Zlatan Ibrahimovic ajiachia mtaani na Ferrari yake ya Sh BILIONI 1.2

Zlatan Ibrahimovic ajiachia mtaani na Ferrari yake ya Sh BILIONI 1.2

Mifano yako ni irrelevant, huyu ng'ombe aliyetajwa kwenye mfano wako ni sawa na hao ng'ombe wa Wamasai?
Branding branding nasisitiza tena branding, Ferrari is a big brand which means hata huyo ng'ombe tajwa in a way 'alitengenezwa' kuwa brand.
View attachment 2117045

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa wewe umejibu nini na mimi tangia mwanzo nasema nini ?

What is Branding ? Utagundua kwamba branding ni kui-place bidhaa fulani kwenye akili ya wanunuzi / walaji ili kukidhi mahitaji yao..., pia ndio maana kuna market segmentation Ferrari wanabrand bidhaa zao kutokana na watu fulani au status fulani..., kwa macho ya celebrity (walengwa) brand hio hio huenda isifanye kazi kwa Mmasai..., Sababu kwa macho ya mmasai yeye value kwake ni tofauti...., Status / Chakula / Utajiri vyote vinapatikana kwenye ng'ombe....

Pili sio kila mtu anakuwa swayed na marketing (in essence wewe unaweza kuambiwa kwenye adverts kwamba Juice ya kwenye Pakti processed ni bora na ndio inafaa zaidi) ila uhalisia ukawa ya kukamua mwenyewe ikawa bora kwa afya ingawa ya kukamua ni bure kwa bibi yako na ya pakti ni elfu kadhaa....
 
Ninajua vizuri ulipoanzia,rejea kwenye jibu lako la kwanza kabisa....mleta Uzi kaongelea gari la thamani ukaanza kubisha thamani kwenye macho ya Nani,
Mleta uzi kaulizia ni kitu gani cha thamani ulishawahi kununua..., Likaulizwa swali Thamani kwa Macho ya Nani, Hilo ni Swali sio Kubisha Jibu lake ndio lingeweka mipaka, sababu thamani, gharama na bei sio necessarily kitu kilekile....
Kuna vitu Ni vya thamani tu haijalishi viko jangwani,umasaini au down town Washington DC......
Hapana sio kweli kila kitu kina thamani kutokona na matumizi / mahitaji ya wakati husika, na tamaduni za sehemu husika na upatikanaji wake mfano ukiwa na Ferrari Jangwani katikati ya mchanga au ngamia na Chupa ya Maji ya Kilimanjaro kipi kina thamani zaidi ?
Tuje na tabia ya ku appreciate vtu vya watu na sio kubeza jamani.
Nani Kabeza !!!, Tena huenda mimi ndio nina-appreciate zaidi matakwa ya mtu husika na ninajua kabisa kwangu mimi Smartphone huenda ikawa na thamani zaidi ingawa mtu anayetuma mpesa pekee huko kijijini akaona nokia kitochi kwake ina thamani zaidi kutokana na kukaa na chaji na simplicity of usage (kwake smartphone imejaa vitu visivyo na manufaa kwake....)

To each his/her own....
 
haya wapenda tu chuma mwambieni jamaa yenu aongeze kengine kanauzwa bilioni 8.7 ila kametumika kama km 1000 na ushee
Screenshot_20220212-140731.jpg
 
Ukifuatilia ninachojibu huenda ukaelewa..., Mmasai unampelekea Ferrari ili atumie fuel gani (maziwa ?) au aendeshe kwenye barabara zipi ? na Spare zitoke wapi ?

Kwa mfano mwingine labda nikuulize ni kipi chenye thamani Jangwani ? , Ngamia au Ferrari ?
Kumbe mihogo inaharibu ubongo... kwani kuna Tajiri anaeishi jagwani. Jagwani ngamia ni muhimu ila thamani itabaki kwa Ferrari

Unamfano wa kijinga sana.. pia kadabra haendeshi hio gari jangwani
 
Mleta uzi kaulizia ni kitu gani cha thamani ulishawahi kununua..., Likaulizwa swali Thamani kwa Macho ya Nani, Hilo ni Swali sio Kubisha Jibu lake ndio lingeweka mipaka, sababu thamani, gharama na bei sio necessarily kitu kilekile....

Hapana sio kweli kila kitu kina thamani kutokona na matumizi / mahitaji ya wakati husika, na tamaduni za sehemu husika na upatikanaji wake mfano ukiwa na Ferrari Jangwani katikati ya mchanga au ngamia na Chupa ya Maji ya Kilimanjaro kipi kina thamani zaidi ?

