Zoezi la kumwaga sumu ya kuua nzige kuendelea kesho Kilimanjaro, rubani aliyetelekeza ndege na kurudi Kenya kufuatiliwa!

Zoezi la kumwaga sumu ya kuua nzige kuendelea kesho Kilimanjaro, rubani aliyetelekeza ndege na kurudi Kenya kufuatiliwa!

Waziri wa kilimo Prof Mkenda ameagiza zoezi la kuua nzige waliovamia mkoa wa Kilimanjaro liendelee kesho baada ya leo kusimama kwa sababu pilot wa ndege ya kumwaga sumu aliiacha ndege na kurejea Kenya.

Prof Mkenda amesema atamfuatilia pilot huyo kupitia mamlaka zake za juu na kwamba kesho itatumika ndege ya Shirika la Chakula Duniani FAO.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Nzige na Rubani wote wanatokea Kenya.
 
Serikali ina uwezo wa kununua ndege na kuzipaki pale JNIA bila kutumika lakini haina uwezo wa kumiliki helkopta moja kwa ajili ya majanga kama ya nzige ambao ndani ya muda mfupi wanaweza kuliingiza Taifa katika Janga kubwa la Njaa, sasa sijui watu wataenda kula zile dremliner pale airport?
 
Hakuna mbinu mbadala ? Kwani mababu zetu walikabilianaje na nzige enzi hizo?
 
Sisi ni wabovu sana kwenye ku sustain miradi, tunachoweza ni procurement tu, tukishapata 10% tuna dump mitambo na kujipanga kuhujumu mradi tulioanzisha wenyewe kwa fedha zetu wenyewe
Uko sahihi! Nimepita stend ya Msamvu, Morogoro...taa za kwenye dali kwenye vizimba vya mawakala wa mabasi inaning'inia kwa kushikiliwa na waya! Pia kuna kasoro nyingine ambazo inaonekana bajeti ya ukarabati ama haijatengwa ama imetengwa na inatafunwa na wasiotakia mema miradi yetu hii!
 
Uko sahihi! Nimepita stend ya Msamvu, Morogoro...taa za kwenye dali kwenye vizimba vya mawakala wa mabasi inaning'inia kwa kushikiliwa na waya! Pia kuna kasoro nyingine ambazo inaonekana bajeti ya ukarabati ama haijatengwa ama imetengwa na inatafunwa na wasiotakia mema miradi yetu hii!
Ndivyo tulivyo, ni watu wa ajabu sana
 
taa za kwenye dali kwenye vizimba vya mawakala wa mabasi inaning'inia kwa kushikiliwa na waya!
Hapo ujue hizo taa zilinunuliwa sub-standard, ukienda maeneo ya Mission utaona taa zilizowekwa na wazungu miaka hiyo bado zinafanya kazi mpaka leo, lakini kwenye hii miradi taa zinadumu mwaka zinakufa
 
..inakuwaje kama NCHI HURU hatuna ndege za kupambana na majanga kama haya?

..kuna wakati kulitokea ajali ya moto maeneo ya Ngara[kituo cha magari ya mizigo] gari ya zimamoto ilitoka Rwanda.

..Je, ni busara kuwa na ma-bondadier na ma-dreamliner huku tukiwa hatuna ndege na vifaa vya kupambana na majanga pamoja na ajali?

NB:

..pia msisahau kwamba Wizara ya kilimo imekuwa ikigawiwa 6% ya bajeti wakati sekta ya kilimo ndiko waliko waTz zaidi ya 70%.
 
No kuna kama jointventure au tuseme mradi wa pamoja kukabiliana na janga la ndege inaendeshwa kwa pamoja baina ya Kenya na Tanzania....baada ya kunyunyiza siku moja rubani kapaki ndege karudi kenya bila taarifa wala sababu.
Ni kama Kuna hujuma flan zoezi hili lisifanikiwe

..inawezekana pia rubani kaamua kuacha kazi, au amepatwa na matatizo.

..nadhani waTz tunapaswa kupunguza malalamiko ya kila wakati kuwa tuhahujumiwa.
 
Dili tu za watu. Ukienda hapo Kilombero sugar ndege za kunyunyiza dawa zipo karibu kila week.
Ila kama nazo hukodiwa kutoka Kenya, basi kutakua na shida ya kimfumo.

Tuombeane maendeleo.
Sasa kama zipo hapa kwetu kwanini wakakodi huko? Mbona nzige wenyewe waliwahenyesha sana Kenya? Mambo haya halafu sie Africa vichwani sijui mnanini!
 
Sawa kabisa. Hizo ndege zilikuwa za Serikali zikimilikiwa na Wizara ya Kilimo zikitumiwa na Kituo chake cha Bird Control kilichokuwa kule Arusha ambacho nacho kimekufa. Shirika la nzige lilikuwa linathibiti hao panzi, Kituo cha Bird Control kilikuwa kinathibiti ndege waharibifu na viwavi jeshi kwa hiyo Taasisi hizi mbili zilikuwa zinashirikiana sana mpaka Shirika likajenga Ofisi zake Arusha karibu na Kituo.
Ndege moja iliharibika ukauzwa laki 5 kama screpa
 
Msije kuwa mlimkopa maana nyie CCM hamuaminiki!!
 
Back
Top Bottom