KERO Zoezi la uhakiki wa taarifa NMB

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Unafuata nini benki ni wasumbufu sana ukipata tatizo la ghafla na pesa zipo benki utalia weka pesa ndani mahali pa siri inakuwa siri yako mwenyewe asijue mtu yeyote na kwenye simu
Pesa zina kaharufu ka pekee watu watajua tu zilipo. Pesa ni tofauti na makaratasi mengine
 
Spendi kupoteza muda Wangu bila sababu nitaenda foleni ikipungua,Hela zangu wao kufanya hivyo Wako kazini wanaingiza mshahara ngoja nami nipambane foleni ikipungua au wakiongeza muda nitahakikiwa
Umesema kweli halafu unakuta mshahara unapitia kwao na una mkopo ili uwalipe lazima mshahara upitie kwao, wanafungaje account yangu. Basi kuwpuka usumbufu huu kushindishwa njaa, kupoteza muda wa kufanya kazi mimi nitakwenda baada ya zoezi kuisha najua nao account yangu wanaihitaji sana tu.
 
Unapata kero kabla hujaenda kuhakiki taarifa zako kwa meseji za mara kwa mara kwenye simu yako.

Ukienda kuhaki unakutana na kero ya utitili wa watu na foleni mtoa huduma ni mmoja tu.

Ukimaliza kuhakiki unapata tena kero yao ya kukutumia meseji za mara kwa mara za kukutaka kwenda kuhakiki ili hali tayari umesha hakiki.

Hivi hiyo mifumo yao inafanyaje kazi..!?
 
Washaniongezea muda hapa, juzi nilipita nje ya branch moja nikaona nyomi nikasepa zangu.
 
NMB na CRDB ni bank za waswahili, zinaendeshwa kiswahili sana.

Hamia Equity Bank au ABSA Bank, utakuja kunishukuru.

kama mkoa ulipo hakuna equity, hamia hata NBC Bank
Kwa watumishi wa Umma wa Serikali hawaepukiki na NMB, CRDB.

Ila kama una hustle zako na hutegemei salary, kuhamia huko ni babu kubwa sana
 
Equity ni wakenya huwezi linganisha na watanzania hata siku moja,jamaa wapo mbali sana.
Leo kuna jamaa wa Equity nimemuuliza kwanini majirani wanawapangisha wateja foleni ili tu kuhakiki na kuupdate taarifa zao?

Akadai majirani hawakuwa wakitumia mfumo wa biometric (Fingerprint), hivyo kwa sasa wanahamia huko, pia kwao National ID haikuwa lazima kwa kipindi hicho.

Ila Equity tangu mteja kufungua A/C lazima fingerprint ihusike.
 
Maswali yao sasa
Umeoa?
Kipato chako kwa mwaka!?
Umewahi kujihusisha na siasa?
Duu hapa wanazingua sasa kwa nini waulize haya maswali personal hivi.

Wanashindwa kujua akaunti inapokea sh ngapi kwa mwaka. Yaani statement za akaunti wanashindwa kuzifanyia analysis.

Ishu ya Siasa, Prezidaa wa TLS kashasema hamna mtu ambaye hajihusishi na Siasa
 
Kama unapitishia mshahara utaenda tu. Baada ya trh 31 zinakuwa temporary closed ili watu wakahakiki. But kutakuwa na usumbufu tu ila permanent close haitatokea kwa account zenye pesa.
Kwahiyo mfano miezi sita usipoenda kuhakiki na account inahela wanakupeleka mahakamani au hela inakua ya kwao
Nchi ya usumbufu kila eneo. Mwenyehela anasumbuliwa na vibaka mtaani akizificha benki napo kila mara kuitwaitwa
 
mimi sijafanikiwa, nahisi kama watafunga account nianze kuhamishia pesa zangu CRDB wiki hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…