Nani Kabeza !!!, Tena huenda mimi ndio nina-appreciate zaidi matakwa ya mtu husika na ninajua kabisa kwangu mimi Smartphone huenda ikawa na thamani zaidi ingawa mtu anayetuma mpesa pekee huko kijijini akaona nokia kitochi kwake ina thamani zaidi kutokana na kukaa na chaji na simplicity of usage (kwake smartphone imejaa vitu visivyo na manufaa kwake....)

To each his/her own....
Sawa,nimekuelewa,mchana mwema......by the way unajua kutetea hoja zako Sana,thumbs up!
 
Hio Bilioni nani kasema Value yake ni kama Ndama Dume ?

Je ni kweli Value ya Karatasi lililoandikwa Dollar na Sifuri kadhaa linashinda value ya Kiumbe hai kinachoweza kuleta Ndama kadhaa na kutoa maziwa...

What's the Really Value of a Product ?

Mwisho wa siku utagundua Marketing na Promotion na Pia Product Placement (Exclusivity) vinaweza kupelekea an inferior product kuonekana ina value kuliko uhalisia..., ila when push comes to shove kwenye scarcity na sina excess (disposable income) utaona kwamba slice ya mkate na maji inaweza ikawa na value kuliko jiwe linaloitwa (diamond) ?

Huenda tu tatizo la Mmasai ni kwamba hajui marketing...
Aisee kwa hii "comment" we sio TABULARASA kabisa, toa hio profile foto hapo haraka sana.
 
Mleta uzi kaulizia ni kitu gani cha thamani ulishawahi kununua..., Likaulizwa swali Thamani kwa Macho ya Nani, Hilo ni Swali sio Kubisha Jibu lake ndio lingeweka mipaka, sababu thamani, gharama na bei sio necessarily kitu kilekile....

Hapana sio kweli kila kitu kina thamani kutokona na matumizi / mahitaji ya wakati husika, na tamaduni za sehemu husika na upatikanaji wake mfano ukiwa na Ferrari Jangwani katikati ya mchanga au ngamia na Chupa ya Maji ya Kilimanjaro kipi kina thamani zaidi ?

Nani Kabeza !!!, Tena huenda mimi ndio nina-appreciate zaidi matakwa ya mtu husika na ninajua kabisa kwangu mimi Smartphone huenda ikawa na thamani zaidi ingawa mtu anayetuma mpesa pekee huko kijijini akaona nokia kitochi kwake ina thamani zaidi kutokana na kukaa na chaji na simplicity of usage (kwake smartphone imejaa vitu visivyo na manufaa kwake....)

To each his/her own....
Kwahio hizo nokia toch huko vijijini zinauzwa million ngap?
 
Kumbe mihogo inaharibu ubongo... kwani kuna Tajiri anaeishi jagwani.
Nani anaishi Jangwani ? Unadhani Zlatan akienda Jangwani atachukua Ferrari ?
Jagwani ngamia ni muhimu ila thamani itabaki kwa Ferrari
Nini maana ya Thamani ?

in regard that something is held to deserve; the importance, worth, or usefulness of something...., Unadhani kama mnataka kuvuka Jangwani alafu kuna Ngamia mmoja, Ngamia huyo atanunuliwa kiasi gani ?, Kumbuka hizi bei ni man made kutokana na Marketing prowess..., ila sio necessarily uhalisia... Inategemea unanunua nini kwa ajili ya nini (ndio maana thamani kwa individual au tamaduni tofauti ni subjective...
Unamfano wa kijinga sana.. pia kadabra haendeshi hio gari jangwani
Nadhani takuwa nimekujibu Thamani na Bei sio Necessarily kitu kile kile.....,
 
Kwahio hizo nokia toch huko vijijini zinauzwa million ngap?
Tatizo unadhani thamani inapimwa kwa bei pekee, au thamani na bei ni kitu kilekile..... Hivi nikiwa nina Almasi zangu mfukoni msituni na mwenye mtego wa kutega Sungura ni kipi chenye thamani hapo ?

Naona kama najirudia rudia ingawa haya maswali yako yote yashajibiwa....

Monetary Value / Prices - inategemea na Marketing...., True Value ya Product inategemea na Usefulness ya Muhusika.... Kitimoto huenda kikawa ni asset kwa mmoja ila kwa mwingine laana....
 
