KERO Zoezi la uhakiki wa taarifa NMB

KERO Zoezi la uhakiki wa taarifa NMB

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

MambuluS

New Member
Joined
Nov 10, 2021
Posts
3
Reaction score
25
Zoezi la uhakiki wa taarifa bank ya NMB ni kero kwakweli, foleni ni ndefu kila branch, watendaji hawajipanga, inchukua hadi dk 20 kwa mtu mmoja kuhudumiwa na wahudumu kwa kila branch ni mmoja.

Mara waseme mtandao unasumbua kwahyo mshine inachelewa.

Nimezunguka NMB branch zote Dodoma, msururu wa foleni ni mrefu, uwe umekula umeshiba n uwe n nguvu za kusimama ili kusibiri foleni yako ifike.

Wajipange upya na waongeze muda wa zoezi.
 
hama , toka kwenye usumbufu huo
 
Tatizo la wabongo ni deadline 🤣🤣🤣🤣🤣🤣mwasubiri siku ziishe ndio mwende kuhuisha taarifa zenu.
 
Tatizo la wabongo ni deadline 🤣🤣🤣🤣🤣🤣mwasubiri siku ziishe ndio mwende kuhuisha taarifa zenu.
Nimeenda Jumapili iliyopita sio ya juzi Mlimani City, nikakuta watu kibao. Nikakutana na rafiki yangu aliyekuwa anajisajiri kuwa mteja mpya ili apitishie msahahara uko ila akawa amekaa masaa manne kupata kadi wakati benki jirani KCB alitumia chini ya dakika 10.

Nikatoka MCity nikaenda Magomeni siku nyingine. Pale nikakuta anayehakiki ni mmoja, kuna wamama wameshinda pale jana yake mpaka usiku na wakaambiwa warudi kesho yake. Nikapewa namba 100+ ila nikapima rate ya kuita namba ni mteja mmoja kwa 15 mins, nikaona hata nikae mpaka saa mbili usiku siitwi.

Nikatoka nikatoa hela zote kwenye akaunti wakifungia hamna shida.
 
Nimejaribu kwenda mara kadhaa, Mlimani city branch, Sinza, U/Plaza na pale UDSM, foleni haivumiliki. Nikaishia kujiondokea mara zote.

Nangoja wafunge hiyo account ili tujue kama wao ni benki ya biashara au ofisi ya serikali. Kama wao ni benki ya biashara basi wajue benki ziko nyingi, sioni shida kihamia hata Azania Bank!!

Maana kwa namna walivyoendesha hili zoezi lao la kujinga ni kama wanashindana na taasisi kama NIDA, TANESCO, Ardhi na nyinginezo kwenye kusumbua wananchi kwa huduma mbovu.
 
Kuna benki inaitwa Equity hawa jamaa wako mbele sana ya muda hasa hasa upande wa teknolojia nakumbuka kuna wakati nilpata changamoto ya kadi yangu hasa hasa kuhusu kuhuisha taarifa sikulazimika kufika kwenye tawi lao mambo yote yalifanyika online tu, Nilitamani hata niwape ya soda.

NMB sio vibaya mkaenda kupata semina elekezi pale Equity ili kusudi mjiimarishe kiteknolojia zama za kupanga foleni ndefuuu kupata huduma ni ushamba sana
 
Huwezi kubali kuwa wa Tanzania wengi hivi ni wateja wa NMB, tuliowahi walau hatukuteseka sana,

Tatizo la kuongojea tarehe za mwisho mwisho ndilo limewakumba wengi.

Jana mmama mmoja kapewa namba 370, just imagine.
 
Back
Top Bottom