KERO Zoezi la uhakiki wa taarifa NMB

KERO Zoezi la uhakiki wa taarifa NMB

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwamfano hapa nilipo wilaya nzima tawi la nmb ni moja watoa huduma ni kituo kimoja tu,malalamiko makubwa ni wingi wa wateja,pia mtandao kusuasua ,zoezi linachukua dkk 15 hadi 20 kuhakiki mtu mmoja.

Sasa kwa mwendo huko zoezi ni gumu kukamilika kwa wakati mana watu ni wengi foleni ni kubwa na wengi wanaondoka kwa kuchoka kukaa foleni au kuwa na majukumu ya muhmu zaidi.

Ushauri waongeze vituo vya kuhakiki,pia wahakikisha mashine zao zina mtandao wa kutosha..waache kusumbua wateja benki zipo nyingi sana hii kero itawafanya wapoteze wateja.
 
Zoezi la uhakiki wa taarifa bank ya NMB ni kero kwakweli, foleni ni ndefu kila branch, watendaji hawajipanga, inchukua hadi dk 20 kwa mtu mmoja kuhudumiwa na wahudumu kwa kila branch ni mmoja.

Mara waseme mtandao unasumbua kwahyo mshine inachelewa.

Nimezunguka NMB branch zote Dodoma, msururu wa foleni ni mrefu, uwe umekula umeshiba n uwe n nguvu za kusimama ili kusibiri foleni yako ifike.

Wajipange upya na waongeze muda wa zoezi.
Watu mnajua kulalnila,zoezi limetangazwa miezi miwili iliyopita Halafu wote mnaenda siku Nne za mwisho...unategemea Nini! Tuache lawama...,! Wiki mbili nyuma zoezi lilikiwa smooth Kabisa ! Mnawayesa Wafanyakazi wa NMB Kwa uzembe wenu!
 
Huwezi kubali kuwa wa Tanzania wengi hivi ni wateja wa NMB, tuliowahi walau hatukuteseka sana,

Tatizo la kuongojea tarehe za mwisho mwisho ndilo limewakumba wengi.

Jana mmama mmoja kapewa namba 370, just imagine.
shida ni kwamba wateja wao wengi ni waajiriwa. ukiangalia waajiri wengi unakuta wanakwambia kuwa ili upate salary lazima uwe na bank account ya benki fulani uwe unapokelea mshahara. kwa utumishi navyojua huwa ni NMB na CRDB tu unless kama kuna mabadiliko mapya yalifanyika
 
Watu mnajua kulalnila,zoezi limetangazwa miezi miwili iliyopita Halafu wote mnaenda siku Nne za mwisho...unategemea Nini! Tuache lawama...,! Wiki mbili nyuma zoezi lilikiwa smooth Kabisa ! Mnawayesa Wafanyakazi wa NMB Kwa uzembe wenu!
Yaani watu wanapata mateso before deadline, kosa lao ni nini? Kwani wapi ilikatazwa kwenda siku za mwisho? NMB huduma zao ni mbovu hata kusiwe na zoezi la uhakiki, watu ni haki yao kusema ukweli, wewe ndio unatakiwa kuacha kulaumu wanaolalamika.
 
Wametoa miezi miwili,maana yake naruhusiwa kwenda siku yeyote katika hizo siku 60...
 
Hivi tunahakiki ili iweje sasa...??Haya mambo ya kuhakiki physically yaliishapitwa na wakati..wawaze wanachokitaka na wafikiri namna teknologia inavyoweza kusaidia...waty wafanye wakiwa vitandani wametulia.
Yaani akaunti watu wamefungua kwa miaka mingi watu wengi then wahakiki ndani yani ya mwezi mmoja - physically...lazima utokee usumbufu tu...
Halafu kuhakiki taarifa ni kama unafungua mara ya pili akaunti...
 
Watu mnajua kulalnila,zoezi limetangazwa miezi miwili iliyopita Halafu wote mnaenda siku Nne za mwisho...unategemea Nini! Tuache lawama...,! Wiki mbili nyuma zoezi lilikiwa smooth Kabisa ! Mnawayesa Wafanyakazi wa NMB Kwa uzembe wenu!
Wao ni benki ya biashara, sie ni wateja. Wafunge hizo akaunti basi ili tuone nani ameahika mpini na nani ameshika kwenye makali.
 
Yaani watu wanapata mateso before deadline, kosa lao ni nini? Kwani wapi ilikatazwa kwenda siku za mwisho? NMB huduma zao ni mbovu hata kusiwe na zoezi la uhakiki, watu ni haki yao kusema ukweli, wewe ndio unatakiwa kuacha kulaumu wanaolalamika.
Mmeenda wote /wengi siku z mwisho.mnategemea.kisiwe na foleni...Jana nimeona NMB Mkoa Fulani kundi la watu kama 300,Sasa hapo utalaumu Nini
 
Screenshot_20240828-195753_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom