Tetesi: Zoezi la vyeti: 256 kupigwa chini NSSF

Lakini kwa nini serikali haielezi ni lini wataanza kukagua vyeti vya askari waliopo kwenye majeshi yetu wakati huko ndiko kuna balaa zaidi kuliko sehemu yoyote?

Robo tatu watarudisha hm,mtaani hapata kalika
 
Ila mkuu mimi naona ubaguzi wa kidini upo pande zote mbili, wakristo na waisilamu wote wanabaguana tu
Wapo wakristo wanao wabagua waisilamu na hawako radhi kushirikiana nao au kuwaajiri na wapo pia waisilamu wanaowabagua wakristo hivyo hivyo, haya nimeyashuhudia mimi mwenyewe
Hta nchi zenye waisilamu na wakristo wakawa ni minority, ile minority ya wakristo huwa wanakuwa na wakati mgumu sana kutokana na kutoendana kiimani nao hivyo kubaguliwa, ila natumaini haya yataondoka kabisa siku moja
 

Sehemu kama TANROADS sijui ukaguzi utafanyika lini huu
 
Jamani mnachosha vidole vyenu narudia tena now nchii hii inasera ya kubana bajeti pamoja na kupunguza rasilimali watu unapo jidanganya hawa wakifukuzwa mi ndio nitapata kazi unajidanganya nibora uwe na mawazo ya kujiajiri kuliko kuajiriwa utajikuta unazeeka na vyeti vyako mkononi na kama mnabisha mtaona siasa mbaya haya mambo nayajua huwasishabikiagi kabisa
 
Kwani shirika linalokaguliwa vyeti ni nssf pekee?? mengine yote ni masafi na nssf pekee ndo lina wafanyakazi hewa??
 
Mkuu hili naona linaukweli nimetembelea ofisi za NSSF Iringa leo mida ya saa 8 nilikuta milango mingi imefungwa sijui kulikuwa na kikao fikiri hata Mlinzi hakuwepo nadhani walikuwa na kikao, Kwa kweli NSSF nimekuwa siwapendi walikuwa na kiburi na dharau za ajabu hasa wale wa front desks.
 
Watu wanajadili mada ya wafanyakazi vihio we unaleta udini. Maana yake huna reading skills, maana take we pia ukaguliwe vyeti vyako.
 
Zoezi tamu sana hili ..lifanyike taasisi zote ..tena na watu huru kabisaa..kuna madogo wapo kitaa wkt watu wasio na sifa wamekalia vitengo...
 
Mkuu,unao ushahidi usio na hata tone la Shaka kuwa pesa za hilo shirika ndio anazogawa kujengea makanisa??

Ushahidi wa matumizi ya pesa za shirika(kama unavyodai)kujengea kanisa..
Tuanzie hapo..
 
Kumekucha..sasa ni wakati wa kuhesabiana haki. Makanjanja wakipigwa chini kila kona utaona mambo yatanza kwenda vizuri. Tulifika mahali ubaya ukaonekana ndio wema. Ufisadi ukatukuzwa na uadilifu ukadhalilishwa.
 

Shirikisha ubongo sometimes..inaelekea hujui hata shirika la uma ni kitu gani
 

Mfano ni Zanzibar, kanisa la kwanza la Katoliki limejengwa huko na wakristo wazawa wa Zanzaba bado wapo lakini kuna wakristo wangapi kwenye Cabinet?. Hata wa kuteuliwa na President tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…