Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

Zanzibar ni tanzania na Tanzania ni zanzibar.

Hakuna mjadala kuhusu hili
kama watanganyika hamna mjadala waZanibar tunao tena mkubwa na unazidi kushika kasi bila ya kuzisahau au kuziacha nyuma zile kilomita kumi tayari mikoa husika imeshajulishwa hadi Mombasa.
 
hata ile miji inaypakana na Ziwa Malawi nayo inaweza ikajikata na kujiunga Malawi . Kama Chato wamejikata wanajiita Mkoa na airport ya Kimataifa.
 
Kabisa mkuu,ipo siku watasema hata Kyela ni yao kulingana na jiografia ya ziwa lao
Hawawezi kudai kyela ni yao, hilo ziwa Malawi walishapewa tangu zamani usifikiri wamekurupuka, sema tu walikuwa wanatuonea aibu kutuambia ukweli. Ndiyo maana rais wao alivyokuja aliitumia kauli Fulani ya kwamba anatukaribisha tukale samaki wa ziwa nyasa hii binafsi niliona ya kwamba watanzania hatutaziwiwa kuvua samaki Ila tujue hatuna chetu
 
kama watanganyika hamna mjadala waZanibar tunao tena mkubwa na unazidi kushika kasi bila ya kuzisahau au kuziacha nyuma zile kilomita kumi tayari mikoa husika imeshajulishwa hadi Mombasa.
Hizo km wajerumani walishamalizana na sultani
 
Nimetoka kuprove kama mtoa mada yupo sahihi, nilichokuja kugundua Watanzania tumeporwa Kipande cha Ziwa NYASA na Jina nalo limebadilishwa kutoka LIKE NYASA mpaka LAKE MALAWI.
 
Mkuu hivi kulikuwa na mkataba wa pili wa kugawanywa ziwa kweli? Ni onavyo Mimi Kama ulikuwepo basi ni wa msumbiji chini ya wareno na Malawi chini ya waingereza na sio tanganyika. Nakumbuka Bernard membe alikuwa anauelezea huu mgogoro kipindi kile cha jk hakuelezea uwepo wa mkataba wa pili zaidi ya kulaumu huo mkataba wa mwanzo ulivyowanyima haki watanganyika
Ukiangaliza kwa makini ukiwa neutral unaona Malawi wana evidence kubwa kutuzidi. Bahati nzuri sio wagomvi kama mfano Kenya
 
Hao maaskari wanaolindaga mipaka walikuwa wapi hadi wamalawi wahamishe mipaka?

Ina maana hamna wanajeshi kabisa kwenye hilo ziwa!? Kama ni hivyo, basi hatuko salama!

Hili ziwa lina kesi na iko kwenye usuluhishi
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Iko hivi, kipindi kulivyoibuka vita ya maneno kati yetu na Malawi niliangalia mpaka wetu na Malawi kupitia picha za satellite nikaona mpaka huo umepita katikati ya ziwa Nyasa.

Siku chache mbeleni nikaangalia tena nikaona mpaka upo pale pale lakini sehemu hiyo/mpaka huo ukiwa umebadilishwa rangi kuwa nyekundu.

Kuchorwa mpaka huo kwa rangi nyekundu ni kuashiria kuna mzozo ambao umoja wa mataifa haujaelewa ni nani hasa mwenye haki na eneo hilo kati ya Tanzania na Malawi.

Tangu 2015 sikuwahi kuchungulia tena eneo hilo, ila leo nimeangalia mpaka huo kupitia camera za satellite nikashtuka baada ya kuona mpaka huo umehamishwa alafu wakabadili na jina la ziwa hilo na kuliita ziwa Malawi 😠

Yaani kwa kifupi lile ziwa hatuna mamlaka nalo tena! Tumeporwa kilomita nyingi sana za mraba huku serikali yetu ikiwa haijui kinachoendelea juu ya ziwa hilo lenye utajiri wa gesi, mafuta na spish za samaki zaidi ya 1500.

Mpaka huo umehamishwa kutoka katikati ya ziwa hadi kwenye fukwe za nchi yetu huku wakibadili kabisa jina la ziwa letu na kuliita ziwa Malawi kama inavyoonekana kwenye picha.

View attachment 1804817

Linganisha na mpaka ambao tuliachiwa na wakoloni katika picha hii.

