uraisi, na hii inathibitishwa na mgombea wao kutofanya kampeni yoyote kubwa hata katika maeneo yenye kuungwa mkono sana ACT kama vile Kigoma na mikoa ya kusini ukiondoa Lindi kwa mheshimiwa Membe.
Katika hali hii huu utakuwa ushirikiano wa kisayansi kuwahi kutokea nchini, na umeonyesha kuzaa matunda ndiyo maana CCM inahaha kutumia vyombo vya serikali kama NEC na polisi kuipa upendeleo wa dhahiri. Kama upepo wa kampeni utaendelea hivi, basi CCM wajiandae kuachia Ikulu au wajiandae kuchakachua uchaguzi, lakini ni dhahiri wananchi wameshapitisha hukumu yao kuwa CCM imepwaya sana.