LGE2024 Zoezi la Uchukuaji na Urejeshaji wa fomu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mbwembwe linaloendelea nchini nzima ni ishara ya uvunjifu wa amani

LGE2024 Zoezi la Uchukuaji na Urejeshaji wa fomu za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mbwembwe linaloendelea nchini nzima ni ishara ya uvunjifu wa amani

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Sioni sababu yoyote ya watu kukusanyana kwa ajili ya zoezi la kwenda kuchukua fomu tu ya kugombea, kwangu naona ni ishara kuwa wanaofanya hivi lengo lao wakishindwa kwenye uchaguzi ionekane wameibiwa kura, period.

Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za 2024, mwongozo wa uchaguzi na mwongozo wa elimu ya mpiga kura vimeeleza vizuri tu namna uchaguzi utakavyokuwa, sasa kuna watu ambao wanapenda kuingia mgogoro na vyombo vya usalama wameanzisha mkakati kwenda kuchukua fomu kwa mbwembwe wakiwa na mabodaboda na vurugu za kila aina.

Kanuni tumezisoma na kuzielewa wazi kabisa, we unaenda kuchukua fomu umejaza wavuta bangi tu ambao hawajajiandikisha halafu baadae uje useme umeibiwa kura.

Mkakati wenu Chadema umeshabainika.
 
Back
Top Bottom