Ziwa Jipe hatarini kutoweka, samaki adimu wa ‘Jipe Tilapia’ wakabiliwa na tishio la kutoweka Duniani

Ziwa Jipe hatarini kutoweka, samaki adimu wa ‘Jipe Tilapia’ wakabiliwa na tishio la kutoweka Duniani

Tuone picha ya hilo ziwa maana mwanzo hadi mwisho sijaliona naona njia ya kuingilia tu 
 
Hili ziwa lilikua maarufu kwenye maarifa ya jamii nilipomaliza sijawahi kulisikia tena mpaka leo hapa
Ni kwamba mimi sijasoma shule zamani ama, maarifa ya jamii hili bwawa lilitajwa? Embu tukumbushane chief
 
Wazanzibari mnajistukia sana. Mbona nyakati zile miaka ile ulionekana mtu smart sana upstairs kaka?

Mtu ambaye hajakusoma vizuri hawez kuelewa kama umeandika sarcasm
Bado niko smart mkuu. Sisi ni old school. Ila kuna vijana wapuuzi ambao wameiharibu JF ile tuliyoizoea.
Sorry kama nimekukwaza.
 
Ni kwamba mimi sijasoma shule zamani ama, maarifa ya jamii hili bwawa lilitajwa? Embu tukumbushane chief
Lilitajwa mkuu. Haswa maarifa ya jamii ya la tatu
 
Kutoweka kwa samaki chanzo chake ni uvuvi, usiozingatia uhifadhi. Samaki wanavuliwa kwa wingi wenda hata bila usimamizi, kwanini wasitoweke!! Wanavua mpaka mazalia ya samaki.

Ni sawa Ziwa Rukwa, siku hizi visamaki (Tilapia), samaki wadogo wadogo sana wanavuliwa.

Kuhusu magugu: Magugu yanadhibitika, uvuvi usiozingatia uhifadhi ndio unaoleta hatari zaidi ya kutoweka samaki.
 
Samaki wake huwa watamu sana

Hayo magugu hayafai kung'olewa?
 
Aseeeh hiyo kitu bado ipo kumbe...... Ilikuwa Rombo zamani na wakenya
Ndio kama sio wanawinda wanyam basi ni mbao
Walipiga kazi wakazulumiana. Wakamuua, sasa hata aliozulumiana nao hawajahulikaba kesi ikaishia hivyo

Ila polisi wa Kenya walitusaidia sana, hata walimsafirisha kwenye defender yao mpaka Huruma Hospital.

Mwili haukufaa kuacha tulizika na polisi fasta tu
 
Tanzania au Afrika Kwa ujumla watu wanaangalia matumbo Yao tu, hawaangalii kwamba vizazi vya baadae itakuwaje
 
Hili ziwa moja kati ya chanzo muhimu kwa mto Pangani ambao umefanya kupatikane kwa kwa bwawa la Hale. Tawi mto la Mto Pangani liitwalo mto Ruvu (Si mto Ruvu wa Pwani), limetokana na ziwa hilo. Kupungua maji kunaweza kuathiri kwa namna fulani mto Pangani.

Pia hayo Magugu maji ni hatari sana ukiachilia mbali kupunguza kina, pia yanaficha wanyama hatari ikiwemo Nyoka na Mamba, watu wanaweza shambuliwa hata kuliwa
 
Iko siku watu watasafiri kwenda kuona mto sehemu kama Utalii na watalipia
 
Back
Top Bottom