Zlatan Ibrahimovic ajiachia mtaani na Ferrari yake ya Sh BILIONI 1.2

Jamaa unamifano ya kimaskini sana... ondoa fikra hasi kichwani, mifano yako sio halisi

Ila we jamaa unaakili nyingi sana[emoji3] tatizo unafikiria hadi na ujinga mifano yako ni kama hiii.

Umefungiwa kwenye jumba la kifahari lenye midollar na MAroserose,bugati ma vipper nakila kitu ila hakuna chakula na mwingine hivyo hivyo kwenye nyumba ya nyasi na msosi wa wa kufa mtu, ni yupi kati ya hao wawili anamiliki vitu vya thamani[emoji38]

Huo ujinga ni sawa na ule wa jamaa mwenye red diamond mfukoni na mwenye mtengo wa sungura msituni in real world hizo myths tu
 
thamani yake haifikii Scania mbili za Mtanzania Bakhresa, kwa hiyo kawaida nilijua Till kumbe Bill.. Yani Milioni 1200 tu ambazo wananchi wa kawaida wanakopa benk wanajengea maghorofa mjini.
 
Unajua kujenga hoja kwenye ujinga ilo ni tatizo... dawa ya kuongeza maisha tena kwani tumejua tukifa tunaenda wapi?

Jamaa unafikiri sana hongera
 
Sasa Zlatan ng'ombe wa nn? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hana kazi nae..., maana itakuwa ni uchafu kwake..., kama vile Tyson alivyokuwa anafuga Tiger kwa mwingine ni kukaribisha hatari kwenye maisha yake...., Na mmasai kununua hili dude kwake ni useless..., na kwake muhimu zaidi ni kata mbuga za kuweza kukatia mbuga..., Ferrari haiwezi pita hizi zinapopita....

 
Kaka umesomea nini maana point nzuri sana hii

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu wamevamia thd hoja zao zinatakiwa zikawekwe kwenye uzi wa kimasikhara ila hizi nondo za huyu jamaa keysersoze[emoji119]
 
Boxer za 10,000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa unamifano ya kimaskini sana... ondoa fikra hasi kichwani, mifano yako sio halisi
Na hapo nadhani tunafungua pandoras box nyingine ya umasikini ni nini (siongelei ufukara yaani kukosa hadi basic needs bali umasikini) at what point tuna cut off baina ya utajiri na umasikini na je umasikini wa fikra unaendana sawa na umasikini wa kipato (hapo nachukulia umasikini kama ni lack of enough of something according to ones desires).... Nadhani pitia hapa chini sababu watu tumekuwa tukichukulia uhusiano kati ya uzembe / uchapakazi na umasikini / utajiri wrongly

 
Mkuu kwanini unahangaika kutafuta maana halisi ya thamani ya hivyo vitu kwa watu wenye pesa? Mifano yako sio mibaya ila kadabra anaweza kuish kimasai, ila masai hawezi kuish kama kadabra. Ina logic nzuri ila sijaona hata sehemu moja ulioongelea cost of production. Simu moja Warren Buffet alisema anaeruhusiwa kusema money is not everything ni yule mwenye nazo kama huna hela hizo kauli zinakuwa hazikufit. Anyways mini binafsi mtu kama wewe naweza nikamshinda logically throws tumeonana physically sababu watu kama wewe wanasema hivyo ila ukikutana nae unakuta Yupo na simu flagship, kavaa Gucci, sasa huwa napenda tuanzie kwenye physical appearance yake lakin hapa hatutakuweza kamwe. Waache kina bill Waish flashy lifestyle wana pesa na waache wamasai wacheze na kinyesi cha ngombe wana ngombe, hata wewe ukiambiwa uchague wapi ni wapi ni dhahiri utachagua upande wa bill, mambo ya kunuka mavi ya mbuzi utawaachia wamasai.
 