View attachment 1804818

Ikumbukwe kwamba miaka michache kipindi cha serikali ya Jakaya kikwete tulikuwa na mzozo Malawi kuhusiana na hili ziwa hadi kukatokea vitisho vya kuingia vitani kila nchi ikidai italinda mpaka wake. Malawi wakidai ziwa lote ni lao huku Tanzania tukidai mpaka wa wakoloni ambao ulipita ndani ya ziwa huku sisi tukiwa na eneo lenye upana zaidi ya Malawi.

Hii maana yake nini? Sisi ni wapole sana au hatupo tayari kulinda mipaka yetu?

Kwanini wazungu wameridhia kumega nchi yetu na kuikabidhi Malawi?

Naomba serikali yetu tukufu itoe maelezo kuhusu hili jambo maana sio dogo.

Tukiendelea kunyamaza kuna siku watasema mkoa wa Mbeya ni wao
Ile tume ya usuluhishi ikiongozwa na rais wa zamani wa Msumbiji Chisano hatukupata mrejesho wa suala hili lilliishia wapi.
 
Katika hili ndio inatakiwa uzalendo wetu uonekane.
Hakuna cha ccm, Chadema, CAF, ACT Wala chawuma
Ila uzalendo kwa uangalifu wa hali ya juu sana. Kati ya majirani zetu tulionao ambao wamepinda ni Malawi.
You can imagine kwamba askari wanafuatilia mhalifu na kwa kujisahau kidogo tu wameingia nchini mwao, gari ya Polisi inapigwa mawe na askari wetu kunusurika kuuawa, badala ya wao (wamalawi) nao kuangalia ule upande mwingine kwamba hawa askari nao walikuwa kazini na walikuwa wanafuatilia mhalifu. Kwao wao wamalawi kwa mfano, tuseme KIBINADAMU (siyo kisheria), na katika ule ubinadamu wa kawaida kabisa usiohitaji kuwa na sifa za kimalaika, nani alikuwa na kosa kubwa zaidi kati ya askari wetu na mhalifu aliyekuwa akiwakimbia Polisi?

Hili swala la hawa askari kufukuzwa kazi mimi limenigusa sana na kama ningekuwa mwanasheria, ningejaribu kuishauri Serikali ili iwarudishe kazini. Adhabu waliyowapa ya kuwafukuza kazi askari hao ni kubwa mno, japo inalingana na KOSA WALILOFANYA, lakini ukiangalia kwa upande mwingine hailingani na MAZINGIRA YA KOSA WALILOFANYA, sana sana wangewasimamaisha kazi kwa muda na kuwarudisha tena kazini. Mimi ningeshauri warudishwe kazini na kwa sababu hata wakirudishwa, hao wamalawi wenyewe hawataweza kujua kuwa wamerudishwa, wao watatendelea kujua tu kuwa walishafukuzwa kazi, that way they will continue being happy kuhusiana na swagga la askari hawa
Kwa hatua kali kama hizi walizochukuliwa askari hao kwa sasa, wakati mwingine tutakuwa tunatengeneza nidhamu ya woga kwa askri wetu, kitu ambacho siyo kizuri sana. Juzi tu wametupigania kwenye janga la ajabu la mtu aliyekuwa ameshika silaha na kuua baadhi ya askari, sasa leo tena askari hao hao wanafukuzwa kazi kwa kosa ambalo liliwaponyoka na la kuchochewa zaidi na wamamalwi wenyewe kwa kutokuwa loyal lwa askari wetu?
Sisemi kwamba kuingia na silaha ndani ya mipaka ya nchi nyingine siyo kosa, ni kosa ila wakati mwingine tuangalie hao walioingia na silaha motive yao ilikuwa nini nini!

Ingekuwa kwa mfano tuseme, askari hao hao kwa bahati mbaya wameingia ndani ya nchi kama Kenya au Uganda, wangepigwa hayo mawe? Kenya au Uganda wasingepigwa isipokuwa wangepewa ushirikaiano na badala yake mhalifu aliyekuwa akiwakimbia askari angekamatwa

Mimi kama mtanzania maskini nashauri askari hao wasamehewe kwa onyo kali la kutokurudia kosa hilo kwenye utumishi wao wote, warudishwe kazini ikiwezekana. After all, wamalawi wenyewe hawatajua kama wamerudishwa kazini. Wawarudishe kimya kimya wala wasitutangazie hata sisi wanachi kuwa wamewarudisha.

