Ziwa Nyasa limeporwa kikamilifu?

Huu ni mwanzo. Kama wazungu wamekubali kubadili huo mpaka kwa kumega nchi yetu huoni kuna siku tutapigwa marufuku kukanyaga ndani ya hilo ziwa?
Wabongo wanachukuliaga vitu rahisi sana,ila mwishoni wanabak kulia kumbe ni mambo ya kudharau. Heb waza mtoto anaezaliwa na kuona mipaka ikiwa hivyo. Baada ya miaka 50 halijaporwa? Nani atasema hakuona mipaka? Hapo mazingira yametengenezwa ya kizazi hata kingine kipate urahisi wa kulichukua kwa maneno tu.

Kwa sababu sisi tunaangalia na kuwaza leo hatuna habari na kesho ndio maana
 
Kama vipi tuwavamie,tujipime ubavu,maana wanajeshi wetu,wana vitambi balaa kwa kukosa mishemishe.
 
Binafsi hiki kitu kilinifikilisha Sana enzi za jk na kujaribu kufuatilia habari mbalimbali, mwishowe nilifika kwenye ukweli mchungu ya kwamba ziwa nyasa lote ni la Malawi ingawaje wagawaji wa mipaka kipindi hicho yaani wakoloni walifanya makosa ya ugawaji kwa kutozingatia baadhi ya kifungu. Kifungu hicho ni kwamba mipakani Kama Kuna ziwa au bahari basi mpaka lazima upite katikati ili kila nchi inufaike na maji. Kwa kuzingatia kifungu hicho wareno ambao walikuwa watawala wa msumbiji walikaa mezani na waingereza ambao walikuwa watawala wa Malawi na kukubaliana kuchora mpaka upya ndiyo maana utaona katika ziwa,msumbiji na Malawi mpaka umepita katikati. Lakini kipindi hayo yanafanyika Tanganyika na Malawi zote zilikuwa chini ya waingereza, kwahiyo hawakuona haja ya kubadili mpaka yote ni makoloni yao na hali hiyo iliendelea mpaka hizi nchi zikapata uhuru. Sasa Malawi hawataki kukaa mezani kugawana ziwa nyasa wanadai kwa mujibu wa mipaka ya mkoloni ziwa ni mali yao, ni kweli lakini mbona walikubali kufanya marekebisho enzi za wakoloni Kati yao na msumbiji? Hii inaonesha haki haikutendeka ndiyo maana Hilo liliwezekana ila halikufanyika enzi za muingereza kwa sababu hakuona haja ya kufanya hivyo nchi zote mbili ziko chini yake. Sasa tukae mezani tugawane ziwa,Malawi hawataki wanasema tufuate mpaka wa wakoloni. Tukumbuke mgogoro huu upo tangu enzi za Nyerere na Kamuzu Banda
 
Sasa kwanini hao maaskari wasitoe taarifa kwa wenye mamlaka?
 
Tunatakiwa kuwa na msimamo mmoja kuwatangazia walimwengu wote juu ya mpaka wa ziwa nyasa, kwasababu kadiri sik uzinavyoenda malawi wanaiaminisha dunia kuwa wao wanamiliki hadi upande wetu, wakati sisi pengine hatujitangazi kuwa tunamiliki hadi katikati ya ziwa, jambo ambalo baadaye kikinuka malawi ambao watakuwa wamejitangaza kwa wengi watapata uungwaji mkono toka kwa wengi.
 
 
Ni busara kufanya tafiti na angalau hata kujua chanzo cha huo mzozo, kabla ya kuandika kitu usichokielewa kwa ufasaha. Ikumbukwe mzozo
wa mpaka katika hilo ziwa, ulikuwa toka tunapata uhuru.Aliyekuwa raisi wa kwanza wa taifa hili, marehemu Julius K. Nyerere alizozana na marehemu raisi Kamuzu wa Malawi na mpaka wakaitana majina.Na viongozi wengine waliofuata waliingia katika majadiliano kuhusu mpaka
bila mafanikio na ilifikia wakati likapelekwa kwa wasuluhishi wa kimataifa wakati wa uongozi wa raisi Jakaya Kikwete ila mrejesho sikufanikiwa kuupata.
 
Nani kakuambia serikali yetu ni maskini was kifedha??? Hii ni maskini wa akili
 
Heligoland treat
Heligoland Treaty ilikuwa 1890 na sio 1870 kama ulivyosema. Hii no katika kuweka mambo sawa. Ndo raha ya Jamii forum
 
Halafu ukiwa hapo hotelini kwa Mwamunyange, tunatumiwa sms kwenye simu zinasema Welcome to Malawi.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Huku hayo mambo ya mipaka hata haituhusu, Waswahili tuna mashamba tunalima Kitwika/Kyungu na Wangonde wanavuka kuja kulima Kabanga karanga na mahindi, hata hatuulizani tunavyo vuka mto songwe.
 
Mkuu achana na ramani za google, sijui na maneno ya kwenye kanga, naamini wamalawi bado wanaupenda ugali, hawawezi kuchezea sharubu za simba kizembe namna hiyo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…