Zombe aachiwa huru, Mshirika wake ahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Zombe aachiwa huru, Mshirika wake ahukumiwa kunyongwa hadi kufa

km mm ndio Bageni baada ya hapo ni kutoka nduki tuu...bora nipigwe risasi.....ila Zombe kachomoka vp humo??...hawa lengo lao si lilikua moja??
 
Katika vitu ambavyo sitavisahau ambavyo alifanya jk ni hili la kuunda tume ili kuchunguza hakika alinigusa ktk uvungu wa moyo vinginevyo tungeendelea kuaminishwa na polisikuwa hawa wafanyabiashara walikuwa majambazi, lakini swali la kujiuliza ni watanzania wangapi wamepoteza maisha ktk hali kama hiyo ya kusingiziwa na polisi......?
nilikuwa kadato cha tano tukio hilo lililopotendeka kesi iliendeshwa mahakamani kwa mda mrefu baadae nikasikia jamaa yupo huru. familia ya hao wafanyabiashara niliwaona kwenye runinga wakilia sana kwa hukumu ya kuwekwa huru. baadae siku ya pili rais jk alitangaza warudishwe rumande kwa uchunguzi zaidi. ilikuwa jambo zuri mh rais kuingilia vinginevyo haki isingetendeka. god bless our retaired president
 

Yes that is what he meant. He has raised that allegation
 
Ni kweli mkuu. Unajua ten haya mawasiliano yasiyo rasmi. Hata kwenye maungamano ya wale polisi kuna mmoja alinukuliwa akisema ''mkuu amesema wachijwe''. Lakini kwa udukuzi wangu niliofanya issue iko hivi: kipindi hicho kulikuwa na ongezeko la ujambazi wa kutumia silaha hivyo kulikuwa na ''un-written order'' kwa polisi kuto-mess up na mshukiwa yoyote aliyeonekana ni jambazi. Sasa wale marehemu walipokamatwa na kiasi kikubwa cha fedha huku wakiwa na silaha (waliyokuwa wanaimiliki kihalali) hawa polisi wetu kama wasivyopenda kujiridhisha walichukulia kuwa na majambazi. Lakini hata hivyo kuna kitu kimoja kiliwafanya wasipenda kuchunguza zaidi: i.e. zile fedha walizobeba ziliwalevya polisi na kuona kuwa kama wakiwaondoa watakuwa na nafasi nzuri ya kujipatia chochote. Hivyo wakawasiliana na Zombe aliyewapa order ya kuchinja huku akiamini wanachinja majambazi. Sasa hapa unaweza kugundua kuwa huyu mhukumiwa na wenzake hawakupenda kujiridhisha kama ni majambazi kweli au la kwa ajili ya tamaa ya kuchukua zile fedha.
Mkuu hata kama ni majambazi kwanini umuue mtu ambae yuko chini ya ulinzi wako? manake tayari wale victims walishakuwa overpowered.
 
Mkuu
Nivosikia ni kuwa huyu bwana bageni kakutwa na kosa kwa kutoa amri ya kuua ambayo wengne wanahisi kuwa ilitoka kwa zombe ingawa mahakama haijamkuta na hatia mr zombi..ila watekelezaji yaani washikabbunduki wao wako huru kwa ku adhere order from superior in chain of command from mr bageni
mkuu kwa hiyo kumbe sheria inamfunga muamrishaji na kumuacha mshika bunduki? kama ndivyo, basi hata Zombi angehukumiwa kunyongwa...hakustahili kuachiwa huru hata kidogo. hapa lazima kuna jambo limejificha. huenda mahakimu walifanya yao baada ya Zombi kueleweka.
 
ninavyojua na ninavyosikia kuwa endapo jambazi au mateka wowote wale wakitii sheria hawauawi bali wanachukuliwa kama mateka na siyo vingine hii yakuwaua imetoka wapi?
 
Nakumbuka tukio la mauaji lilipotokea, Zombe alitetea sana mauaji ya wale vijana akisisitiza kuwa ni majambazi akaonyesha kwenye TV hata eti silaha walizokuwa wanatumia!!
 
kesi zllizokuwa zimeishiwa kiki, zinaanza kupewa kiki ili kuonyesha fulani anafanya kuliko fulani, UNADHANI KWA UANZISHWAJI HUU WA MAHAKAMA ZA .... halafu sheria za mahakama hizo anatunga fulani na fulani wakiwa sehemu fulani, Ni dhahiri tusubiri suprise toka kwa jamaa yetu. Huwa hawachagui pa kupiga wakikosa kiki ya kutusahaulisha majanga kedekede yanayoendelea bongoland chiniya mwamvuli wa DDN (-1)
Wataanza na ESCROW halafu rader na Yale mengine !!
 