Jamani tukumbuke kwenye issue ya juzi risasi zilipokuwa zinarindima barabarani kazi waliyofanya haikuwa ndogo, mpaka wengine wamepoteza maisha. Leo kwa bahati mbaya tu watu hao hao wame-tress pass tena kwa bahati mbaya tu na wakiwa na nia njema, tunawafukuza kazi?. Nashauri IGP awafikirie na hawa pia kama alivyowafikiria wale ambao walihangaika na tukio lile la ughaidi. Kwanza kile itendo tu cha kuwa wamefukuzwa kazi mpaka muda huu, kinawatosha kama adhabu inayolingana kabisa na kosa walilofanya, assuming wanarudishwa tena kazini hata leo
Watanzania maskini hawa hawana ajira, kwa bahati mbaya hawa watoto pengine wamejiunga na jeshi la Polisi hata miaka 10 wengine hawajafikisha, mambo mengi bado wanajifunza. Naomba rai positive ya watanzania iwe juu ya watoto hawa ili waweze kusamehewa na kurudishwa kazini

I have been in Malawi, nawajua attitude yao ilivyo kwetu
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Iko hivi, kipindi kulivyoibuka vita ya maneno kati yetu na Malawi niliangalia mpaka wetu na Malawi kupitia picha za satellite nikaona mpaka huo umepita katikati ya ziwa Nyasa.

Siku chache mbeleni nikaangalia tena nikaona mpaka upo pale pale lakini sehemu hiyo/mpaka huo ukiwa umebadilishwa rangi kuwa nyekundu.

Kuchorwa mpaka huo kwa rangi nyekundu ni kuashiria kuna mzozo ambao umoja wa mataifa haujaelewa ni nani hasa mwenye haki na eneo hilo kati ya Tanzania na Malawi.

Tangu 2015 sikuwahi kuchungulia tena eneo hilo, ila leo nimeangalia mpaka huo kupitia camera za satellite nikashtuka baada ya kuona mpaka huo umehamishwa alafu wakabadili na jina la ziwa hilo na kuliita ziwa Malawi 😠

Yaani kwa kifupi lile ziwa hatuna mamlaka nalo tena! Tumeporwa kilomita nyingi sana za mraba huku serikali yetu ikiwa haijui kinachoendelea juu ya ziwa hilo lenye utajiri wa gesi, mafuta na spish za samaki zaidi ya 1500.

Mpaka huo umehamishwa kutoka katikati ya ziwa hadi kwenye fukwe za nchi yetu huku wakibadili kabisa jina la ziwa letu na kuliita ziwa Malawi kama inavyoonekana kwenye picha.

View attachment 1804817

Linganisha na mpaka ambao tuliachiwa na wakoloni katika picha hii.

View attachment 1804818

Ikumbukwe kwamba miaka michache kipindi cha serikali ya Jakaya kikwete tulikuwa na mzozo Malawi kuhusiana na hili ziwa hadi kukatokea vitisho vya kuingia vitani kila nchi ikidai italinda mpaka wake. Malawi wakidai ziwa lote ni lao huku Tanzania tukidai mpaka wa wakoloni ambao ulipita ndani ya ziwa huku sisi tukiwa na eneo lenye upana zaidi ya Malawi.

Hii maana yake nini? Sisi ni wapole sana au hatupo tayari kulinda mipaka yetu?

Kwanini wazungu wameridhia kumega nchi yetu na kuikabidhi Malawi?

Naomba serikali yetu tukufu itoe maelezo kuhusu hili jambo maana sio dogo.

Tukiendelea kunyamaza kuna siku watasema mkoa wa Mbeya ni wao
Sio kila kitu basi ukitegemee ktk google, kwa hili lanmipaka ya nchi binafsi nasa hapana google sio wanao nyoosha nankuitambua mipakq ya mchini vipo vyombo vya kisheria kabisaa tena vya ki dunia mfano ule mgogoro wa kenya na somalia juu ya mpaka wa bahari !!

Lkn pia niulize hawa Malawi je wamedai umiliki wa ziwa hili kwa upande ule wa Mozambique ?
 
Ila uzalendo kwa uangalifu wa hali ya juu sana. Kati ya majirani zetu tulionao ambao wamepinda ni Malawi.
You can imagine kwamba askari wanafuatilia mhalifu na kwa kujisahau kidogo tu wameingia nchini mwao, gari ya Polisi inapigwa mawe na askari wetu kunusurika kuuawa, badala ya wao (wamalawi) nao kuangalia ule upande mwingine kwamba hawa askari nao walikuwa kazini na walikuwa wanafuatilia mhalifu. Kwao wao wamalawi kwa mfano, tuseme KIBINADAMU (siyo kisheria), na katika ule ubinadamu wa kawaida kabisa usiohitaji kuwa na sifa za kimalaika, nani alikuwa na kosa kubwa zaidi kati ya askari wetu na mhalifu aliyekuwa akiwakimbia Polisi?

