Zitto: Wanasiasa Tanzania wanapata ugumu wa kufanya siasa bila uadui

Zitto: Wanasiasa Tanzania wanapata ugumu wa kufanya siasa bila uadui

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kiongozi wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema siasa zilizo bora ni siasa za Ushawishi.

Hata hivyo amesema wanasiasa wa Taznzania wanapata ugumu wa namna ya kufanya siasa bila kuhasimiana na kugawa watu.

Mwenye mawazo tofauti sio adui. Anawaza tofauti na wewe tu.

1625463333016.png
 
Bora zito kabwe nao kauona mchezo.

Kuna watu wanatengeneza uadui kwanza alafu ndo wanaanza siasa.
 
... ila usisahau kwamba CCM ndiye baba wa chuki siasa za Tanzania!
 
Zitto ni super smart.

Chadema bado hawakui kabisa.
 
Zitto ni super smart..
Chadema bado hawakui kabisa..
He is not super smart, rather he is an opportunist, anajipendekeza kwa CCM akitegemea kupata kitu, ila wakimpiga tena kama alivyopigwa kule Kigoma kwenye chaguzi ndogo ataanza kulia, kumuamini Zitto ni kujipotezea muda.

Kwake Katiba Mpya haina maana kama atapata viti viwili/vitatu vya ubunge kwa hii katiba mbovu iliyopo, Chadema wao wameshapevuka mara elfu mbili, hawafikirii tena viti vya ubunge kwani wameshakuwa navyo vya kutosha, Chadema sasa wanaangalia maslahi ya taifa kwa ujumla wake.
 
Zitto angeacha unafiki kidogo kwanza angejiuliza huo anaoita uadui unasababishwa na nani? akishapata jibu unasababishwa na CCM na viongozi wao kwa kuvunja sheria za nchi makusudi, angeanza kuwakemea hao wanaosababisha "tension" kwa wengine kwa kuwanyima haki zao, kabla hajasisitiza siasa za kustahimiliana.

Ningependa nae akawekwe ndani na CCM miezi atleast sita akitoka huko nimuone kama ataandika hizo taarabu zake twitter, siasa zake za kujipendekeza zimemfanya awe "rafiki" wa CCM ndio maana haaminiwi na vyama vya siasa vinavyojitambua nchi hii, bora Rungwe kuliko Zitto, akitoka twitter atawaomba Chadema waungane kwenye uchaguzi fulani, jamaa ni popo.
 
Kwa kiswahili cha mtaani maana yake wanasiasa wanatengeneza 'kiki' kwanza ili kupata mileage ya kufanya siasa! How true!!!
 
Kiongozi wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema siasa zilizo bora ni siasa za Ushawishi

Hata hivyo amesema wanasiasa wa Taznzania wanapata ugumu wa namna ya kufanya siasa bila kuhasimiana na kugawa watu

Mwenye mawazo tofauti sio adui. Anawaza tofauti na wewe tu.

Nilimkubari Zitto kabla hajatoka Chadema, na bado naendelea kumkubali.. Zitto ni mwanasiasa msomi, anayetumia elimu na ubongo wake vizuri Sana.. nitaendelea kukusungwa mkono ZZK maana naona wewe ndiwe first ya upinzani wa kweli, na siasa zisizogawa taifa.. najua Kuna muda mwingine unaumia kutoka a na rafu za CCM, lakini huwa hukimbilii maandamano, huwa unafuata sheria, Kama ni mahakamani utaenda kudai hako yako
 
Kiongozi wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema siasa zilizo bora ni siasa za Ushawishi.

Hata hivyo amesema wanasiasa wa Taznzania wanapata ugumu wa namna ya kufanya siasa bila kuhasimiana na kugawa watu.

Mwenye mawazo tofauti sio adui. Anawaza tofauti na wewe tu.

Chumvi ikiharibika itatiwa nini nini ili kuifanya upya? Haifai kabisa bali huambulia kutupwa na kukanyagwa na watu!!
Zito ni chumvi iliyoharibika!
 
Zitto ni super smart.

Chadema bado hawakui kabisa.
U-super smart wa Zitto ni upi? Zitto angeweza kuwa mwanasiasa mzuri kama siyo ubinafsi. Ana ubinafsi sana na kupenda kujiona ana akili kuliko watu wengine. Huyu hata akipewa nchi ni mtu hatari sana. Halafu katu hataki challenge kutoka sehemu nyingine.
 
Siasa siyo uhasama, siasa siyo uadui.
Unazalisha maadui mwenyewe kwa siasa zako za ovyo, ukidhibitiwa unalia lia kutafuta huruma za wananchi.
Zitto Kabwe piga siasa za kistaraabu tuko nyuma yako
 
Kiongozi wa ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema siasa zilizo bora ni siasa za Ushawishi.

Hata hivyo amesema wanasiasa wa Taznzania wanapata ugumu wa namna ya kufanya siasa bila kuhasimiana na kugawa watu.

Mwenye mawazo tofauti sio adui. Anawaza tofauti na wewe tu.

Baada ya kufariki kwa JPM ndo wamejua?

Matusi yote na chochoko zote ndo walikuwa wana mmwagia?

Eti hadi wanamchongea kwa wazungu.

Sasa wamebaki waparuane wao kwa wao.
 
Back
Top Bottom