KERO Zoezi la uhakiki wa taarifa NMB

KERO Zoezi la uhakiki wa taarifa NMB

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kati ya benki zenye uswahili mwingi na huduma za chini Na RIBA kubwa basi huwezi kuacha kuitaja NMB

Hili zoezi lao la uhakiki ni uhuni mtupu,
Na wanatakiwa kuwalipa wateja hata nauli na posho ya usumbufu..
Hii bank niliachana nayo nilipomalizana na bumu la chuo. Hivi kweli unaenda kupanga foleni kuhakiki taarifa zako kwenye bank ya NMB kwenye nchi yenye banks lukuki?

Reality is: Hii bank inawachukulia powa. Maybe inajua kila customer ni mwalimu na nesi au mfanyakazi wa halmashauri Mpwayungu Village.
 
usip
Zoezi la uhakiki wa taarifa bank ya NMB ni kero kwakweli, foleni ni ndefu kila branch, watendaji hawajipanga, inchukua hadi dk 20 kwa mtu mmoja kuhudumiwa na wahudumu kwa kila branch ni mmoja.

Mara waseme mtandao unasumbua kwahyo mshine inachelewa.

Nimezunguka NMB branch zote Dodoma, msururu wa foleni ni mrefu, uwe umekula umeshiba n uwe n nguvu za kusimama ili kusibiri foleni yako ifike.

Wajipange upya na waongeze muda wa zoezi.
usipo hakiki wanafanyaje? ngoja nikatoe hela zote ili kama wakifunga zibaki kwenye simu.muda wa kukaa kwenye foleni hauko.kama wameshindwa kufanya digal verification basi watuache.
 
Mwezi uliopita nilidhamilia 100%nihakiki,kwa unynyekevu nikasogea tawini,panga foleni nafika tu naambiwa NIDA mtandao unasumbua,zoezi likaishia hapo,naeudi nyumbani niko kwenye harakati nyingine nikaangusha kitambulisho cha NIDA,na hawataki namba wanataka kitambulisho kabisa.

Kwa sababu shida ni yao,nasubiri wafunge hiyo acc nihamishe bank ya kupokelea mshahara maana naona tunasumbuana tu.
 
Kuna benki inaitwa Equity hawa jamaa wako mbele sana ya muda hasa hasa upande wa teknolojia nakumbuka kuna wakati nilpata changamoto ya kadi yangu hasa hasa kuhusu kuhuisha taarifa sikulazimika kufika kwenye tawi lao mambo yote yalifanyika online tu, Nilitamani hata niwape ya soda.

NMB sio vibaya mkaenda kupata semina elekezi pale Equity ili kusudi mjiimarishe kiteknolojia zama za kupanga foleni ndefuuu kupata huduma ni ushamba sana
CRDB pia kadi unaomba juu kwa juu wewe mwenyewe tu utasema kadi utaichukulia tawi gani .
CRDB wako mbele sana sema makato yao sometimes ni ya hovyo
 
Hela yangu nikahakiki? No way
Unaboresha taarifa za kwenye akaunti yako. Eg. Makaazi, kazi, kipato e.t.c. na huwa na agizo la bank kuu. Kuna baadhi ya wateja wanatakiwa kuboresha kila baada ya miaka mitano, wengine mitatu na wengine mmoja tu. Inategea...kila ukiwa assessed km high risk customer ndio unatakiwa uhakiki kila mwaka..mfano kwa wanasiasa
 
Back
Top Bottom