Hili swala la hawa askari kufukuzwa kazi mimi limenigusa sana na kama ningekuwa mwanasheria, ningejaribu kuishauri Serikali ili iwarudishe kazini. Adhabu waliyowapa ya kuwafukuza kazi askari hao ni kubwa mno, japo inalingana na KOSA WALILOFANYA, lakini ukiangalia kwa upande mwingine hailingani na MAZINGIRA YA KOSA WALILOFANYA, sana sana wangewasimamaisha kazi kwa muda na kuwarudisha tena kazini. Mimi ningeshauri warudishwe kazini na kwa sababu hata wakirudishwa, hao wamalawi wenyewe hawataweza kujua kuwa wamerudishwa, wao watatendelea kujua tu kuwa walishafukuzwa kazi, that way they will continue being happy kuhusiana na swagga la askari hawa
Kwa hatua kali kama hizi walizochukuliwa askari hao kwa sasa, wakati mwingine tutakuwa tunatengeneza nidhamu ya woga kwa askri wetu, kitu ambacho siyo kizuri sana. Juzi tu wametupigania kwenye janga la ajabu la mtu aliyekuwa ameshika silaha na kuua baadhi ya askari, sasa leo tena askari hao hao wanafukuzwa kazi kwa kosa ambalo liliwaponyoka na la kuchochewa zaidi na wamamalwi wenyewe kwa kutokuwa loyal lwa askari wetu?
Sisemi kwamba kuingia na silaha ndani ya mipaka ya nchi nyingine siyo kosa, ni kosa ila wakati mwingine tuangalie hao walioingia na silaha motive yao ilikuwa nini nini!

Ingekuwa kwa mfano tuseme, askari hao hao kwa bahati mbaya wameingia ndani ya nchi kama Kenya au Uganda, wangepigwa hayo mawe? Kenya au Uganda wasingepigwa isipokuwa wangepewa ushirikaiano na badala yake mhalifu aliyekuwa akiwakimbia askari angekamatwa

Mimi kama mtanzania maskini nashauri askari hao wasamehewe kwa onyo kali la kutokurudia kosa hilo kwenye utumishi wao wote, warudishwe kazini ikiwezekana. After all, wamalawi wenyewe hawatajua kama wamerudishwa kazini. Wawarudishe kimya kimya wala wasitutangazie hata sisi wanachi kuwa wamewarudisha.

Jamani tukumbuke kwenye issue ya juzi risasi zilipokuwa zinarindima barabarani kazi waliyofanya haikuwa ndogo, mpaka wengine wamepoteza maisha. Leo kwa bahati mbaya tu watu hao hao wame-tress pass tena kwa bahati mbaya tu na wakiwa na nia njema, tunawafukuza kazi?. Nashauri IGP awafikirie na hawa pia kama alivyowafikiria wale ambao walihangaika na tukio lile la ughaidi. Kwanza kile itendo tu cha kuwa wamefukuzwa kazi mpaka muda huu, kinawatosha kama adhabu inayolingana kabisa na kosa walilofanya, assuming wanarudishwa tena kazini hata leo
Watanzania maskini hawa hawana ajira, kwa bahati mbaya hawa watoto pengine wamejiunga na jeshi la Polisi hata miaka 10 wengine hawajafikisha, mambo mengi bado wanajifunza. Naomba rai positive ya watanzania iwe juu ya watoto hawa ili waweze kusamehewa na kurudishwa kazini

I have been in Malawi, nawajua attitude yao ilivyo kwetu
Wewe Makanyaga waweza kuwa ni mmoja wa Polisi waliofukuzwa au ni ndugu wa hao Polisi. Adhabu waliyopata kwa kufukuzwa kazi inastahili kabisa.

Hakuna excuse ya kungia Nchi jirani bila kufuata protocol za kimataifa kwa kisingizio cha kutafuta mhalifu. Hao maPolisi walikuwa wanatafuta rushwa tu kwa huyo wakiyedai ni mhalifu.

Wamepata wanachostahili
 
Hata siwajfahamu kabisa wote, na hata kwenye line ya ukoo wangu sina ndugu ambaye kwa sasa ni Polisi. Nilikuwa najaribu tu kuangalia hali halisi, assuming hakuna taarifa zingine za ziada tofauti na zile ambazo nilikuwa nimesikia hapo awali.