Mkuu hata kama ni majambazi kwanini umuue mtu ambae yuko chini ya ulinzi wako? manake tayari wale victims walishakuwa overpowered.
Ni kweli mkuu. Ndio maana huwa polisi hawarusiwi kuua jambazi labda wawe wanajihami baada ya jambazi kuonyosha kutishia maisha yao. Katika kila washukiwa wa ujambazi 100 wanaokamatwa kuna wengi tu wanakamatwa kimakosa.
 
Mkuu
Nivosikia ni kuwa huyu bwana bageni kakutwa na kosa kwa kutoa amri ya kuua ambayo wengne wanahisi kuwa ilitoka kwa zombe ingawa mahakama haijamkuta na hatia mr zombi..ila watekelezaji yaani washikabbunduki wao wako huru kwa ku adhere order from superior in chain of command from mr bageni

Hukumu hii ni muhimu sana kuisoma. Please mwenye nayo atuwekee
 
Something wrong, murder case rufaa unasikilizia nje?

Basi ndio maana Zombe limepata nafasi ya kukesha kwa waganga.

Ukishinda unaachiwa huru. Rufani unakuwa nje kwa sababu ulishinda kesi.
 
Nani wa ku appeal mkuu..
Wakati anaeshtaki ni jamhuri..kumbuka kuwa wiki moja kabla ya kuhukumiwa yule askari jaji alilalamika kusema serikali imeshindwa kuleta mashahidi na mtaalam wa mlipuko licha yakuwa na rasilimali za kutosha kufanya hivo...
Ujiulize ni kwa kiasi gani upande wa jamhuri haukuwa serious ktk kuitetea haki ya mwangosi
Well said, ila muda ni msema ukweli siku zote, ukweli utadhirika tu muda ukifika, 10, 20 or 30 years bado haki ya mtu itapatikana one day
 
Hatimae Miaka 10 baada ya mauaji yale, Hukumu imetoka japo ina ukakasi kidogo.

Zombe ameachajwe, iannikumbusha movie moja ya Bollywood iitwayo, " Andha Kanoon " yaani Sheria ni kipofu.


Hahahahhaa mkuu kweli Hui Andhaa kanoon (mahakama kipofu/sheria haioni
 
Duniani kuna sheria hamna haki wengi wamefungwa kwa she ria sio haki
 
Mahakama ya Rufaa imemhukumu aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni kunyongwa hadi kufa katika kesi ya vifo vya wafanyabiashara wa madini iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maofisa wenzake wawili.

Katika hukumu hiyo, Zombe na maafisa wengine wawili wameachiwa baada ya kushinda rufani hiyo dhidi yao.

Hukumu hiyo imehitimisha mvutano wa muda mrefu wa kisheria kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na maofisa hao kwani baada ya kimya kirefu hukumu hiyo imetolewa.

Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Hukumu hiyo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu, wakiwamo ndugu wa marehemu hao, wanasheria na jamii kwa jumla baada ya miezi minne, majuma mawili na siku mbili, tangu rufaa iliposikilizwa.

DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaachia huru Zombe na wenzake wanane katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wawili wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teksi, mkazi wa Dar es Salaam.

Katika kesi ya msingi, Zombe na wenzake walidaiwa kuwaua kwa kukusudia wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, aliyekuwa dereva wa teksi wa Manzese.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Agosti 17, 2009, Mahakama Kuu iliwaachia huru washtakiwa hao ikisema baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mawakili wa pande zote iliridhika kuwa hawakuwa na hatia ya mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Badala ya kosa la mauaji ambalo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufaa, DPP aliiomba Mahakama imtie hatiani Zombe kwa kosa la kuwalinda wahalifu, ambao adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka saba jela.

Wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Timon Vitalis alidai DPP alifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani Zombe kwa kosa la mauaji.


Chanzo: HiviSasa Blog

TUNATAKA AKIWA ANANYONGWA TV ZOTE ZIRUSHE LIVE HILO TUKIO ILI TUSHUHUDIE ANAVYO KUFA NA WATU WENGINE WENYE TABIA KAMA ZA BAGENI WAACHE MARA 2. HONGELA MAHAKAM KWA KUTENDA HAKHI.
 
Anaweza fia gerezani hata bila kunyongwa maana wakuu wengi hukwepa kusain hati ya kifo
 
Back
Top Bottom