Mkuu kwanini unahangaika kutafuta maana halisi ya thamani ya hivyo vitu kwa watu wenye pesa?
Nadhani hapa naendelea kujirudia rudia ila ukinisoma tangia mwanzo sidhani kama hata ungeleta hii comment; Pesa ni nini ? Pesa haina intrinsic value ;Yaani hio pesa tunasema ni pesa ya value hio sababu kama community / wanadamu tumekubali kwamba hio ndio value.., leo hii ukienda Ukraine au Tanzania vikitokea vita huenda punje mbili za karanga zikawa na value kwa wakati husika kulika karatasi lenye maneno 1 na sifuri nne / au ukiwa kwenye baridi huenda hayo makaratasi yakawa na value ya kuwashia moto
Mifano yako sio mibaya ila kadabra anaweza kuish kimasai, ila masai hawezi kuish kama kadabra.
Kwahio unasema hakuna Mmasai mwenye vitu ambavyo vinaweza vikawekwa kwa thamani ya sasa kama Ibrahimović; Unajua wamasai baadhi wana ardhi kiasi gani na umeangalia porfolio ya Ibra na kuona ana madeni kiasi gani na hizo nyingine amechukua kama lease kiasi gani na huenda hao Ferrari wanampa subsidy kiasi gani ili aweze kuwatangazia product ? Na hapa issue sio fulani ana ngapi za kuweza kununua nini bali ni nani anathamini nini ili aweze kukichukua na akishachukua ni vipi kitasaidia maisha yake ya kila siku..., Ukienda kwa Mmasai huenda ukimpa hili gari kwake atali value kama pesa (yaani tauza hili lichuma linalokula mafuta ili ninunue ng'ombe kiasi kadhaa na kamwe hawezi kuuza ng'ombe ili anunue hili li petrol grabber) na kwakwe it makes sense sababu moja linampa maziwa jingine linakula pesa zake wala haliwezi kukata mbuga kwenye mazingira yake...
Ina logic nzuri ila sijaona hata sehemu moja ulioongelea cost of production.
Ukiongelea cost of production unadhani ni nani anatumia pesa / muda / rasilimali nyingi..., yule mangi anayeshona kiatu kimoja kwa wiki nzima na kujichoma na sindano na kukusanya ngozi na kuanika juani au Viatu ambavyo vinakuwa mass produced na mashine na kwa kutumia cheap labor ?; Magari siku hizi mengi tangia Ford alipoweka Mass Production kwenye mainstream production yake per unit imepungua sana ila ndio hivyo Ferrari sababu ya Product Placement / Promotion / Brand na Exclusivity wameamua kufanya magari yao kuwa luxurious na kwa wachache (huo ni uamuzi and has nothing to do na cost of production)
Simu moja Warren Buffet alisema anaeruhusiwa kusema money is not everything ni yule mwenye nazo kama huna hela hizo kauli zinakuwa hazikufit.
Buffet ana haki ya kusema anachosema lakini mtu anayeongelea pesa kama pesa hajaangalia the complete equation (pesa ni kiwezeshaji) na uzuri wa Pesa sababu ya liquidity ni kwamba ukiwa na elfu moja sio kwamba una elfu moja bali una kitu chochote ambacho kwa wakati huo jamii imekubaliana kwamba kwa elfu moja utakipata...; ila linapokuja suala la not everything kuna vitu hata ukiwa na hizo pesa hauvipati; mfano labda kutokana na kauli zako na tabia zako unaweza ukakosa madada mtaani ingawa wengine bure au kwa pesa theluthi ya na ya kwako wakapata...

Point yangu ni kwamba maisha / life sio black or white kuna a lot of grey areas...
Naam huenda mimi nina kila simu mpya ikitoka.., huenda nikinunua perfume mwingine akinunua ofisini au mtaani ninatupa yangu..., huenda nikisifiwa nimependeza mimi ndio usiku ninalala usingizi wa pono; huenda kwangu mimi wapambe au machawa ndio marafiki zangu..., Au huenda mtu kama Diamond ku-maintan status ndio ataendelea kuuza vitu (sababu akionekana amefulia na mashabiki wanamkimbia)...; LAKINI kuwa kwangu VAIN au Materialistic hakuniondolei kufahamu kwamba watu wapo tofauti na self fulfilment ni tofauti kwa watu tofauti...

Waache kina bill Waish flashy lifestyle wana pesa na waache wamasai wacheze na kinyesi cha ngombe wana ngombe, hata wewe ukiambiwa uchague wapi ni wapi ni dhahiri utachagua upande wa bill, mambo ya kunuka mavi ya mbuzi utawaachia wamasai.
Nadhani kusema wamasai wananuka mavi tunakosea..., , mwisho wa siku maisha ya watu ni peace of mind..., Hivi unajua kuna Mfalme Uingereza alikataa Ufalme ili aweze kwenda kuoa mke USA ambaye ilikuwa against sheria za Ufalme ?, Hivi unajua watu kama kina Mama Theresa waliamua kwenda kuishi na masikini sababu kwao self fulfilement ni kusaidia Masikini ?; Hivi unadhani mtu akishapata Pesa ndio safari imekwisha au baada ya hapo anaanza kuwaza ni jinsi gani anaweza ku make change..., Na unadhani furaha ya Ibra ni Ferrari ngapi anazo au huenda ni Records ngapi anaweza kupata ? Umemuongelea Baffet hivi unajua gari analomiliki ?
 
We jamaa una talent ya ubish na ina backup kabisa sababu you know stuffs. Ila mwanangu usibeze hela mfano Dar ni kali sana kama miundo mbinu yako haijakaa sawa na joto lake ni linaumiza sana...Anyways other things being constant, we gon grind till our last bit mpaka our duffle bags zijae every president that ever died...as long as we are living high we alright...
 
Mkuu siwezi kubeza pesa, sababu pesa ndio kiwezeshi cha mambo mengi sana, hata Mtu anayependa watu wapate chakula (Mfano Mama Theresa) ni rahisi kwake kufungua wallet na kutoa pesa magunia ya chakula yakaja; kwahio hio pesa inaaminiwa na hao wote anayetoa na anayechukua, ingawa thamani hio ni sababu ya Imani ya hao watu (thamani hii inaweza kubadilika) lakini chakula ni chakula hata pesa ikiacha kuaminika watu watakula chakula..., ila ukitaka kupeleka mtoto shule ni rahisi kupeleka pesa kuliko gunia zako za chakula sababu mwalimu huenda hataki chakula wakati huo bali kununua Kanzu... Kwahio when it comes to liquidity Cash is KING... Pia hapo linakuja suala la need / huitaji, sababu mazao hayo yakiwa mengi na yanaoza / expiry date huenda yakaishia kulishia mifugo....

Sasa kumbuka tukiongelea kitu kama Ferrari hio sio pesa (ingawa unaweza kuuza ukapata pesa) ila ukiwa nalo limekwama sehemu kama huko kwa wamasai sababu limekosa mafuta usishangae mtu anayeuza majani ya ng'ombe akapata mteja kabla ya wewe na Ferrari yako; na hata mtu ukimpa bure huenda insurance yake na mafuta ikamdumbukiza kwenye umasikini (ukizingatia mabinti wa eneo hilo huenda kwao wanaona ujanja ni nani mwenye ng'ombe nyingi) yaani mahari kuliko hilo ligari wanaweza kusema fulani amechanganyikiwa...

Kwahio hapa utaona kwamba it DEPENDS..., na ndio maana mwanzo kabisa nilimuuliza mleta uzi Thamani kwa Macho ya Nani ? Nikimaanisha watu, nyakati na mazingira vinatofautiana, la karne za hivi karibuni thamani inaendana na promotion / marketing iwapo kitu ni cha matamanio ila linapokuaja suala la uhitaji hapo ndio utaona true value ya kitu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…