Polisi ninao jamaa tu na marafiki pamoja na wale niliosoma nao akiwemo role model wangu DCI Kamanda Camillus Wambura. Huyu tulisoma wote O-level na UDSM
 
Hawa viumbe waone hivyo hivyo siyo wa kuwaonea huruma kabisa. Aslimia 80 ya watu walio rumande na jela ni matokeo ya dhuluma za Polisi
 
Wamehamisha kwenye makaratasi kama wakitaka kujua nani mmiliki waje kuvua Kipande yetu au wafaye mazoezi ya kijeshi upande wetu ndio watajua hawajui
 
Asili ya tatizo ni mipaka ya kikoloni iliyofuata ufuko wa ziwa. Yale ambayo mwanzilishaji hapo juu aliona kwenye kompyuta si mipaka inayoonekana kwa satelaiti; ni mistari inayochorwa na kampuni ya google kwenye picha za satelaiti wanazotumia kama ramani.

Kuhusu historia ona makala ya wikipedia, utaona pale baada ya uhuru hadi 1967 hivi, serikali ya Tanganyika na Tanzania ilikubali mpaka wa kikoloni. Hali halisi changamoto ni kufikia mapatano bila kuingia katika mauaji ya watu.

Basi soma:
Kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba mpaka uwe katikati kufuatana na desturi za kimataifa.

Sababu ya mzozo ni utaratibu wa kikoloni. Wakati wa kuundwa kwa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani serikali za Uingereza na Ujerumani zilipatana kuhusu mipaka ya "eneo chini ya athira ya Ujerumani" ("German sphere of influence") kwa kutaja mpaka ulifuata ufuko wa Ziwa Nyasa.[1] Leo inajadiliwa baina ya wanasharia wa kimataifa kama maneno haya yalitaja mipaka halisi ya kiutawala au kama yalikuwa tu mapatano ya awali kuhusu "maeneo chini ya athira" ya nchi husika[2].

Baada ya mwaka 1919 Uingereza ilitawala Tanganyika pamoja na Malawi (Nyassaland), hivyo hakukuwa na shida.

Kabla ya uhuru, wakati wawakilishi wa TANU walichaguliwa tayari kuwa wabunge katika bunge la kikoloni (legislative council) na Julius Nyerere alikuwa waziri mkuu wa Tanganyika tangu 1960, mbunge Chifu Mhaiki alitaka serikali iangalie upya haki za Tanganyika kwa maji ya ziwa. Tarehe 12 Oktoba 1960 waziri mkuu Nyerere alijibu: "Hakuna shaka lolote kuhusu mpaka huu. Tunajua kwamba hakuna tone la maji kwenye Ziwa Nyasa ni mali ya Tanganyika kufuatana na mapatano haya. Hali halisi tungedai serikali jirani ibadilishe mipaka kwa manufaa ya Tanganyika." [3]. Chifu Mhaiki alirudia swali lake alipokuwa mbunge katika Bunge la Kitaifa baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1962 na safari hii waziri mkuu Rashidi Kawawa alijibu tena kwamba hakuna sehemu ya Ziwa Nyasa iliyokuwa ndani ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, kwamba Uingereza haikubadilisha mipaka hii na kwamba hata kama kuna hasara kwa Tanganyika serikali haiwezi kuanza majadiliano juu ya swali hili na Uingereza au serikali ya Nyasaland kabla ya uhuru wa nchi hii jirani[4].

Tarehe 3 Januari 1967 serikali ya Tanzania iliandika mara ya kwanza kwa serikali ya Malawi na kuifahamisha kwamba iliona mpaka baina ya nhci hizi ilifuata mstari wa kati wa Ziwa Nyasa. Malawi ilithibitisha kupokelewa kwa barua hii bila kuijibu rasmi. Hata hivyo rais Banda wa Malawi alikataa madai ya tanzania mbele ya bunge lake. Polisi ya Malawi ilijaribu kutawala wavuvi na feri za Tanzania ziwani. Mzozo huu ulisababisha risasi kufyatuliwa hadi kutulia mwaka 1968.

Hadi leo hakuna mapatano rasmi lakini nchi zote mbili zinaendelea bila kutumia nguvu. Hali halisi Malawi imeheshimu dai la Tanzania, haijasumbua tena wavuvi wala feri za jirani ndani ya robo ya kaskazini-mashariki ya ziwa.

Mzozo ulifufuka tena tangu mwaka 2012 baada ya Malawi kutoa vibali vya upelelezi wa gesi na mafuta chini ya ziwa, tendo linalopingwa na Tanzania.[5]

hivi na huko msumbiji nni hivi hivi au tz tu.

lake-624x510.jpg
 
Back
Top Bottom