Zoezi la kumwaga sumu ya kuua nzige kuendelea kesho Kilimanjaro, rubani aliyetelekeza ndege na kurudi Kenya kufuatiliwa!

Nzige na Rubani wote wanatokea Kenya.
 
Serikali ina uwezo wa kununua ndege na kuzipaki pale JNIA bila kutumika lakini haina uwezo wa kumiliki helkopta moja kwa ajili ya majanga kama ya nzige ambao ndani ya muda mfupi wanaweza kuliingiza Taifa katika Janga kubwa la Njaa, sasa sijui watu wataenda kula zile dremliner pale airport?
 
Hakuna mbinu mbadala ? Kwani mababu zetu walikabilianaje na nzige enzi hizo?
 
Sisi ni wabovu sana kwenye ku sustain miradi, tunachoweza ni procurement tu, tukishapata 10% tuna dump mitambo na kujipanga kuhujumu mradi tulioanzisha wenyewe kwa fedha zetu wenyewe
Uko sahihi! Nimepita stend ya Msamvu, Morogoro...taa za kwenye dali kwenye vizimba vya mawakala wa mabasi inaning'inia kwa kushikiliwa na waya! Pia kuna kasoro nyingine ambazo inaonekana bajeti ya ukarabati ama haijatengwa ama imetengwa na inatafunwa na wasiotakia mema miradi yetu hii!
 
Ndivyo tulivyo, ni watu wa ajabu sana
 
taa za kwenye dali kwenye vizimba vya mawakala wa mabasi inaning'inia kwa kushikiliwa na waya!
Hapo ujue hizo taa zilinunuliwa sub-standard, ukienda maeneo ya Mission utaona taa zilizowekwa na wazungu miaka hiyo bado zinafanya kazi mpaka leo, lakini kwenye hii miradi taa zinadumu mwaka zinakufa
 
..inakuwaje kama NCHI HURU hatuna ndege za kupambana na majanga kama haya?

..kuna wakati kulitokea ajali ya moto maeneo ya Ngara[kituo cha magari ya mizigo] gari ya zimamoto ilitoka Rwanda.

..Je, ni busara kuwa na ma-bondadier na ma-dreamliner huku tukiwa hatuna ndege na vifaa vya kupambana na majanga pamoja na ajali?

NB:

..pia msisahau kwamba Wizara ya kilimo imekuwa ikigawiwa 6% ya bajeti wakati sekta ya kilimo ndiko waliko waTz zaidi ya 70%.
 

..inawezekana pia rubani kaamua kuacha kazi, au amepatwa na matatizo.

..nadhani waTz tunapaswa kupunguza malalamiko ya kila wakati kuwa tuhahujumiwa.
 
Dili tu za watu. Ukienda hapo Kilombero sugar ndege za kunyunyiza dawa zipo karibu kila week.
Ila kama nazo hukodiwa kutoka Kenya, basi kutakua na shida ya kimfumo.

Tuombeane maendeleo.
Sasa kama zipo hapa kwetu kwanini wakakodi huko? Mbona nzige wenyewe waliwahenyesha sana Kenya? Mambo haya halafu sie Africa vichwani sijui mnanini!
 
Ndege moja iliharibika ukauzwa laki 5 kama screpa
 
Msije kuwa mlimkopa maana nyie CCM hamuaminiki!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…