KERO Zoezi la uhakiki wa taarifa NMB

KERO Zoezi la uhakiki wa taarifa NMB

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wanahakiki taarifa ili iweje?

Na kwa nn wafanye hivyo.

Hii benki ya NMB ni wapuuzi sana aisee
Exactly ni wapuuzi. Eti mtu kafungua account hajamaliza hata mwezi una hakiki , una hakiki kitu gani??? Some time nikupotezeana muda tu. Mambo ya kizamani sana .....Nmb badilikeni otherwise mtakosa wateja ....kama mnafanya utafiti watu wengi wana kimbia Nmb kwasababu ya usumbufu
 
Bongo kila siku ni kuchukuliwa finger prints, kila sehemu halafu unaambiwa ni kuhakikisha namba ya nida, sasa finger prints za nini wakati ziko Nida?

Walipaswa watumie watu link waingie kuhakiki taarifa zao, nilienda branch 2 nikakuta ni ujinga kama huo nikaachana na hiyo biashara. Nimeona wamwongeza muda ila sitaenda pia.

Haiwezekani ulimwengu wa sasa unataka niende branch physically?
 
Kwamfano hapa nilipo wilaya nzima tawi la nmb ni moja watoa huduma ni kituo kimoja tu,malalamiko makubwa ni wingi wa wateja,pia mtandao kusuasua ,zoezi linachukua dkk 15 hadi 20 kuhakiki mtu mmoja.

Sasa kwa mwendo huko zoezi ni gumu kukamilika kwa wakati mana watu ni wengi foleni ni kubwa na wengi wanaondoka kwa kuchoka kukaa foleni au kuwa na majukumu ya muhmu zaidi.

Ushauri waongeze vituo vya kuhakiki,pia wahakikisha mashine zao zina mtandao wa kutosha..waache kusumbua wateja benki zipo nyingi sana hii kero itawafanya wapoteze wateja.
Umeshasema wilaya nzima tawi la benki ni moja. Hakuna namna pambaneni na NMB.
 
Zoezi la uhakiki wa taarifa bank ya NMB ni kero kwakweli, foleni ni ndefu kila branch, watendaji hawajipanga, inchukua hadi dk 20 kwa mtu mmoja kuhudumiwa na wahudumu kwa kila branch ni mmoja.

Mara waseme mtandao unasumbua kwahyo mshine inachelewa.

Nimezunguka NMB branch zote Dodoma, msururu wa foleni ni mrefu, uwe umekula umeshiba n uwe n nguvu za kusimama ili kusibiri foleni yako ifike.

Wajipange upya na waongeze muda wa zoezi.
Vijana wa siku hizi hamna ubunifu enzi zetu tulikuwa tunaweka mawe kama foleni kusubiri unga wa Yanga national milling na kwenye kusubiri sukari utafikiri unapewa bure then unaenda kupiga mishe jiwe linakuwa linasogezwa tu no kupoteza muda ukirudi unakuta jiwe lipo namba 2 unakaa dk 2 unahudumiwa unaenda sasa ninyi mnashinda Nyerere square
 
Bongo kila siku ni kuchukuliwa finger prints, kila sehemu halafu unaambiwa ni kuhakikisha namba ya nida, sasa finger prints za nini wakati ziko Nida?

Walipaswa watumie watu link waingie kuhakiki taarifa zao, nilienda branch 2 nikakuta ni ujinga kama huo nikaachana na hiyo biashara. Nimeona wamwongeza muda ila sitaenda pia.

Haiwezekani ulimwengu wa sasa unataka niende branch physically?
Niliwauliza why mnafanya hivi wakasema moja ya kitu hawataki ni kuchukuliana fedha kwenye mashine hivyo soon wataondoa PIN ibaki FP
 
Niliwauliza why mnafanya hivi wakasema moja ya kitu hawataki ni kuchukuliana fedha kwenye mashine hivyo soon wataondoa PIN ibaki FP
Mashine zao zote zina FP Option ama watabadili walete mpya?

Whatever it will be, FP tayari ziko Nida, wanataka nikachukuliwe nyingine za nini?

Lakini pia PIN is the easiest way, FP zina usumbufu sababu ya mitandao yetu. Ngoja tusubiri.
 
Nimejaribu kwenda mara kadhaa, Mlimani city branch, Sinza, U/Plaza na pale UDSM, foleni haivumiliki. Nikaishia kujiondokea mara zote.

Nangoja wafunge hiyo account ili tujue kama wao ni benki ya biashara au ofisi ya serikali. Kama wao ni benki ya biashara basi wajue benki ziko nyingi, sioni shida kihamia hata Azania Bank!!

Maana kwa namna walivyoendesha hili zoezi lao la kujinga ni kama wanashindana na taasisi kama NIDA, TANESCO, Ardhi na nyinginezo kwenye kusumbua wananchi kwa huduma mbovu.
🤣🤣
 
Kuna benki inaitwa Equity hawa jamaa wako mbele sana ya muda hasa hasa upande wa teknolojia nakumbuka kuna wakati nilpata changamoto ya kadi yangu hasa hasa kuhusu kuhuisha taarifa sikulazimika kufika kwenye tawi lao mambo yote yalifanyika online tu, Nilitamani hata niwape ya soda.

NMB sio vibaya mkaenda kupata semina elekezi pale Equity ili kusudi mjiimarishe kiteknolojia zama za kupanga foleni ndefuuu kupata huduma ni ushamba sana
Nitahamia huko
 
Back
Top Bottom