Labda Condom ya Rough Rider niachane na Salama au Dume
Naam kama hio iliweza kunusuru maisha yako (which is priceless) arguably hio itakuwa ni zawadi ya thamani zaidi uliyoshawai kuinunua hata kama kwenye Portfolio yako unamiliki visiwa....
 
Nani anaishi Jangwani ? Unadhani Zlatan akienda Jangwani atachukua Ferrari ?

Nini maana ya Thamani ?

in regard that something is held to deserve; the importance, worth, or usefulness of something...., Unadhani kama mnataka kuvuka Jangwani alafu kuna Ngamia mmoja, Ngamia huyo atanunuliwa kiasi gani ?, Kumbuka hizi bei ni man made kutokana na Marketing prowess..., ila sio necessarily uhalisia... Inategemea unanunua nini kwa ajili ya nini (ndio maana thamani kwa individual au tumaduni tofauti ni subjective...

Nadhani takuwa nimekujibu Thamani na Bei sio Necessarily kitu kile kile.....,
Kwani wewe jamaa ni mgogo.. kinachofanya kitu kiwe na thamani ni jumla na material,brand na historia... kwamwe ngamia au ngombe uwezi kuwaweka ligi moja

Sio kwa uhitaji tu hata kwa upatikaji[emoji3] ni vitu viwili tofauti ngami,boya la kuogelea,sijui maji jangwani,chumvi vyote hivyo vinaumuhimu wake.

Point yako ni nzuri ila imekaa kiumaskini maskini kwamba passo inanifikisha nitakapo Bugatti chiron ya nini?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Kwani wewe jamaa ni mgogo.. kinachofanya kitu kiwe na thamani ni jumla na material,brand na historia...
Kwahio leo ugundue dawa ya kurefusha maisha ambayo materials zake ni maji na sukari katika vipimo fulani exact; hio dawa yako itakuwa na bei kiasi gani ?

Utaona hapo bei itakuwa kubwa sana (kitu ambacho wewe unahusisha na thamani) lakini hapo hio dawa yako itakuwa haina historia raw materials gharama itakuwa ndogo wala utakuwa haujaifanyia branding..... Kwahio tofauti ni nini ?

Thamani inayotokana na usefulness (itaendelea kubaki vilevile no matter nani anasema nini) Oxygen ni muhimu kwa binadhamu ingawa huinunui..., Bila Jua Dunia itakufa (tunajua thamani ya jua katika Solar System) ila hakuna Tozo yoyote ya kupata faida za jua.... (halipo monitized)
kwamwe ngamia au ngombe uwezi kuwaweka ligi moja
Ligi ya nini ? Ya Bei sawa kutokatana na mahitaji ya wakati husika, au marketing inayoleteleza kitu kinachoitwa perceived value..., Kuna watu wanalipa Mabilioni ya Pesa kushikwa mkono na mganga fulani wakiamini kwamba mkono huo una baraka (lakini ukweli ni kwamba huenda jamaa anawachota akili zao na huo mkono kwa kushikwa na wengi unakupatia magonjwa tu)
Sio kwa uhitaji tu hata kwa upatikaji[emoji3] ni vitu viwili tofauti ngami,boya la kuogelea,sijui maji jangwani,chumvi vyote hivyo vinaumuhimu wake.

Point yako ni nzuri ila imekaa kiumaskini maskini kwamba passo inanifikisha nitakapo Bugatti chiron ya nini?
Ukiniambia nichague kati ya hayo mawili hata kama sioni faida ya lolote lile tachagua lenye bei (sababu naweza kuuza hio Bugatti nikanunua passo za kutosha na chenji kubaki...., au kama kwangu status ni ya muhimu tachagua gari ambalo ni wachache wanalo..., ila ukisema unipe nitumie tu na siwezi kuuza ila mimi ndio nafanyia maintenance huenda Bugatti likanitia umasikini, moja gharama za uendeshaji zitakuwa kubwa na huenda kama mimi ni mtu private ile attention ikasababisha nisifanye mambo yangu..., hivyo kwangu Bugatti isiwe na thamani
 
Thamani kwa macho ya nani ?

Hayo machumachuma kwa macho ya mmasai yanaweza kuwa tu kama mtambo wa kuharibu mazingira na kutoboa mifuko kwa gharama...., ila Ng'ombe aliyeshiba na mnono anaweza kulala kwa tabasamu kubwa na kicheko kwa muda wa mwezi mzima
punguza wivu
 
Back
Top Bottom